Kumbe CDM hamna Wasomi

Kumbe CDM hamna Wasomi

cdm ina madaktari, wachumi, wanasheria, mawakili, maprofesa, mainjia, yan kila fani muhimu ktk kuongoza nchi

Inao wote hao hivyo i sawa na CCM ,very interesting ,kama utaangalia na kuchunguza kwa makini sasa hivi ndani ya CDM kuna kutafuta umaarufu ,wengi wa wabunge wao tumeona ni jinsi gani wanakiuka taratibu za bunge na kila mmoja anataka awe mkali kumshinda mwenziwe ,hii ni shida ya kuonyesha hakuna kusikilizana au hakuna wa kuwaelekeza ,zaidi kila mmoja anaonyesha anaweza kufanya atakavyo ,hawana mwongozaji.

Uelewe tu sio kila mtoa makelele kwenye hoja na kuchangia pale bungeni kuwa yale anayoyasema kwa kishindo yana ukweli ,ukiamini hivyo na wewe utakuwa unaburuzwa ,ni sawa na kutoa ushahidi wa uongo mbele ya mahakama.

Huu ni ushamba wa uongozi,makelele ,kejeli na kupinga amri si muonekano wa uongozi bora zaidi ya harufu ya udikteta,haya tuyaonayo leo ya viongozi wa CDM kupinga amri za kuitwa na polisi ni ishara mbaya iwapo watu hawa watapata uongozi.

Mwisho wa siku watu hawa wanaonekana vituo vya polisi kwa maana hiyo waliudanganya umma pale waliposema hawataitikia mwito wa polisi au wa kuitwa na vyombo vya dola. Unafikiri watu hawa watakaposhika uongozi wa Tz wataweza kuwajibika ,ikiwa leo hawajapa wanaonyesha kiburi.

Nyota njema huonekana alfajiri ,viburi hivi vya CDM vinavyoonyeshwa pale bungeni na kupinga wito si ishara nzuri za wao kuwa viongozi bora.
 
Fact zipi CCM wangekuwa na wasomi wa kweli sio wa kununua vyeti au waliosoma kweli na kusimama katika principles za usomi na sio kupamba ukuta kuwa nao wana shahada pia Tanzania pamoja na raslimali zote ilizonazo ingekuwa hapo ilipo? Elimu sio lazima uingie darasani ukapate shahada ya uzamili elimu ni ufahamu wa kujua mambo ya kuyatawala mazingira ukatoka katika hali duni na kwenda hali nzuri zaidi. ufahamu huo haujalishi uliupata wapi, kwa njia zipi na katika mazingira yapi ili mradi ufahamu huo unao na umeuonyesha watu wakaona kama ambavyo CHADEMA wameonyesha.

Mfano Kikwete kasoma shahada ya uchumi lakini kiuchumi kathibitisha ni mtupu kiasi kwamba kazidiwa maarifa ya kiuchumi na Mkapa ambaye alisoma habari kwa maana hiyo Kikwete pamoja na kuwa alimaliza shahada ya uchumi shahada yake inaonekana ni ya kupamba ukutani zaidi maana ufahamu wake katika uchumi ni mdogo kulinganisha na Mkapa ambaye hatujui yeye ufahamu wake katika uchumi alipata wapi ili mradi alionyesha ni zaidi ya Kikwete maana elimu haijalishi uliipata wapi na katika njia zipi ili mradi umethibitisha unaweza.

Pia tukumbuke kuna viongozi wamekuwa na kiwango cha elimu cha darasani kidogo sana lakini wameonyesha wanaweza maana wanaufahamu mwingi wanajua wao walikoupata ingawa walikomea madarasa ya chini darasani mfano Jacob Zuma darasa la nne, Lula Da Silva Rais wa zamani wa Brazil darasa la saba, Omar Bongo Certificate, John Major waziri mkuu wa Uingereza Diploma, na wengine wengi. kuhusu wabunge kuwa na elimu ya kawaida haina shida kabisa ili mradi wanakubalika kwa wananchi na wanajua wafanyalo ndio maana CDM inataka mawaziri wasiwe wabunge ili wachaguliwe professionals kushika wizara na sio wanasiasa kama Ngeleja, Maige, Nkullo na Mponda ambao uwezo ni mdogo pamoja na elimu zao za darasani na matokeo ni kuliibia taifa.

mkuu umenena vema. Kama wana uwezo wa kutafakari hata kidogo watakuwa wamekuelewa.
 
kwa nini mnatutafutia ban wengine 2015 huo mdomo wako utaufunga wasomi tz hawatusaidii chochote zaidi ya kunenepesha matumbo yao, huwezi hata siku moja kufananisha jimbo la lema na la huyo anayejiita msomi mwenye degree ya wake za watu
 
Mtoa mada hapa anataka umutoe Shaka Kwamba CDm ni zaidii ya uwazili wa akina sugu,vicent,lema...... Mi naona it's a right time kuvaa gwandaz iLi hofu Itoke...............

Kwa wasiojua:

1. The brightest young brains wenye degree zaidi ya moja wako CDM
2. Kuna professors na Doctorate brains za kutosha.
3. Kuna wenye Diplomas
4. Kuna wenye certificates
5. Kuna form six leavers
6. Kuna Form four leavers
7. Kuna std Seven wenye uwezo mkubwa

Wote hao wako kila kona ya Tanzania wanajenga chama. Nadhani wakuu wa ccm wanaujua ukweli huu ndio maana wanaihofia sana CHADEMA kwa sasa hata kuandaa magaidi kuvuruga mikutano yake.
 
Nawashangaa sana CDM ,wanataka kuongoza Nchi hii ,ukiangalia pale ndani utaona hamna kitu ,hivi wanafikiria wanataka kuongoza kijiji ? Ndio maana unawasikia wataunda serikali ndogo iliyo na mawaziri wachache sana,nikakumbuka pale walipoweka mgombea mwenza jamaa aliehitimi darasa la saba ,na kwa Zanzibar hakuna darasa saba ,inamaana alikimbia shule. eti watategemea washauri ,unategemea washauri wakati nao wanahitaji elimu ya juu.

Hebu tupangieni hapa safu yenu ,tuiite proposed safu ya uongozi ,ukianza na Raisi labda tuseme wizara kumi mpaka kumina tano ,tuone ! na kuwajadili au kuijadili hio safu !

Mimi ndio kabisaaa nakishangaa chama chako kwa udhaifu hadi kufikia hatua ya kukubali kuolewa na chama cha magamba!!!!!!!
 
Mimi ndio kabisaaa nakishangaa chama chako kwa udhaifu hadi kufikia hatua ya kukubali kuolewa na chama cha magamba!!!!!!!

Bora kuolewa kuliko kufanyana mashoga pale bungeni !
 
Hivi wanafikiri kuongoza nchi ni kama kuongoza mkoa? labda watu tukianza kutembea kichwa chini miguu juu ndio tuwape nchi. utampa mtu urais mara kesho anapelekwa mahakamani na waziri mkuu wake, et oh nilipe fidia ulivunja ndoa yetu, sasa hapo nchi itakwenda?
 
mm nadhan ndugu hauhitaji kuwa na woga kuhusu CDM kuongoza nchi kimafanikio. Chadema ina wasomi makinisana na kwa bahati nzuri ni vijana na wazee ni wachache. ukitaka kujua ukweli watafute marafiki na wapenzi wa chama cha CDM


Sasa wewe ndiyo hujui kitu, mbona CCM ina wanachama makini, lakini inaongozwa na wazembe wachache?

CHADEMA kua na wanachama wasomi inaweza kua nao, sikatai, lakini ile safu yao ya uongozi ni tatizo kidogo Kielimu na kiuzoefu wa uongozi na kazi nyinginezo. Taifa kubwa na gumu hili CHADEMA wasifikirie kukosoa makosa yanayoonekana ni kujitayarisha kwa uongozi.

Hata mimi siyo mwanasiasa nayaona haya makosa, yako obvious na hii hainifanyi mimi kua Rais wa tz 2015 bila uzoefu wala elimu tosha.
 
Kwa wasiojua:

1. The brightest young brains wenye degree zaidi ya moja wako CDM
2. Kuna professors na Doctorate brains za kutosha.
3. Kuna wenye Diplomas
4. Kuna wenye certificates
5. Kuna form six leavers
6. Kuna Form four leavers
7. Kuna std Seven wenye uwezo mkubwa

Wote hao wako kila kona ya Tanzania wanajenga chama. Nadhani wakuu wa ccm wanaujua ukweli huu ndio maana wanaihofia sana CHADEMA kwa sasa hata kuandaa magaidi kuvuruga mikutano yake.

Masters nafikiri ni Zitto na Lissu (warwick pongezi zake pamoja na kwamba baada ya hapo hakufanya kazi za maana kama wanasheria wenzake waliomaliza top 10 law schools za UK). Huku Zitto hakiwa hana uzoefu mkubwa wa kuajiriwa

Mbowe, secondary
Slaa, Phd ya dini (useless)
Mnyika..hana elimu ya kutosha, hana uzoefu wa kazi
Wenje. BA sijui ya nini, former head teacher
Mch Msigwa, elimu ya chini ya dini, hana uzoefu wa kazi
Ndesamburo, certificate, uzoefu binafsi ni mkubwa*
Lema, secondary/certificate, uzoefu hamna kitu
V. Nyerere, form 4, uzoefu hamna

Kwa kifupi hawa ni basdhi wa watu muhimu kwenye chama na mawazo yao yanaheshimika kwa hiyo kwenye serikali ya CDM watahusika sana na sera na dira ya serikali na taifa kwa kiasi kikubwa.

Hivi mnategemea hawa watafanya nini, au wataanzisha think tank ya kuwasaidia kufikiria na kufikia maamuzi yenye busara ya kitaifa yasiyo na athari mbaya za muda mrefu? Hawa watu ukimtoa labda Zitto, Lissu na Ndesamburo (kwa uzoefu wake wa siku nyingi katika shughuli zake binafsi na elimu ya wakati ule ilikua nzuri kulinganisha na hii ya waliyosoma akina Zitto) Sioni kabisa timu makini hapa ya kutatua matatizo yetu na kwa hulka za kakikundi haka hawatawapa nafasi wananchama wa kawaida wenye uzoefu na wasomi kuingia kwenye maamuzi ya juu.

Lazima tuwe makini, hawa wanahitaji uzoefu zaidi, Tanganyika haiko tayari kwa hawa watu kuja kujaribu kazi.
 
mwanamutapa...tunajua kua Sokoine na Mrema walikua katika historia yetu kama effective leaders, si ndiyo? lakini kwa nini katika muda tofauti tofauti walienda kuongeza elimu?

Uongozi kuna technicalities nyingi ambazo zinahitaji kujua angalau mambo fulani fulani ili uamuzi wako wa busara utumike na siyo kushauriwa tu kila kitu. Vile vile elimu ni nidhamu, na uongozi bila nidhamu ni hamna kitu.

Ningekubali angalau kidogo kama watu hawana elimu lakini wana uzoefu mkubwa kwa sababu uzoefu mkubwa unajifunza makosa ndani yake na unajifunza mambo mengi mengine ya kitaalam na kinidhamu ya uongozi na utawala...hawa watu wa CHADEMA wengi hawana elimu na uzoefu pia hawana.

Kumbuka hatuna taasisi zenye nguvu za kitaifa zenye za kuja kuwabana hawa watu pindi wakishika dola na wakianza kujaribu jaribu na kuunga unga kazini, hatuna. Na hapa inabidi tuwape muda zaidi na siasa na uongozi bungeni kwanza, kabla ya kuwapa taifa letu.
 
Tuambie kwanza hao Wasomi wa Ccm wenye Mawaziri zaidi ya 50 kina Ngeleja,Maige na Lowasa wamelifanyia nini Taifa letu zaidi ya Ufisadi.
 
WaTz ndani na nje ya nchi ,kweli wapo tena wengi sana,ila hawa hawawezi kukubalika kushika nafasi za uongozi kama za Uraisi na mawaziri wake ,haiingii akilini ,mimi hapa napigana na chama tawala kufa kupona nadhalilika mitaani nanyanyasika bungeni halafu tunaibuka kidedea unamtoa mtu ulaya aje kuwa waziri ,naona kitanuka.

Karume hakusoma baada ya Mapinduzi ,wengi walimfuata kudai wadhifa akawambia haiwezekani kumtoa mtu kijijini akaendeshe meli akimaanisha kwamba si kila mtu anaweza kuwa kiongozi kuongoza serikali.

Jambo moja nitalikubali ikiwa Raisi anaweza kumchagua mtu yeyote yule ambae pengine si wa chama chake,sio mbunge kuwa waziri wake ,hapo mnaweza kuwategemea hao WaTz watakaoweza kusaidia kulisukuma gurudumu la maendeleo.

Ila kwa ninavyoiona CDM ndani ya nchi yetu na jinsi walivyo viongozi walio mstari wa mbele katika chama hiki ambao tegemeo lao na waongozwa ni kwa wao kutoa Raisi na mawaziri,sioni kama kitatosheleza ngazi nilizohitaji kupangiwa safu(proposed)

Hoja yako nzuri lakini umeangalia zaidi bunge la sasa ambalo lina wabunge wa CDM ambao kwa idadi yao hawawezi kuunda serikali, kwa kuwa hoja yako ni kuunda serikali maana yake kwa idadi ya majimbo iliyopo maana yake hapa unafikiria 2015 na sio sasa which means kama wataunda serikali maana yake watakuwa na wabunge zaidi ya nusu ya wabunge wote (kuanzia wabunge 150) which means lazima wasomi watakuwepo plus hapo nilipo bold nimekupa like maana nikiangalia wananchi wengi huku uraiani kuna wasomi pia CDM wanaungwa mkono hivyo kuna uwezekano wakawa included. Naomba kuwakilisha hoja ndugu Mwiba kwani navyoona wewe umeangalia wakati huu ambapo CDM haina wabunge wa kutosha na serikali imeshaundwa na hujaangalia kama chama kina watu gani ambao watakuwa mtaji kwa 2015
 
Last edited by a moderator:
Masters nafikiri ni Zitto na Lissu (warwick pongezi zake pamoja na kwamba baada ya hapo hakufanya kazi za maana kama wanasheria wenzake waliomaliza top 10 law schools za UK). Huku Zitto hakiwa hana uzoefu mkubwa wa kuajiriwa

Mbowe, secondary
Slaa, Phd ya dini (useless)
Mnyika..hana elimu ya kutosha, hana uzoefu wa kazi
Wenje. BA sijui ya nini, former head teacher
Mch Msigwa, elimu ya chini ya dini, hana uzoefu wa kazi
Ndesamburo, certificate, uzoefu binafsi ni mkubwa*
Lema, secondary/certificate, uzoefu hamna kitu
V. Nyerere, form 4, uzoefu hamna

Kwa kifupi hawa ni basdhi wa watu muhimu kwenye chama na mawazo yao yanaheshimika kwa hiyo kwenye serikali ya CDM watahusika sana na sera na dira ya serikali na taifa kwa kiasi kikubwa.

Hivi mnategemea hawa watafanya nini, au wataanzisha think tank ya kuwasaidia kufikiria na kufikia maamuzi yenye busara ya kitaifa yasiyo na athari mbaya za muda mrefu? Hawa watu ukimtoa labda Zitto, Lissu na Ndesamburo (kwa uzoefu wake wa siku nyingi katika shughuli zake binafsi na elimu ya wakati ule ilikua nzuri kulinganisha na hii ya waliyosoma akina Zitto) Sioni kabisa timu makini hapa ya kutatua matatizo yetu na kwa hulka za kakikundi haka hawatawapa nafasi wananchama wa kawaida wenye uzoefu na wasomi kuingia kwenye maamuzi ya juu.

