JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

🌅 UJUMBE WA ASUBUHI YA LEO | IJUMAA, 13 NOVEMBA 2026

Usiianze siku yako kwa kuhofia mambo ambayo bado hayajatokea. Anza kwa kushukuru kwa uhai, kuamini uwezo wako na kuwa na matumaini kwamba mambo yanaweza kuwa mazuri kuliko jana.

Kumbuka, si kila jambo litakwenda kama ulivyopanga, lakini hilo halimaanishi kwamba siku yako imeharibika. Wakati mwingine kuchelewa si kushindwa, kukataliwa si mwisho wa safari, na changamoto si ishara kwamba huna uwezo.

Leo jipe nafasi ya kujaribu tena. Usijilinganishe na wengine, usijilaumu kwa makosa ya jana, wala usikubali mawazo hasi yakupokonye amani yako.

Maneno ya kujiambia leo:

* Nina uwezo wa kukabiliana na changamoto za leo.

* Nina thamani, hata kama si kila mtu anaitambua.

* Nitaendelea kujifunza na kukua.

* Sitakata tamaa kwa sababu ya changamoto za muda mfupi.

* Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, nina matumaini ya kesho iliyo bora.

🌿 Kumbuka: Jana imepita, kesho bado haijafika. Leo ndiyo nafasi yako ya kufanya jambo lenye maana.

Amka, shukuru, tabasamu na endelea kupambana. Maisha bado yana nafasi nyingi za kukushangaza kwa mazuri.

Ijumaa njema! 🤲❤️
 
usisahau leo ni siku ya birian mbuzi,, utaniijia au nikufate mwenyew?
 
Nimefungua uzi huu kutokana na kuwa na janga la kukata usingizi usiku. Kama na wewe ni mmojawapo naomba tuungane pamoja hapa kwa kuandika ulipo na unafanya nini kwa wakati huo baada ya kukosa usingizi.

Muda wa jukwaa ni kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 asubuhi. Mimi hapa leo tangu nimeamka nimeamua KUFANYA IBADA Tuuuu!
Uzi wako umetimiza miaka 10 juzi

Muda unakimbia sana
 
-Kuna msemo maarufu wa kiafrika ambao unasema kuwa "Let the young man go and hunt the elephant, if he kills it he will avoid poverty and if the elephant kills him he will also avoid poverty"

Ukimaanisha kuwa... "Mwache kijana akawinde tembo, akimuua atauepuka umasikini, na kama yeye ndio akiuliwa na tembo basi atakuwa ameuepuka umasikini pia"

Hii ina maana gani katika maisha?
-Maisha yana hadithi nyingi za kupata na kukosa jambo la msingi ni kuelewa kuwa mafanikio makubwa yanahitaji uthubutu mkubwa, bila kuthubutu hakuna mafanikio makubwa utakayoyapata.

-Watu wengi wanabaki wakiishi maisha duni kwasababu ya hofu ya kushindwa, wanasahau kuwa kushindwa ni ishara kwamba unajaribu.🤷

Hata hivyo...
-Steven Pressfield, Mwandishi na mtaalamu wa mambo ya mafanikio katika kitabu chake cha "The War of Art" anaeleza kwa kina kuwa kila ndoto kubwa hupingwa na hofu ya ndani, lakini siku zote ushindi huwa upo kwa wale wasiokata tamaa na kuendelea kusonga mbele.

-Bila kujali ni fursa ngapi zimekupita kwasababu ya hofu ya kushindwa amini kwa uthabiti 🎯 kuwa unaweza kufika viwango vya juu.

-Tembo wako anaweza kuwa ni biashara ambayo unaogopa kuanza, inaweza kuwa ni kazi,mradi au ndoto yako kubwa ambayo kila wakati unahofia kuchukua hatua, leo inuka tena, simama ukamuwinde tembo wako.

-Kumbuka kuwa,mara nyingi hatima ya mafanikio yetu huwa iko kwenye maamuzi muhimu tunayoyaogopa.
-The Power Is Within You-
✨🫵🏅

(Yona Morice Yona)
 
Mel Robbins....
Ni mwandishi na mtaalamu wa maendeleo binafsi Katika kitabu chake cha "The 5 Rule Second" alieleza jambo la msingi sana kuwa.

Watu wengi huwa hawashindwi kwasababu hawana uwezo,bali kwasababu ya kusubiri muda sahihi wa kuanza.

Robbins anasisitiza kuwa....
Mara nyingi hatua ya kwanza ndio inayotengeneza ujasiri wa kusonga mbele💪

Ukweli ni kuwa hakuna siku ambayo kila kitu kitakuwa tayari kwa asilimia zote 100%,Unachotakiwa kufanya ni kuanza.

Tafiti nyingi za kisaikolojia zimebaini kuwa kadiri unavyoahirisha kufanya jambo muhimu ndivyo akili yako inavyozidi kuliona gumu zaidi.

Kumbuka kuwa....
Ulizaliwa ukiwa ORIGINAL usisubiri kuondoka duniani ukiwa COPY🤷

Leo acha kuendelea kusubiri hadi ujisikie kuwa tayari,Anza tu na ulichonacho hata kama ni kidogo.

Hatua ndogo unayoichukua leo inaweza kuwa mwanzo wa mafanikio makubwa kesho.

Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie mtu mmoja tu unayemthamini ili tuendelee kujifunza zaidi ✨📚
-The Power Is Within You-
🫵 💥

(Yona Morice Yona)
 
Wakati mwingine tunachohitaji ni kuamua kuanza tu na the rest inakuwa ni history​

Tukumbuke hata safari ya kilomita 100 huanza na hatua moja wadau wangu

Tuanze sasa na tusisubiri kila kitu kiwe tayar kwa asilimia mia moja,hakutakuwa na kitu kama hicho
 
Back
Top Bottom