HATUA SITA ZA MAUMIVU YA HISIA:
Elizabeth kubler Ross daktari wa AKILI na Mtafiti wa Saikolojia ya huzuni na vifo,baada ya kufanya utafiti wa kina alikuja na hitimisho kuwa,Mtu hupitia hatua kuu 5 za hisia kabla ya kurudi kwenye hali ya kawaida.
Brian Tracy katika kitabu chake cha "Believe It to Achieve It" aliongeza hatua moja ya mwisho na hivyo kufanya ziwe hatua 6.
1.Kukataa-(Denial Stage)
Mtu hukataa ukweli anakuwa kama haamini kilichotokea🤔taarifa mbaya kama za msiba,kufukuzwa kazi au kuachwa kwenye mahusiano,mwanzoni unakuwa hataki kukubali kilichotokea.
2.Hasira-(Anger Stage)
Hapa hisia za lawama na kukasirika huanza kutokana na kilichotokea.
Kwanini nifukuzwe kazi?
Kwanini nifiwe na mtu muhimu?,Kwanini niachwe?.
Kwanini mimiiii!! n.k katika hatua hii mtu huongea kauli zenye ukali na utata sana.
3.Kujadiliana-(Bargaining stage)
Mtu huanza kufanya mazungumzo ya kihisia na nafsi yake kuhusu kilichotokea,Huanza kujifariji na kujipa matumaini "Nikipata kazi nyingine sitafanya makosa"
Nikipata mpenzi mwingine...n.k
4.Huzuni Kali-(Depression Stage)
Hii ni hatua ya maumivu ya ndani ambapo mtu hukubaliana na ukweli kwa uzito na hisia kali za kukataa tamaa ya maisha.
-Ni kama vile unakuwa
huoni mwanga tena mbele unapoteza matumaini wengine hujifungia chumbani na kulia tu😥
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa.. Katika hatua hii ndipo wengine huchukua maamuzi magumu ya kujiua.
Ili kuepuka madhara makubwa katika hali hii inashauriwa.
1️⃣Ujichanganye na watu wengine.
-Usipende kukaa muda mrefu ukiwa mwenyewe.
2️⃣Tafuta mtu unayemwamimi umshirikishe hali unayopitia.
Kisaikolojia hii inasaidia mno.
5.Kukubali-(Acceptance stage)
-Mtu hukubaliana na kilichotokea na kuanza kuona uhalisia wa maisha na kusonga mbele.
6.Kujijenga upya-(Resurgence stage)
Hii ni hatua ya nguvu mpya mtu huinuka tena akiwa na uelewa, hekima na mwelekeo mpya wa maisha.
Kumbuka:
Nyakati ngumu hazikupi maumivu tu bali zinakujenga na kukufanya uwe imara zaidi,Baadhi ya watu huchukua muda mfupi kupita katika hatua hizo
hadi kurudi kuwa sawa na wengine hutumia muda mrefu sana.
Je wewe unatumia muda gani?🤷
Niambie kupitia reaction.
❤️=muda mfupi.
😥=Muda mrefu.
-The Power Is Within You-
💥🫵
(Yona Morice Yona)