Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 7,581
- 22,392
Tukio hili lilitikisa taifa zima. Jeshi la Polisi chini ya aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, lilianzisha operesheni kabambe ya kuwasaka wahusika kila kona ya nchi.
Siku nane baada ya uvamizi huo, mnamo Aprili 28, 2006, makachero wa polisi walifanya uvamizi wa kushtukiza nyakati za usiku katika eneo la Sakina mkoani Arusha. Katika operesheni hiyo, walifanikiwa kumnasa mmoja wa watuhumiwa wakuu, Frank Lyatuu, na kukamata mabegi yenye sehemu ya fedha zilizoibwa. Baadaye, watuhumiwa 16 walifikishwa mahakamani, na baada ya kesi iliyodumu kwa miaka mingi, washtakiwa sita walipatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa