TPDC yaeleza ukweli wa gesi ya Ruvu

TPDC yaeleza ukweli wa gesi ya Ruvu

Hayo mautalamu yenu ya Kiingilishi mnatuchosha wenzenu. "Wire line Logging" "Cross over" "Pressure vs Depth" "Drill stem test" "appraisal Program" na "Location" huo utaalamu hauwezi kuandikwa kwa kiswahili!!?
 
Kama Watanzania hawatamiliki asilimia kubwa katika uvunaji wa rasilimali hizi za Tanzania,basi uwepo wake hautaleta manufaa makubwa kwa Watanzania wenyewe.Dubai,Qatar,Saudia hazikujengwa na Total,Shell wala kampuni yoyote nje ya Dubai,Qatar au Saudi.Tusipigane vita kwenye umiliki wa Raslimali hizi.Big up Tanzania kwa kuendelea kuwa na hazina kubwa ya nishati ya gesi...kazi kwetu kuitumia kwa manufaa yetu zaidi.
TPDC ni mdau mkubwa namba moja anayewakilisha watanzania wote ktk masuala mazima ya nishati ya mafuta na gesi. Hao wengine wakomae tu watapata hivyo vitalu lakini inabidi waingie ubia tu na wazungu coz technologia na gharama za kutafuta na kuchimba mafuta au gesi si mchezo sizikieni tu kwenye vyombo vya habari. MKIAMBIWA UKWELI KWAMBA MITAJI YENU NI MIDOGO MNAKASIRIKA WAKATI NDIO UKWELI. Madini yenyewe kama dhahabu na Tanzanite ambayo utafutaji na uchimbaji wake naweza kusema gharama zake ni nafuu tunashindwa sembuse gesi na mafuta! Let's us be realistic.
 
kulikuwa na sababu gani ya kujenga bomba kutoka mtwara hadi dar kumbe nyingine iko ruvu tu hapa!

Hata Mkuranga ipo, bomba limepitiliza kwenda Mtwara!
Mambo haya siyo rahisi kama tunavyoweza kufikiri haraka haraka!
Pamoja na mambo mengine ya kitaalam, Swali la msingi la kujiuliza; nini maana ya kumiliki kitu?
 
TPDC ni mdau mkubwa namba moja anayewakilisha watanzania wote ktk masuala mazima ya nishati ya mafuta na gesi. Hao wengine wakomae tu watapata hivyo vitalu lakini inabidi waingie ubia tu na wazungu coz technologia na gharama za kutafuta na kuchimba mafuta au gesi si mchezo sizikieni tu kwenye vyombo vya habari. MKIAMBIWA UKWELI KWAMBA MITAJI YENU NI MIDOGO MNAKASIRIKA WAKATI NDIO UKWELI. Madini yenyewe kama dhahabu na Tanzanite ambayo utafutaji na uchimbaji wake naweza kusema gharama zake ni nafuu tunashindwa sembuse gesi na mafuta! Let's us be realistic.
Sijui lini tutakuwa na mawazo ya kujitegemea an kujiamini sisi wenyewe, kila siku tuwaza wazungu. Kama Julius angeyawaza haya na kutoogopa kuthubutu tungekuwa tunaendelea kulamba miguu ya mzungu.
 
Sijui lini tutakuwa na mawazo ya kujitegemea an kujiamini sisi wenyewe, kila siku tuwaza wazungu. Kama Julius angeyawaza haya na kutoogopa kuthubutu tungekuwa tunaendelea kulamba miguu ya mzungu.
Juliuze kwa nini julius hakuchimba mafuta, gesi na madini hususani dhahabu. Siyo kwamba Julius hakujua thamani na mchango wa hivyo vitu kwenye uchumi na maendeleo ya nchi ila tatizo lilikuwa ni wataalamu, technologia na mtaji wa kuchimba. Kwenye suala la utaalmu naweza kusema at least tunaweza kusema tumepiga hatua lakini kwenye technologia na mitaji tukubali tu ukweli kwamba bado. Na ndio maana hata TPDC pamoja na kuwa shirika la serilai lakini Bado halina uwezo wa kufanya hizo shughuli peke yake ndio maana lianshirikiana na wadu wengine wenye mitaji na technolojia. KUBALI UKWELI KUHUSU CHANGAMOTO ULIONAYO HALAFU UTAFUTE NAMNA YA KUITATUA KULIKO KUJIFANYA HUNA CHANGAMOTO YOYOTE HALAFU MAMBO YAKO YANAKUDODEA!
 
