Kwanini wanawake wanapenda kuuliza maswali haya, uko wapi?, unafanya nini?, uko na nani? n.k
Utafiti uliofanywa na watafiti wa saikolojia ya mahusiano kutoka chuo kikuu cha California, nchini Marekani 🇺🇲 kuhusu wanawake ulibaini kuwa.
Wanawake wengi sana huwa wana hofu ya kupoteza kitu wanachokithamini sana (fear of losing/fear of abandonment)
Hali hii husababisha kila wakati awe na wasiwasi ndio maana hupenda kuuliza maswali utasikia uko wapi? unafanya nini? umekula? uko na nani? n.k
Sio kwasababu hakuamini,bali anatafuta tu uhakika (assurance) kwamba bado upo nae, bado unamjali, na bado hajakupoteza.
Aidha kwa upande wa wanaume utafiti huo ulibaini kuwa WANAUME huwa hawapendi kabisaaa! kuulizwa..ulizwa maswali ya aina hiyo kila wakati.
Kwani huona kama wanadhibitiwa na kukosa uhuru, mwanaume anapoulizwa sana.
Ubongo wake huona kama anahojiwa na sio anajaliwa (cared) ndio maana wengi hujibu kwa hasira au kukaa kimya.
-Kama wewe ni mwanamke unayejali sana hakikisha unawasiliana na mwanaume wako kimkakati (Strategically)🧠
-Muulize mambo machache muhimu tu pale inapobidi sio kila wakati uko wapi? mbona hujajibu sms zangu? au ulikuwa na wanawake zako?😁
-Kwasababu kadiri unavyozidisha maswali na kuuliza kila wakati ndivyo unavyomfanya mwanaume huyu awe makini na wewe.
-Kosa kubwa sana ambalo mwanamke utalifanya ni kutaka ku mu "over proctect" mwanaume.
"Kumlinda kupita kiasi" yeye akili yake itaona kama unataka kumtawala🙌😁
-Na hapo ndipo itakapoibuka vita ya tatu ya dunia,utasikia "kwanini unanifatilia?", "Eeeh si nina kuuliza eeh?" inakuwa ni kamzozo!😁
Kwa kifupi ni kwamba!!..
mwanamke ni mtu ambaye anapenda kuuliza ili ajisikie SALAMA na kupata uhakika kuwa bado anapendwa na kuthaminiwa.
-Jambo la msingi ni kuwaelewa tu na kuishi nao kwa hekima.
-The power Is Within You-
🫵🥇✨
(Yona Morice Yona)