Unayosema ni kweli maana hata mie ninaamini kwenye uzoefu na elimu lakini nachotofautiana na wewe inabidi tujue kazi ya chama nini katika kuendesha serikali maana hata kama nchi itachukuliwa na CDM, CUF na CCM watendaji wa serikali wataendelea kuwepo ambao wao ndio kila kitu na wanasiasa kazi yao ni kusimamia sera na ilani ya chama husika kama zinatekelezwa, Tatizo hapa watu wengi wanaangalia mawaziri kama watendaji wakuu kumbe kwa kushirikiana na wataalamu waliopo katika wizara mbalimbali wanatakiwa kuleta mabadiliko kwa kuhakikisha wataalamu wa wizara wanafanya kazi kwa mujibu wa sera. TUMEHARIBIWA NA NAMNA SERIKALI INAVYOFANYA KAZI NDIO MAANA TUNAWAANGALIA MAWAZIRI KWA JICHO LA WATENDAJI WAKUU, MFANO HAPA UNAKUTA KITU AMBACHO ANATAKIWA AONGEE MTAALAMU KAMA MTU WA TANESCO, MKURUGENZI WA HALMASHAURI N.K UNAKUTA WAZIRI NDIO MSEMAJI MKUU MWISHO WA SIKU HATA SIE TUNAANGALIA MAWAZIRI KAMA NI MHIMILI MKUU WA KUTATUA MATATIZO YETU. Nina imani hata CDM wakiingia madarakani wataweza kuongoza tu kwani kinachotakiwa kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wa serikali kuu na mitaa kufanya kazi kwa kujiamini na kuata kanuni bila kuingiliwa kwa issues ambazo ni za kitaalamu. Wizara hata kama uwe nazo 30 au 10 kama hujajipanga haziwezi leta mabadiliko
Nimependa majibu yako, uko makini. Hii unayosema wewe ni kimantiki, kiutekelezaji, mawaziri ndiyo waamuzi wa mwisho wa mambo mengi na ndiyo wanamshauri Rais moja kwa moja. Waziri kumsikiliza katibu mkuu wake, mkuu wa kitengo/vitengo ndani ya wizara ni sawa, lakini waziri kwa uzoefu wake anatakiwa apime na ya kwake alinganishe na sera za chama chake na maslahi ya taifa na kuchukua uamauzi wa mwisho. Na hapa sasa ninakua na wasiwasi na hawa wa CDM katika kufikia decision ya mwisho ambayo haitaumiza taifa wala chama, na kukaa kwenye cabinet kama washauri wa mwisho wa Rais.
Bila ya kua na nidhamu na utaalam kidogo inakua ni vigumu waziri kuoanisha haya kiufasahaa zaidi. Na kiongozi yeyote anayetegemea ushauri kwa kiasi kikubwa sana anapoteza baadhi ya sifa za uongozi na anakua hajiamini. Katika uongozi kuna kuweka dira, kuchukua risk mbali mbali (ukiwa na ufahamu wa kutosha wa faida au hasara zake), na ili kuhamasisha watendaji wako haswa kwenye wizara zenye wataalam wengi na wasomi wengi lazima uheshimika kwa wepesi wako wa kuelewa mambo kama kiongozi wao mkuu, vinginevyo morali itakua chini.