Lazima tuwe makini, hawa wanahitaji uzoefu zaidi, Tanganyika haiko tayari kwa hawa watu kuja kujaribu kazi.

Unayosema ni kweli maana hata mie ninaamini kwenye uzoefu na elimu lakini nachotofautiana na wewe inabidi tujue kazi ya chama nini katika kuendesha serikali maana hata kama nchi itachukuliwa na CDM, CUF na CCM watendaji wa serikali wataendelea kuwepo ambao wao ndio kila kitu na wanasiasa kazi yao ni kusimamia sera na ilani ya chama husika kama zinatekelezwa, Tatizo hapa watu wengi wanaangalia mawaziri kama watendaji wakuu kumbe kwa kushirikiana na wataalamu waliopo katika wizara mbalimbali wanatakiwa kuleta mabadiliko kwa kuhakikisha wataalamu wa wizara wanafanya kazi kwa mujibu wa sera. TUMEHARIBIWA NA NAMNA SERIKALI INAVYOFANYA KAZI NDIO MAANA TUNAWAANGALIA MAWAZIRI KWA JICHO LA WATENDAJI WAKUU, MFANO HAPA UNAKUTA KITU AMBACHO ANATAKIWA AONGEE MTAALAMU KAMA MTU WA TANESCO, MKURUGENZI WA HALMASHAURI N.K UNAKUTA WAZIRI NDIO MSEMAJI MKUU MWISHO WA SIKU HATA SIE TUNAANGALIA MAWAZIRI KAMA NI MHIMILI MKUU WA KUTATUA MATATIZO YETU. Nina imani hata CDM wakiingia madarakani wataweza kuongoza tu kwani kinachotakiwa kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wa serikali kuu na mitaa kufanya kazi kwa kujiamini na kuata kanuni bila kuingiliwa kwa issues ambazo ni za kitaalamu. Wizara hata kama uwe nazo 30 au 10 kama hujajipanga haziwezi leta mabadiliko
 
Tuchukulie mfano tu kwa baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya kwanza kwa upande wa elimu na baraza la mawaziri la awamu ya pili mpaka ya sasa tuone contribution ya wasomi kwa mambo mbalimbali. Wale walithubutu kuweka nadharia kwenye vitendo na mtu akichemsha anaondolewa na kulikuwa hakuna mikataba ya ajabuajabu ambayo imesababisha hasara kama sasa na issue kibao ambazo kwa sasa zimeshindikana kama mashirika kama ya reli, ndege na mengine yalikuwa yanafanya kazi vizuri na mitaala ya elimu ilikuwa nzuri sana tofauti na sasa kila siku mabadiliko na hakuna tija na bado elimu ya mawaziri wengi ilikuwa si kubwa kama ya sasa. Kinachotakiwa hapa ni maadili tu na watu kufanya kazi kwa mujibu wa sheria
 
