TANESCO BIG UP!

TANESCO BIG UP!

juzi Jumatatu Tanesco Mbagala umeme ulikuwa mkubwa kupindukia, uliunguza vifaa vya majumbani. Jana Jumanne kununua umeme hautumiwi token unaambiwa wanaifanyiakazi na hela hairudishwi.
Ndugu Mteja,

Pole kwa changamoto hiyo na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Tafadhali tupatie namba ya taarifa ili tuweze kukusaidia zaidi.

Kuhusu kufanya manunuzi ya umeme, tafadhali tupatie namba yako ya mita ili tuweze kukuhudumia.

Asante.^NI
 
Wakati naishi karibu na nyumbani kuna huduma fulani ya kijamii ni muhimu, walikuwa wanawahi ukiwaambia tatizo lako na walikuwa wamekariri maeneo korofi yenye matatizo ya mara kwa mara. Nikajua ni vile umuhimu wa lile eneo.

Nikaenda sehemu nyingine nikapata changamoto nayo wakatoa suruhisho mapema. Na mara nyingine tena wakafanya mapema. Nikajua hawa wapo vizuri kwenye customer service na uzuri wana wataalam local area kwenye maeneo yanayofikika.
 
Ndugu Mteja,

Pole kwa changamoto hiyo na tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Tafadhali tupatie namba ya taarifa ili tuweze kukusaidia zaidi.

Kuhusu kufanya manunuzi ya umeme, tafadhali tupatie namba yako ya mita ili tuweze kukuhudumia.

Asante.^NI
Ndugu Mteja, Taarifa Na. TEM112026TB-7378 imeshafanyiwa kazi, Tafadhali bofya kutupima tulivyokuhudumia. https://tupime.tanesco.co.tz?a=TEM112026TB-7378

Hiyo hapo.
 
Kwa kweli TANESCO wanajitahidi sana, jamaa wapo active kupita kiasi. Juzi nilipiga 180 kutoa changamoto yangu fulani, aisee haikupita nusu saa jamaa hawa hapa. Nilijikuta natoa machozi ya furaha na kujiona nimethaminiwa sana. Taasisi zote za umma zikifanya kazi kama hawa jamaa, nadhani itapunguza sana manung'uniko ya wananchi.
 
Makosa machache hufuta mazuri mengi, tanesco mnajitahidi sana ila ebu ongezeni ufanisi hasa wakati huu wa masika, muwe ikitokea changamoto mnaitatua haraka iwezekanavyo sio umeme mpaka siku mbili umekata alafu tuwapongeze,japo angalau mnastahili kupongezwa
 
Kuna mti mkubwa wa mnazi uliokauka, karibu kuangukia nguzo ya umeme, tanesco mna msaada gani? Ukikatwa kiholeka utaangukia nyaya za umeme ambazo zitavuta nguzo. Ukatwe kabla ya hizi mvua. Kerege ccm, Bagamoyo.
Habar, ndugu mteja na asante sana kwa hii taarifa. Tunaomba tuipokee na kuifanyia kazi.

Tafadhali, tunaomba ututumie mawasiliano yako kupitia inbox yetu ili, endapo wataalamu wetu watahitaji ufafanuzi au taarifa za ziada, waweze kuwasiliana nawe moja kwa moja.

Asante. ^Ni
 
Ndugu Mteja, Taarifa Na. TEM112026TB-7378 imeshafanyiwa kazi, Tafadhali bofya kutupima tulivyokuhudumia. https://tupime.tanesco.co.tz?a=TEM112026TB-7378

Hiyo hapo.
Ndugu Mteja,

Taarifa namba TEM112026TB-7378 inaonesha kuwa tayari imeshughulikiwa. Tunapenda kufahamu iwapo bado mnakabiliwa na changamoto ya kupata umeme mkubwa katika eneo hilo, ili tuweze kutoa msaada zaidi.

Asante.^NI
 
Tanesco wametuzingua sana kununua LUKU jana.
Habari, ndugu mteja.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza jana. Mfumo wa malipo ya Serikali ulikuwa na hitilafu za kiufundi, jambo lililosababisha changamoto katika kufanya miamala. Hata hivyo, huduma ya ununuzi wa umeme kupitia mawakala wetu iliendelea kupatikana.

Tunapenda kukufahamisha kuwa hitilafu hiyo imeshatatuliwa na huduma zimerejea katika hali ya kawaida. Kwa sasa, unaweza kuendelea na ununuzi wa umeme kama kawaida.

Endapo utakutana na changamoto yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa msaada zaidi.

Asante. ^NI
 
Kwakweli watu wakifanya vizuri tuwasifie. Hata mimi juzi nilikuwa na,shida ya Luku inagoma kuingia. Tena ilikuwa usiku, nilipiga Customer care walipokea fasta, na walinielekeza vizuri na nikapata ufumbuzi. Big up TANESCO customer care, angalau kwa sasa
Habari, ndugu mteja.

Tunashukuru sana kwa ujumbe wako na kutuonyesha imani. Mrejesho chanya kama huu unatupa hamasa ya kuendelea kujituma na kuboresha huduma zetu zaidi.

Asante sana. ^NI
 
Leo nimetumia fulsa hii kutoa Pongezi kwa Tanesco
1) Wana Call center,Wanasikiliza vizuri wateja na kuwapa namba za taarifa na kuzifuatilia.
2) Nililete Malalamiko ya kuwekewa nguzo,Muongozo ni siku sitini,lakini nimeletewa ndani ya mwezi mmoja
3) Issue ya kuhamisha nguzo,Wameshughulikia kwa taarifa niliyotoa.
4) Wana group za wateja wanatoa Taarifa za kukatika umeme na kupokea changamoto za wateja na kuzitatua
5) Wako very active na kitengo chao cha Mawasiliano kutoa ufafanuzi za changamoto za wateja,mpaka hapa Jf,ni member

NB Baniani Mbaya lakini Upatu wake Apewe!
Najua TANESCO wana matatizo mengi, lakini katika mashirika ambayo angalau yanajaribu kuja hapa JF kujibu na kutoa updates nafikiri wamejitahidi, ni kama shirika pekee ninaloliona hapa.

Na kuna matatizo mengine inawezekana yakawa ni ya kisera na kimfumo zaidi yamewapita kimo watendaji wanajitahidi lakini huko juu kabisa kunakofanyika maamuzi hawasikii.
 
Wamejitahidi mno.
Kila sehemu ni watsup Group.
Wanafanya vizuri mno.

Akija admini TANESCO naomba nimuachie swali.
Nyumba Ghorofa kwenye kiwanja kimoja ina Mita tatu
Flow ya chini kati na Juu.

Mita zote tatu zinakatwa Kodi ua Jengo kwa Mwezi.
Nataka ikatwe kodi ya Jengo mita Moja tu.

Naomba unipe Muongozo
Habari, ndugu mteja.

Tunashukuru sana kwa ujumbe wako wa pongezi.

Kuhusu suala la mita, tafadhali fahamu kuwa ikiwa kila floor kwenye ghorofa ina mita yenye jina tofauti tofauti, kodi ya jengo itatozwa kwa kila mita. Ni kwasababu kwa utaratibu wa nyumba za ghorofa, makato ya huduma hufanyika kwa kila floor

Hata hivyo, ikiwa mita zote zina jina moja na zinakatwa kodi ya jengo, unashauriwa kutembelea ofisi za Halmashauri husika na kujaza fomu ya maombi ili makato ya kodi ya jengo yafanyike kupitia mita moja.

Asante. ^NI
 
Leo nimetumia fulsa hii kutoa Pongezi kwa Tanesco
1) Wana Call center,Wanasikiliza vizuri wateja na kuwapa namba za taarifa na kuzifuatilia.
2) Nililete Malalamiko ya kuwekewa nguzo,Muongozo ni siku sitini,lakini nimeletewa ndani ya mwezi mmoja
3) Issue ya kuhamisha nguzo,Wameshughulikia kwa taarifa niliyotoa.
4) Wana group za wateja wanatoa Taarifa za kukatika umeme na kupokea changamoto za wateja na kuzitatua
5) Wako very active na kitengo chao cha Mawasiliano kutoa ufafanuzi za changamoto za wateja,mpaka hapa Jf,ni member

NB Baniani Mbaya lakini Upatu wake Apewe!
Umeme kila dakika unakatika yaani kwa siku moja si chini ya mara kumi.Vitu vingine sijui watu tumekosa kazi ya kufanya.
 
Juzi Jumatatu wakazi wa Mbagala Rangitatu Dar es Salaam umeme uliunguza vifaa vya majumbani, Tanesco wanapigiwa simu wakate umeme wanauchuna tu.
Habari, ndugu mteja.

Pole sana kwa changamoto uliokutana nayo. Tunaomba ufike katika ofisi yetu iliyo karibu nawe ili upate msaada zaidi. Wataalamu wetu wataweza kufanya tathmini ya changamoto yako na kukupitisha katika hatua stahiki za kuchukua.

Tunaomba radhi tena kwa usumbufu uliojitokeza. ^NI
 
Makosa machache hufuta mazuri mengi, tanesco mnajitahidi sana ila ebu ongezeni ufanisi hasa wakati huu wa masika, muwe ikitokea changamoto mnaitatua haraka iwezekanavyo sio umeme mpaka siku mbili umekata alafu tuwapongeze,japo angalau mnastahili kupongezwa
Habari, ndugu mteja.

Tunashukuru sana kwa ujumbe wako na tunathamini maoni yako. Tunatambua umuhimu wa umeme katika shughuli za kila siku za Watanzania na tunaendelea kujitahidi kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu.

Asante. ^NI
 
Back
Top Bottom