Bro, suala la kujitegemea halina sera mbadala, kama kuna eneo hatujiwezi ni vyema tukavuta subira, haraka ya nini mpaka tunatengeneza sera mufilisi ili tuendelee kuibiwa!
 
Hii ndo TZ utadhani chama kipya kumbe ni walewale ukiondoka utawala huu wataanza kuuponda na kusifia utawa mwingine ili mradi chama na mawazo ya walewale yaendelee kuwepo na kupumbaza watz
 
Hata ingalivumbuliwa uvunguni mwa kitanda changu ni faida gani kwangu wakati mnakula nyie tu hata harufu kuipata shida?? Tuambieni kuwa mtaitumia kwenye nini? Sisi zile by-products zake (Taka taka baki) ni zipi zitatupwa uani kwetu tuone zikitusumbua kuzitupa?? Hayo tu ili tusife kimya kimya, bali tufe tukijua, wakubwa wanashiba huko.
Mwanza wanafaidi ma pank, mbona hata kuku hawapati mifupa tena. Mtanzania uwezo wake ni kuwekeza kwenye juisi tuuuuu, Limeni maembe na mafenesi sahauni habari ya gesi.
 
TPDC ni mdau mkubwa namba moja anayewakilisha watanzania wote ktk masuala mazima ya nishati ya mafuta na gesi. Hao wengine wakomae tu watapata hivyo vitalu lakini inabidi waingie ubia tu na wazungu coz technologia na gharama za kutafuta na kuchimba mafuta au gesi si mchezo sizikieni tu kwenye vyombo vya habari. MKIAMBIWA UKWELI KWAMBA MITAJI YENU NI MIDOGO MNAKASIRIKA WAKATI NDIO UKWELI. Madini yenyewe kama dhahabu na Tanzanite ambayo utafutaji na uchimbaji wake naweza kusema gharama zake ni nafuu tunashindwa sembuse gesi na mafuta! Let's us be realistic.
Mkuu unakumbuka gesi ya visima vya songosongo kilwa
kwamba iligundulika kipindi cha mwalimu nyerere?
Lakini pia swali la kujiuliza,ni shilingi ngapi kufanya utafiti
wa uwepo wa gesi sehemu fulani? ni shilingi ngapi kuchimba kisima cha gasi?
Tusiwatishe watanzania kwa kusema lugha inayoitwa "Pesa nyingi"
na ndo wimbo unaoimbwa.Na huu wimbo una lengo la kuwanufaisha wachache
na kuwaacha wengi bila matumaini nchini mwao

Nadhani tunapotoa maoni tuepuke woga wa tusilolifahamu(the fear of the unknown).
mfano kuchimba kisima cha gesi kunaweza kuchukua dola za
kimarekani milioni mia moja.Ukizibadili kwa fedha ya
kitanzania kwa kiwango cha sh.2000.00 kwa dola utapata fedha ya kitanzania
bilioni 200,sasa jiulize je ufisadi kuanzia wa Richmond,EPA na ESCROW
ni visima vingapi vingechimbwa? au kufanya utafiti angalau wa kisima kimoja?

Binafsi naamini nchi hii haijapata wazalendo wenye
lengo la kujenga nchi na si kujenga maisha ya familia zao.
Tukuwapata wazalendo nchi hii itafika mbali.

Hivi vilio vya kusema serikali haina pesa,lakini tunasikia
fedha ya rada inaibiwa nchini inarudishwa kwa hisani
ya waingereza afu waziri bila aibu anatokwa na povu
kwa kudai kuwa uingereza isitupangie matumizi ya fedha hiyo
eti sisi ni taifa huru,wakati hiyo fedha ilipolipwa kama rushwa
hiyo nchi huru haikuwa na habari,au ilikuwa na taarifa ikaona ni sawa tu.

Kiukweli natamani kuanzia wananchi hadi viongozi tubadilike
fikira zetu tuache kuogopa jambo tusilolifahamu.
 
Mkuu unakumbuka gesi ya visima vya songosongo kilwa
kwamba iligundulika kipindi cha mwalimu nyerere?
Lakini pia swali la kujiuliza,ni shilingi ngapi kufanya utafiti
wa uwepo wa gesi sehemu fulani? ni shilingi ngapi kuchimba kisima cha gasi?
Tusiwatishe watanzania kwa kusema lugha inayoitwa "Pesa nyingi"
na ndo wimbo unaoimbwa.Na huu wimbo una lengo la kuwanufaisha wachache
na kuwaacha wengi bila matumaini nchini mwao

Nadhani tunapotoa maoni tuepuke woga wa tusilolifahamu.
mfano kuchimba kisima cha gesi kunaweza kuchukua dola za
kimarekani milioni mia moja.Ukizibadili kwa fedha ya
kitanzania kwa kiwango cha sh.2000.00 kwa dola utapata fedha ya kitanzania
bilioni 200,sasa jiulize je ufisadi kuanzia wa Richmond,EPA na ESCROW
ni visims vingapi vingechimbwa? au kufanya utafiti angalau wa kisima kimoja?

Binafsi naamini nchi hii haijapata wazalendo wenye
lengo la kujenga nchi na si kujenga maisha ya familia zao.
Tukuwapata wazalendo nchi hii itafika mbali.
Hivi vilio vya kusema serikali haina pesa,lakini tunasikia
fedha ya rada inaibiwa nchini inarudishwa kwa hisani
ya waingereza afu waziri bila aibu anatokwa na povu
kwa kudai kuwa uingereza isitupangie matumizi ya fedha hiyo
eti sisi ni taifa huru,wakati hiyo fedha ilipolipwa kama rushwa
hiyo nchi huru haikuwa na habari,au ilikuwa na taarifa ikaona ni sawa tu.

Kiukweli natamani kuanzia wananchi hadi viongozi tubadilike
fikira zetu tuachi kuogopa jambo tusilolifahamu.
Mkuu hili ndilo linalotakiwa. Kuna watu wapo kwa ajili ya kuwatisha Watanzania na kuwaona wazungu ni bora na ndio viumbe pekee vyenye akili na maarifa. Hawaoni kama ipo haja ya kuangalia dirisha lingine la fikra, wamekumbatia msemo wa Bwana Muongo kwamba sisi hatuwezi.
La hasha kwa kutumia raslimali za ndani na uzalendo tunaweza kufanya mambo ya mazuri na kuushangaza ulimwengu.
 
Hapo ndipo utakapogundua kwamba tulikurupuka na tukafanya kasi ya ajabu ya ujenzi wa Bomba la Gesi ili itakapogundulika hapo Ruvu mradi wa ujenzi utakuwa umekamilika. Ukichunguza hayo matukio yamepangwa kisanii sana.
Hapana, nadhani sasa imetusaidia sana katika kusambaza network ya miundombinu. Badala ya kujenga bomba toka Mtwara kwenda Bukoba na sehemu nyinginezo sana tutajenga kuanzia Ruvu
 
Hapana, nadhani sasa imetusaidia sana katika kusambaza network ya miundombinu. Badala ya kujenga bomba toka Mtwara kwenda Bukoba na sehemu nyinginezo sana tutajenga kuanzia Ruvu
Subiri utasikia vituko vya wenye ofisi na maamuzi ya bushara
 
Wametupa asilimia ngapi jmn ndo tunaloweza kufanya imefika 10% mana dah hali tete
 
Mkuu hili ndilo linalotakiwa. Kuna watu wapo kwa ajili ya kuwatisha Watanzania na kuwaona wazungu ni bora na ndio viumbe pekee vyenye akili na maarifa. Hawaoni kama ipo haja ya kuangalia dirisha lingine la fikra, wamekumbatia msemo wa Bwana Muongo kwamba sisi hatuwezi.
La hasha kwa kutumia raslimali za ndani na uzalendo tunaweza kufanya mambo ya mazuri na kuushangaza ulimwengu.
Ni kweli mkuu,
Sisi hatukatai kuwa wazungu wana technologia katika uchimbaji
wa gesi na uki-google utaiona hiyo technolojia kwamba ipo juu,na huu ni ukweli.

Lakini tukumbuke kwamba kama umefanikiwa kujenga,
sio kwamba umejenga wewe,bali umewatafuta watu wenye utaalam
huo ukawalipa wakakukfanyia kazi hiyo,na hata kuweka umeme hivyo
hivyo.
Sasa serikali inatakiwa kujua kuwa hata hao tunaowaita wataalam
unakuta nao wanakodi watu na makampuni yenye vifaa kutoka ulaya,marekani
na kanada au uarabuni wanachimba gesi/mafuta nasi tunawalipa gharama na faida juu.
serikali inao uwezo wa kufanya hivyo,badala ya kuwekeza kwenye miradi hewa
wafanyakazi hewa,ujenzi wa barabara hewa n.k.

TPDC ina watu waliosomeshwa kwa fedha ya walipa kodi
tuwatumie na wao waweke maslahi ya taifa mbele badala ya kutanguliza
matumbo yao kutumia utaalam wao kuleta wapiga deal.
 
Hiyo gesi ya mstaafu jamaa na familia amejineemesha sana kwenye gesi ya taifa! Hao wacimbaji na vibali amewapa yeye na familia! Nilibahatika kwenda site nikajionea exploraration ikiwa hatua za awali.....jamaa amejilimbikizia mikataba mikubwa ya gesi hata sijui kama ita mature yote! Angeirudisha tu kwa serikali! JPM nadhani ana taarifa zote anasubiri muda tu awe mwenyekiti awe na power kote kote! Asubiri miaka 5 ya mwisho afumue mikataba yote ya kipuuzi!!kina simbatrust...ya australia!!!
 
Hizi gesi zinatakiwa zitumike na kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi, kusema imegunduliwa ipo haimsaidii kitu mwananchi kama mimi, maana hata madini yaligunduliwa na yapo lakini mwananchi wa kawaida hayamsaidii kitu, kutumia dhahabu ni jambo la ajabu kwa mwananchi wa kawaida kama haipatikani nchi hii.

Ndiyo nini hicho?
 
hii gas muhongo alisema itaiingizia serikali sh.12trillions,.....kitu cha uongo kabisa muongo kadanganya taifa,.....
kwa wataalamu wa calculations zake ilibidi iingizie nchi 35trillions,.....
naona kuna upigaji deal wa muhongo.....watoe elimu ya calculations za hiyo gas ili wananchi tujue nchi itaingizaq kias gan kwa tr 12.7 of gas,......
kuna calculations zipo serikali itoe elimu kwa raia waelewe tunafaidika nayo vipi na fedha zitazopatikana ktoka hii gas zionekane zitavyotumika
kuepuka upigaji wa wahuni waliozoea kupiga...........
+MBUGA+MADINI+GAS YA MTWARA+MLIMA klm wa1 afrika+OLDUVAI GOERGE+BAHARI(BANDARI) YA DAR+BANDARI YA TANGA+BANDARI YA MTWARA+MBUGA NK,......lakini raia wanaotumia umeme nchi nzima ni 11% kati ya watu 40millions............deni la taifa trillion 48,...hii nchi ya ajabu sana,...
tunaweza kuendesha nchi tukitegemea bandari2 bila kutegemea bajeti ya mikopo toka kwa wahisani,......na tungeizidi hata afrika ya kusini kwa maendeleo
ila viongoz wetu wameweka siasa mbele kuliko nchi,.....
tubadilike
Njoo na hoja muhongo alitoa makadirio watanzania kwa kulalama amjambo
 
Hiyo gesi ya mstaafu jamaa na familia amejineemesha sana kwenye gesi ya taifa! Hao wacimbaji na vibali amewapa yeye na familia! Nilibahatika kwenda site nikajionea exploraration ikiwa hatua za awali.....jamaa amejilimbikizia mikataba mikubwa ya gesi hata sijui kama ita mature yote! Angeirudisha tu kwa serikali! JPM nadhani ana taarifa zote anasubiri muda tu awe mwenyekiti awe na power kote kote! Asubiri miaka 5 ya mwisho afumue mikataba yote ya kipuuzi!!kina simbatrust...ya australia!!!

Wacha porojo, weka ushahidi.

Punguani kama wewe uione mikataba aliyojilimbikizia ukiwa kama nani?

Hivi huu ujinga wa kuropoka ropoka hovyo mtauacha lini?

Na kuna mizumbukuku itakubali porojo zako na kukuunga mkono.
Punguani wahed.
 