Unayosema ni kweli maana hata mie ninaamini kwenye uzoefu na elimu lakini nachotofautiana na wewe inabidi tujue kazi ya chama nini katika kuendesha serikali maana hata kama nchi itachukuliwa na CDM, CUF na CCM watendaji wa serikali wataendelea kuwepo ambao wao ndio kila kitu na wanasiasa kazi yao ni kusimamia sera na ilani ya chama husika kama zinatekelezwa, Tatizo hapa watu wengi wanaangalia mawaziri kama watendaji wakuu kumbe kwa kushirikiana na wataalamu waliopo katika wizara mbalimbali wanatakiwa kuleta mabadiliko kwa kuhakikisha wataalamu wa wizara wanafanya kazi kwa mujibu wa sera. TUMEHARIBIWA NA NAMNA SERIKALI INAVYOFANYA KAZI NDIO MAANA TUNAWAANGALIA MAWAZIRI KWA JICHO LA WATENDAJI WAKUU, MFANO HAPA UNAKUTA KITU AMBACHO ANATAKIWA AONGEE MTAALAMU KAMA MTU WA TANESCO, MKURUGENZI WA HALMASHAURI N.K UNAKUTA WAZIRI NDIO MSEMAJI MKUU MWISHO WA SIKU HATA SIE TUNAANGALIA MAWAZIRI KAMA NI MHIMILI MKUU WA KUTATUA MATATIZO YETU. Nina imani hata CDM wakiingia madarakani wataweza kuongoza tu kwani kinachotakiwa kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wa serikali kuu na mitaa kufanya kazi kwa kujiamini na kuata kanuni bila kuingiliwa kwa issues ambazo ni za kitaalamu. Wizara hata kama uwe nazo 30 au 10 kama hujajipanga haziwezi leta mabadiliko
Mkuu kama ajakuelew atakuwa tu mtoa mada is politically biased umeeleza vizuri sana
Jingine mbona hajiulizi 2005-2010 kulikuwa na wabunge watano tu wa kuchaguliwa na sasa wapo zaidi ya 20.
Hafahamu 80% ya wafanyakazi wote wameshavua magamba toka enzi za kuiotwa mbayuwayu?
Kuongoza nchi si uwaziri na usomi ni hekima na busara za wasimamizi wa sera
Mbona hao maprofesa wanaongoza vyuo matatizo ya vyuo hayaishi na migomo inaendele kila mwaka?
Profesa Mlacha,Mukandara na wengineo ni malehimani?Mbona hawajaweza kumaliza matatozo ya wanachuo?
Chochote kitatokea 2015 CDM wakichukua nchi mi sitashangaa kwani wamekaa nje ya ulingo muda mrefu wanaangalia mchezo wataweza tu kurekebisha mapungufu ya MAGAMBA ambayo hata kamam watapata miaka 100 hakuna jipya ambalo wanaweza kulifanya
WAKUBALI TU WAMESHAEEKA NA ZAMA ZAO ZIMESHAISHA WAWAPISHE WENGINE
 
Tatizo huyu jamaa ndugu yangu master gland alikuwa anaangalia wakati huu uliopo wakati point yake ni ya miaka ijayo, yeye anaamini siku CDM wakiunda serikali watakuwa na idadi hii hii.
 
Last edited by a moderator:
Chademu walisimamisha mgombea mwenza wa Urais darasa la saba, ilhali wao hivi sasa wameshasahau na kuanza kuwakejeli akina Prof. Maji Marefu. Sioni hoja yako ni nini? au kwa nini unajibu post isiyohusu.. #goingincycles

Mkapa did though hatch grand theft and corruption, sijui nayo alisomea wapi? au ndo uchumi wenyewe? recipe ya maendeleo naona bado hujaijua.


Umuhimu wa kuwa viongozi wenye elimu na ufahamu wa kutosha hauwezi kuwa overemphasized zaidi ktk nchi yetu kwa sababu mfumo wetu unawapa hawa madaraka ya kuamua mambo yote ya msingi. Japo binafsi sipendezewi na utaratibu huo lakini ndio hali halisi. Kama SA na wengine waliweza, wamebahatika pengine, lakini hatuwezi kushusha standards kwa visingizio vyovyote vile. Mwakilishi wa wananchi kuanzia ubunge na kuendelea lazima awe amefuta ujinga walau ktk ngazi ya stashahada au shahada, hiyo haikwepeki tena ktk zama hizi.

Kiuchumi utalinganisha Mkapa na Kikwete? under what criteria? kuanzia inflation, unmployment rate? social services? unachekesha utafikiri huishi Tanzania? na kama shahada zingehitajika mtu kuwa mbunge basi Marekani na ulaya wangeanza na huo utaratibu maana wanawasomi zaidi kuliko Tanzania lakini hawajasema mwakilishi awe na shahada walichosema wao kiongozi awe muadilifu yaani mwenye ethics na pia kubadili vyama madarakani ili watawala wasijisahau hiyo ndio demokrasia sio kauli mbiu zisizo na ufumbuzi wa matatizo bali zilizojaa ujinga za kusema tumethubutu, tumejaribu, tumeweza ujinga mtupu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom