JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

Usipokuwa makini kauli hizi zitakuchelewesha sana kutimiza malengo yako:

1."Nitaanza kesho"
-Kesho isiyo na hatua hubadilika kuwa wiki,mwezi na hatimaye mwaka utaisha.

2."Nasubiri kwanza hadi mambo yakae sawa"
-Hakuna siku ambayo kila kitu kitakuwa sawa kwa asilimia 100%,kama kuna jambo lolote muhimu unalopaswa kufanya anza leo.

3."Nasubiri hadi nipate mtaji mkubwa"
-Pesa haijawahi kutosha,anza tu na hicho hicho kidogo ulichonacho, kwasababu huwezi kukua kwa kudharau ulichonacho bali unaweza kukua kwa KUKUZA ulichonacho.

4."Bado sijawa tayari"
-Anza kisha hamu ya kuendelea itakuja ukiwa tayari umeshaanza.

-Hakuna siku ambayo utajisikia utayari wa kuanza kwa asilimia zote 100%,kwasababu kuchukua hatua sio hisia ni maamuzi🤷

-Siku zote kumbuka kuwa, HAMASA itakusaidia kuanza tu ila NIDHAMU ndio itakufanya uendelee.

-Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie mtu mmoja unayemthamini ili tuendelee kujifunza zaidi 📚🧠
-The Power Is Within You-
✨💪


(Yona Morice Yona)
 
Ili kuyafurahia mafanikio yako lazima ujali na kuitunza afya yako:

Chuo kikuu cha Michigan kilichopo nchini Marekani 🇺🇸 kiliwahi kufanya utafiti kuhusu nani huwa anachukua hatua za haraka kufanya matibabu ya kiafya kati ya mwanamke na mwanaume.

-Baadae majibu ya utafiti huo yalichapishwa kwenye Jarida la Journal of Men's Health na kubaini kuwa wanaume wengi sana huwa hawachukui hatua mapema kujua afya zao.

-Huwa wanajikaza na kuvumilia ili kuonyesha ujasiri na kuepuka kuwatia wasiwasi watu wanao wategemea na hivyo kuzidi kuhatarisha afya zao zaidi😢

-Aidha kwa upande wa wanawake utafiti huo ulibaini kuwa idadi kubwa ya wanawake huwa wako makini mno na huwa wanachukua hatua haraka sana pale tu wanapojihisi hawako sawa kiafya.

-Hata hivyo Mahatma Gandhi, mpigania uhuru na mtaalamu nguli wa mambo ya sheria kutoka nchini India aliwahi kusema kuwa "If you don't care about your health, you don't care about your destiny"

Akiwa na maana kuwa..
"Kama haujali kuhusu afya yako, basi haujali kuhusu hatima yako"🤷 Hii maana yake ni kuwa ili kuyafurahia mafanikio yako ni lazima uijali na kuitunza sana afya yako.

-Kwasasabu bila afya bora unaweza kuwa na mafanikio makubwa sana lakini usiyafurahie, kuna watu kila siku wanapambana sana kutimiza malengo yao ila hawajali kabisa kuhusu afya zao.

-Inawezekana hata wewe🫵 umekuwa hujali afya yako kwa muda mrefu, Lakini kuanzia leo amua kubadilika na kujipenda upya usisubiri hadi uzidiwe ndipo uchukue hatua kwasababu mafanikio yako yanaanza na ubora wa afya yako.
-The Power Is Within You-
✨💪


(Yona Morice Yona)
 
Utachelewa sana kufika unakoelekea, kama utasimama kurusha mawe kwa kila mbwa anayebweka.

Hii maana yake ni kuwa....
-Huwezi kuyafikia mafanikio makubwa unayoyataka kama utasimama kupambana na kila kelele unazozisikia juu yako🤷

-Dunia ina watu wengi sana watakao kupinga,kukukosoa na kukukera kuliko wanaokutia moyo na kukupa hamasa ya kusonga mbele.

-Usisahau kuwa kuna siku utaumizwa sana na kutaka kukata tamaa,jambo la msingi ni kuwa USIRUDI NYUMA wala kubakia chini.