Wanagundua gesi tu, gundueni na mafuta ndiyo tutajua nyie ni wajanja mbona wenzenu Kenya, Uganda na msumbiji wanagundua mafuta
Ndio ajabu yenyewe sijui tuamini Watanzania majaliwa yetu ni gesi tu au mafuta yapo ila ni Top Secret?
 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema kiwango cha gesi kilichogunduliwa katika Kitalu cha Ruvu ni cha uhakika na kuwataka wananchi wasiwe na mashaka.

TPDC imesema kampuni ya Dodsal ya Uarabuni imegundua kiwango cha futi za ujazo trilioni 2.17 katika Mambambakofi-1 kimethibitishwa na kwamba hata TPDC wenyewe wamejiridhisha.

============================

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

View attachment 331406

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kutoa maelezo kuhusu taarifa iliyotolewa na gazeti la Matanzania, Toleo namba 8129 la Jumapili tarehe 20 Machi 2016 lenye kichwa cha habari “Gesi ya Ruvu shakani”.

Taarifa hiyo ilikuwa na lengo la kupinga kile kilichoelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo kuwa ujazo wa gesi iliyogunduliwa na Kampuni ya Dodsal ya Uarabuni wenye kukadiriwa kufikia trilioni 2.17 una mashaka.

TPDC inapenda ieleweke kwamba, Kampuni ya Dodsal iligundua gesi katika kisima cha Mambambakofi-1 kwenye kitalu cha Ruvu mwezi Aprili 2015. Taarifa za ugunduzi ziliwasilishwa baada ya kufanya yafuatayo:

1. Vipimo vya kuangalia uwezekano wa gesi au mafuta kwenye mashapo ambapo kisima kilichorongwa kitaalamu iitwayo “wireline logging”. Vipimo hivyo vilionyesha uwapo wa gesi na kwa kitaalamu inaitwa “cross over”

2. Kuchukuliwa kwa vipimo vya mgandamizo kulingana na urefu wa kisima “pressure vs depth” kwenye eneo lenye mashapo lililoonyesha uwepo wa gesi

3. Aidha zilichukuliwa sampuli za gesi katika mashapo hayo ili kubaini aina ya gesi iliyopo pamoja na tafiti zingine.

Baada ya kupitia vipimo hivyo vitatu, vikaonyesha uwapo wa gesi. Kampuni ya Dodsal ikaiarifu TPDC ambayo nayo ilipitia vipimo vya logging na pressure na kujiridhisha uwepo wa gesi asilia. Sheria inaitaka TPDC kama mwenye leseni kuiarifu Serikali kuhusu kufanyika kwa ugunduzi huo. Taarifa hiyo lazima iambatane na kiasi cha awali kinachobashiri ujazo wa gesi ambao ulikuwa ni futi za ujazo bilioni 160 (0.16TCF).

Sheria hiyo pia inamruhusu mkandarasi kuendelea kufanya uchambuzi zaidi wa kina kutumia taarifa za kisima kilichochimbwa. Kwa kufanya hivyo, Dodsal wameleta taarifa ya ongezeko la ujazo wa gesi katika eneo tajwa kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.01. Hivyo basi, kwa ujumla wake Dodsal wameleta makadiria ya ujazo wa gesi wenye ukubwa wa trilioni 2.17.

Mkandarasi atahitajika kufanya Drill Stem Test wakati atakapoleta mpango kazi wa kuhakiki ujazo wa gesi na uwezo wa mashapo kuzalisha “appraisal program”.

Mnamo Machi 2016, Serikali imetimiza matakwa ya kisheria ya kitalu cha Ruvu kuwa na “Location” na Kampuni ya Dodsal inajiandaa kuleta mpango kazi kama inavyoelekeza sheria mpya Petroleum Act 2015 kifungu namba 64 na 65.

Imetolewa na;
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Benjamin W. Mkapa Pensions Towers, Tower “A”,
Azikiwe/Jamhuri Street
P.O. Box 2774,
Tel. +255 22 2200103/4
Dar Es Salaam, Tanzania
Website: www.tpdc-tz.com
Mama yangu kama kuna ndg yangu Ruvu na mtoa huko asija akapigwa na vifaru maana kwetu madini kuwa eneo lenu siyo baraka ni l.... aana
 
Back
Top Bottom