Utamkumbuka Samia kwa yapi?

Utamkumbuka Samia kwa yapi?

Inawezekana akafika mwisho wa term yake hapo 2030

Je kuna yapi ambayo wewe unadhani atakumbukwa kwayo.

Yawe mabaya au mazuri

Uwanja ni wako
My friends ladies and gentlemen,

Kwanza kabisa,
taifa litamkumbuka Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kwa ujasiri, uthubutu na umadhubuti wake wa kukubali kuipokea nchi katika mazingira magumu, kuidhibiti, kuipitisha na kuiongoza katika kipindi kigumu cha majonzi na hatari zaidi za usalama kufuatia kifo cha aliekua Rais wakati huo hayati DR JPM. Hapa, Dr Samia Suluhu Hassan alionyesha umahiri wa kiwango cha juu mno katika uongozi wa taifa.

Lakini pia,
hatua ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassan mara tu baada ya kushika hatamu za uongozi wa nchi na kuamua kwa makusudi kabisa, kuifungua nchi miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, na kuliunganisha taifa kwa falsafa ya 4Rs, hakuna mTanzania anaweza kusahau jambo zito na la maana zaidi kama hili.

Zaidi sana,
falsafa za Dr Samia Suluhu Hassan kama "Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee" au "kazi na utu tunasonga mbele pamoja "ni mambo yatakayoishi milele yote miongoni mwa vizazi vya waTanzania.

Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kukamilisha kwa kishindo miradi mikubwa ya kisasa na yakimkakati kama vile treni ya SGR, bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, ujenzi wa zahanati kila kijiji, kukomesha kabisa tatizo la umeme, kuimarika kwa hali ya usalama nchini na kuongeza uwekezaji nchini ni miongoni mwa mambo machache sana kati ya mengine mengi sana yatayokafanya waTanzania kutomsahau Rais Dr Samia Suluhu Hassan maisha yao yote 🐒
 
Ukituambia wewe utamkumbuka kwa lipi itapendeza sana.
Unaliongelea Taifa lipi? Au ndo ile kasumba ya mbogamboga kuwa inamiliki mpaka uwezo wa kufikiria na utashi wa kila raia wa nchi hii?

Swali limenyooka. Sema wewe utamkumbuka kwa lipi liwe jema au baya
 
Gentleman,
upende usipende,
ukasirike au ufure,
but waTanzania wote zaidi ya milioni 70, bila kumuacha hata moja, katika umoja wao, kamwe hawatamsahau Rais na kipenzi chao Dr Samia Suluhu Hassan kwaajili ya hatua hizo kubwa na za makusudi za kimaendeleo alizochukua na kuhakikisha kila mTanzania ana nufaika na kufurahia matunda ya kazi yake njema ya uongozi kama mkuu wa nchi Tanzania.

Ni muhimu kuupokea ukweli huu mtupu bila makasiriko wala mihemko na itapendeza zaidi licha ya tabia ya ukweli kua mchungu na wenye kukera sana.

waambie na wenzako kuhusu jambo hili la kweli bila kificho wala makasiriko gentleman na itapendeza zaidi 🐒
 
Nitamkumbuka kwa kuua watanganyika wasio na hatia tar 29 Oktoba 2025 wakidai mabadiliko ya katiba na tume huru ya uchaguzi.nitamkumbuka kwa kujaribu kumuua Tundu Lissu kwa kumnyonga lakini akashindwa
 
1000824665.jpg
 
Simsafishi...

Ila yanayotokea ni matokeo ya mfumo flani kuendekezwa.

Na bila mfumo huo kuondolewa, mambo kama haya yatajirudia tu.

Wanaharakati wanapotosha watu. Wanamuongelea yeye tu. Tundu Lissu ndo yupo vizuri ameweka wazi tatizo la mfumo mzima.
Hakuna wanaharakati wanaopotosha watu bana kila kitu kipo wazi

Tatizo ndio ni mfumo na yeye yupo sehemu ya mfumo huo hivyo tu
 
Tamkumbuka kwa kuuwa viongozi wote walioonesha kumpinga hasa wa dini ya kikristo...

Nafikiri baada yake sitarajii tutapata Raisi mwingine kutoka Zanzibar...

Maana nafikiri kulelewa kwenye dini moja(uislamu) ndio kunamfanya afikiri kila anayempinga basi ana chuki na dini yake...

Lakini pia namuombea mwisho mwema maana karma ikifanya kazi yake hatakuwa na mwisho mzuri.
 
Inawezekana akafika mwisho wa term yake hapo 2030

Je kuna yapi ambayo wewe unadhani atakumbukwa kwayo.

Yawe mabaya au mazuri

Uwanja ni wako
1: Ameajiri vijana wote wanaomaliza vyuo.

2: Amepeleka maji na umeme kila kijiii na kitongoji Tanganyika nzima.

3: Amewarudisha wamasai waliofukuzwa Ngorongoro na Loliondo.

4: Amekataa mkataba wa bandari wa kampuni ya DP world na kuagiza wanasheria kuupitia upya na kuufuta.

5: Ameondoa ubaguzi wa ajira na amekemea na hataki kuwapendelea Wazanzibar kinyume cha Katiba ya Nchi.

6: Amepiga marufuku utekaji na kuliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi kwa kila Mtanganyika aliyepotea.

7: Ame Ame ame ame nk nk nk nk
 
Kabisa, japo binafsi siamini kama anapaswa kubeba lawama peke yake kwenye masuala ya demokrasia.

Ni hicho chama kizima chenye falsafa za Mao kutoka kwa Nyerere.

WanaCCM wakubwa wanaamini chama kinakuja kabla ya nchi.
Kiongozi wa nchi ana wajibu wa kuweka msingi

Kwenye utekaji na uuaji wa Ally kibao na mauaji ya Oct 29, ni dhahiri kauli zake zilibariki mauaji
Hakuawahi kemea wizi, ufisadi, utekaji, uuaji
 
Simsafishi...

Ila yanayotokea ni matokeo ya mfumo flani kuendekezwa.

Na bila mfumo huo kuondolewa, mambo kama haya yatajirudia tu.

Wanaharakati wanapotosha watu. Wanamuongelea yeye tu. Tundu Lissu ndo yupo vizuri ameweka wazi tatizo la mfumo mzima.
Moy wake ni mchafu ndio maana anatetea kiti CHAKE kwa maslahi yakr hata kama inamaanisha kuua maelfu

Kauli yake kwenye mkutano wa wazee kuwakejeli wafiwa huwezi sema ana utu hata robo
 
Back
Top Bottom