-Kwasasabu shujaa wa kweli ni yule anayechagua kusonga mbele 🚶hata pale mazingira yanapo mlazimisha kukata tamaa.
-The Power Is Within You-
💥 🫵

(Yona Morice Yona)
 
Mwandishi na mtaalamu nguli wa mambo ya uongozi JOHN MAXWELL,

-Katika kitabu chake cha "Success Is The Choice" alieleza jambo muhimu sana kuhusu maisha na mafanikio kuwa....

-Mafanikio yanahitaji hatua sio mipango pekee,miongoni mwa chaguo muhimu kuelekea kwenye mafanikio yako ni "initiate action" yaani "kuchukua hatua"

-Hata hivyo Maxwell anasisitiza kwamba, watu wengi sana wana vipaji na ndoto kubwa za kufika mbali ila wanabaki pale pale kwasababu HAWAANZI🤷

-Ili kufika kwenye viwango vya mafanikio unayoyataka hutakiwi kuendelea kusubiri hadi ujisikie kuwa tayari kuanza kwasababu kuanza sio HISIA ni MAAMUZI🎯

-Anza na kile ulichonacho hata kama ni kidogo, jifunze na uboreshe unachofanya huku ukiwa unaendelea kufanya.

-Siku zote kumbuka jambo hili.
Kipaji kinaweza kukupa mwanzo mzuri sana lakini hatua unazochukua ndizo zinazokufikisha kwenye mafanikio unayoyataka🏅

-Usijiulize "nataka kufanikiwa lini?" jiulize "Ni hatua gani moja tu naweza kuianza leo?" kisha uchukue hatua.
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
-Chuo Kikuu maarufu duniani cha Stanford kilichopo nchini Marekani 🇺🇸 kiliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa.

-Kuandika malengo yako kwenye karatasi 📝 husaidia kuyatimiza kwa asilimia 42% zaidi kuliko kuyawaza tu kichwani.

-Hii ni kwasababu unapoandika malengo yako kwa uwazi na uthabiti 🎯 ubongo wako huacha kuwaza jambo hilo kwa hali ya kawaida.

-Hivyo huchukulia kama ni jambo la kweli nala lazima sana kulifanya, hii huifanya akili yako izingatie zaidi njia za kuyafikia hayo malengo.

Je,wewe huwa unaandika malengo yako? niambie kwenye reaction.
Ndio=❤️
Hapana=😰
 
RISK & COMPLIANCE MANAGER
INDUSTRY: INSURANCE
HR World Limited, on behalf of our client, is seeking an experienced and strategic Risk & Compliance Manager to develop, implement, and maintain the company’s risk management and compliance frameworks. The successful candidate will be responsible for ensuring effective identification, assessment, monitoring, and mitigation of risks while maintaining regulatory compliance, strong corporate governance, effective internal controls, and a strong risk-aware culture across the organisation.

RESPONSIBILITIES:
• Develop, implement, and maintain the Company’s Risk Management Framework.
• Identify, assess, monitor, and report strategic, operational, financial, insurance, and regulatory risks.
• Establish and maintain risk registers and ensure periodic review of key organisational risks.
• Recommend and monitor appropriate risk mitigation strategies to minimise organisational risk exposure.
• Ensure compliance with applicable insurance laws, regulations, and industry requirements.
• Monitor regulatory developments and assess their impact on business operations.
• Coordinate regulatory reporting and submissions and ensure timely compliance with regulatory obligations.
• Advise management on compliance requirements, regulatory changes, and emerging risks.
• Develop and oversee effective internal control frameworks across the organisation.
• Evaluate the effectiveness of policies, procedures, and internal controls and recommend improvements where necessary.
• Support the implementation of corporate governance best practices and ensure compliance with Board-approved policies and risk management standards.
• Conduct compliance reviews and monitoring activities across all departments.
• Investigate compliance breaches and recommend appropriate corrective and preventive actions.
• Track and follow up on the implementation of audit, compliance, and risk recommendations.
• Prepare accurate and timely risk and compliance reports for Executive Management, the Board Risk Committee, and regulators.
• Present risk findings, trends, key exposures, and recommendations to senior management and relevant governance committees.
• Maintain accurate records of risk assessments, incidents, compliance activities, and corrective actions.
• Develop and maintain Business Continuity Management (BCM) and Disaster Recovery Plans.
• Coordinate business continuity testing, simulation exercises, and operational resilience reviews.
• Ensure business resilience measures are regularly reviewed, tested, and updated.
• Promote risk awareness and a strong compliance culture across the organisation.
• Conduct training and awareness programmes on risk management, compliance, ethics, and regulatory requirements.
• Provide guidance to employees and management on risk management and regulatory matters.
• Support fraud prevention and detection initiatives across the organisation.
• Investigate reported compliance violations, fraud concerns, and ethical issues as appropriate.
• Recommend improvements to strengthen fraud prevention, detection, and misconduct controls.
• Promote high standards of integrity, ethical conduct, accountability, and regulatory compliance across the organisation.
• Identify control weaknesses and drive the implementation of appropriate corrective measures.
• Provide strategic advice to management on complex risk and compliance matters and support sustainable business growth and operational resilience.

QUALIFICATIONS:
• Bachelor’s degree in Insurance & Risk Management or a related field.
• Master’s degree in Risk Management, Finance, Insurance, Business Administration, or a related discipline will be an added advantage.
• Certified Risk Management Professional, ACII, CPA, ACCA, or equivalent professional qualification will be desirable.
• Minimum of 3–7 years of relevant experience in risk management, compliance, audit, governance, or insurance operations.
• Minimum of 2–3 years of experience in a managerial or leadership role.
• Experience within a general insurance company or financial services institution is highly desirable.
• Proven experience dealing with insurance regulators and governance structures.
• Strong knowledge of Enterprise Risk Management (ERM) principles.

Interested candidates may send their CVs to career@hrworld.co.tz before 18th November 2026.

“Only successful applicants will be contacted.”
 
🍀 JOB VACANCY | BEYOND BEAUTY NATURALS 🍀

Beyond Beauty Naturals tunapanua timu yetu! Tunatafuta watu wenye ujuzi, uzoefu na moyo wa kufanya kazi kwa nafasi zifuatazo:

1. HAIR STYLIST / MTAALAMU WA NYWELE

Mahitaji:

  • Awe na uwezo mzuri wa kusuka mitindo mbalimbali ya nywele, hasa Natural Hair.
  • Awe na uzoefu wa kazi za saluni usiopungua miaka 2.
  • Awe msafi, msikivu na mwenye nidhamu kazini.
  • Awe mwepesi wa kujifunza na tayari kupokea maelekezo.
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na timu.

2. NAILS TECHNICIAN

Mahitaji:

  • Awe na ujuzi mzuri katika huduma mbalimbali za kucha.
  • Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2.
  • Awe msafi na anayezingatia viwango vya usafi na usalama.
  • Awe msikivu, mwenye nidhamu na mwepesi wa kujifunza.
  • Awe tayari kufundishika na kukua kitaaluma.

📍 MAHALI: Salasala, Dar es Salaam.

📞 MAWASILIANO: 0652696824

📲 Instagram: @beyondbeautynaturals

ZINGATIA:

  • Waombaji wanaoishi Salasala na maeneo ya jirani watapewa kipaumbele.
  • Tunatoa mshahara mzuri kwa mtu mwenye sifa na uwezo unaotakiwa.
  • Tunathamini ujuzi, nidhamu, usafi, kujituma na utayari wa kujifunza.

🍀 Kama una kipaji, uzoefu na passion ya kazi yako, tungependa kukufahamu!

Mwisho wa kupokea maombi: 30/11/2026.

BEYOND BEAUTY NATURALS
Feel Natural, Be Natural. ❤️

 
Habari naomba nipostie hili tangazo

📢 TANGAZO LA NAFASI YA INTERNSHIP

DMP FINANCIAL SERVICES CO. LTD

NAFASI: AFISA MIKOPO INTERN (LOAN OFFICER INTERN)

DMP Financial Services inakaribisha maombi kutoka kwa vijana wenye sifa, ari na nia ya kujifunza kwa vitendo katika sekta ya huduma za kifedha na mikopo.

MAJUKUMU YA INTERNSHIP

1. Kutafuta na kusajili wateja wapya.
2. Kufanya tathmini ya biashara na uwezo wa mteja kurejesha mkopo.
3. Kujaza na kusimamia fomu za maombi ya mikopo.
4. Kufuatilia marejesho ya mikopo kwa wakati.
5. Kufanya ufuatiliaji wa wateja na kuandaa taarifa za kazi.
6. Kujenga mahusiano mazuri na wateja.

VIGEZO VYA MWOMBAJI

  • Awe na umri wa miaka 18–29.
  • Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (Form Four) au zaidi.
  • Awe mwaminifu, mchapakazi na mwenye nidhamu.
  • Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na watu.
  • Awe tayari kufanya kazi za nje ya ofisi.
  • Awe na uwezo wa kutumia simu janja.
  • Awe mwaminifu katika kushughulikia fedha na nyaraka za kampuni.
  • Awe tayari kujifunza na kufuata taratibu za kampuni.
  • Waombaji wasio na uzoefu wa kazi wanakaribishwa.

POSHO NA MASLAHI

  • Posho ya mwezi: TSh 150,000.
  • Malazi: Kampuni itatoa sehemu ya kuishi kwa waombaji watakaotoka nje ya Dar es Salaam.

MAHALI PA INTERNSHIP: Dar es Salaam.

NAMNA YA KUOMBA

Tuma CV yako kupitia WhatsApp:

0723 600 137

Mwisho wa kutuma maombi: 23/11/2026

DMP FINANCIAL SERVICES CO. LTD
 
Kisayansi ni kuwa ili binadamu apatikane:
-Lazima mamilioni ya mbegu zikimbie kuwahi kurutubisha yai ambapo ni mbegu moja tu ndio ilishinda na kufanikiwa kupenya kwenye yai ili wewe uzaliwe.

Hii maana yake ni kuwa, wewe ni mshindi tangu ukiwa kwenye tumbo la mama yako🤷

-Kama ulishinda ukiwa bado uko tumboni hauna sababu yoyote ya kukata tamaa hapa duniani.
-Mungu alikujua mapema mno hata kabla hujazaliwa(Yeremia 1:5)

-Endelea kusonga mbele bila kukata tamaa,dunia inasubiri kuona uwezo wako wa kipekee ambao Mungu aliweka ndani yako💎

-Leo nenda kaanzishe tena ule mradi uliouacha,mpigie simu huyo mtu ambaye kila wakati unaghairisha kumpigia kwasababu ya hofu.

-Jambo lolote lenye manufaa ambalo unafikiria kulifanya usisubiri muda uzidi kwenda zaidi anza leo,kumbuka kuwa ulizaliwa ili uwe mshindi🏅
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
-Wakati mwingine Mungu huondoa watu muhimu kwenye maisha yako ili kukujengea misuli na ufahamu wa kupambana mwenyewe.

-Kuna wakati unafikiri ukiachwa mwenyewe utakufa au maisha hayataendelea kabisa kumbe ndio mwanzo wa wewe kujijua.

-Watu wengine huwa wanakuja kukufundisha tu, siyo kukaa na wewe milele. Mungu akiwaondoa usilie sana kwa kuwapoteza.

-Bali chukua kama funzo kuwa umejifunza,kwani hakuna shujaa bila kuzishinda nyakati ngumu.

-Leo bila kujali nani aliyekuacha, aliyekudharau au anayekupinga,simama tena,maumivu yako ya leo ndio nguvu yako ya kesho.

-Wakati mwingine maumivu hayaji ili kututesa yanakuja ili kutufanya kuwa wapya na kukua zaidi kihisia na kiakili,Mungu akupe uvumilivu na hekima ya kuvuka salama katika hali unayopitia leo.
-The Power Is Within You-
💥 🫵

(Yona Morice Yona)
 
☀️ UJUMBE WA MCHANA

Usikubali changamoto za asubuhi zikupotezee matumaini ya mchana. Bado una nafasi ya kubadilisha mambo, kujifunza kutokana na makosa na kupiga hatua nyingine kuelekea kwenye ndoto zako.

Kumbuka, maisha hayahitaji uwe mshindi kila siku, yanahitaji uwe na moyo wa kuendelea hata pale mambo yanapokuwa magumu.

Usijilinganishe na kasi ya wengine. Kila mtu ana safari yake, muda wake na mapambano yake yasiyoonekana kwa macho.

Jipe moyo, mshukuru Mungu kwa hatua uliyofika na endelea kupambana. Bado kuna mambo mazuri yanakusubiri mbele.

🌿 Mchana mwema. Usikate tamaa, hadithi yako bado inaendelea kuandikwa.
 
Back
Top Bottom