Mkuu hii movie unaielezeaje kibinafsi.
Sema huwa sipendi kuelezea movie maana najua nitakuwa na kazi ya kuandika maelezo marefu ili niweze kueleweka.
Hii ni Movie inayoelezea maisha ya Muumini wa dini ya kiislamu mwenye character mbili tofauti.
Character moja, ni mtu mwenye kuishika dini na kutimiza swala zote pamoja na kufuata sharia za dini.
Character yake ya pili ambayo ni dark side, huyu ni muuaji wa kulipwa. Huu ni upande wake wa pili ambao hata familia yake haiujui.
Huyu mtu anaitwa Latif.
Latif ana mke pamoja na watoto wawili (wakike na wakiume) lakini mke wake ni mjamzito na yupo hospitalini kujifungua mtoto.
Latif anashindwa kuhudhuria hospitalini kumpa kampani mkewe kwasababu anatekeleza mission ya mauaji.
Katika harakati za kukamilisha mauaji anapokea simu kutoka kwa binti yake ambaye alikuwa hospitalini akimsikilizia mama yake ajifungue.
Bahati mbaya ile simu inakuwa ni taarifa ya kifo cha Mkewe, ila bahati nzuri mtoto anazaliwa akiwa mzima wa afya.
Changamoto inayoibuka ni maziwa ya mtoto, mtoto hatumii maziwa ya kiwandani.
Kifupisha story.
Mwajiri wake anamtuma aende kufanya mauaji akamuue Mkorea ambaye ni kiongozi wa dini ya Kikristo anaitwa Hwang Yoo.
Sababu kuu ya huyo boss kutaka huyo Hwang Yoo auwawe ni kwasababu amekuwa ni tatizo kwa mtoto wake kuoingana na itikadi zake za kidini.
Latif anakuja kubaini kuwa mtoto wa boss wake anajihusisha na maswala ya pornografia ambapo anauza wanawake na pia ana run website za online streaming kwa ajili ya mambo ya porn.
Na mbaya ziaidi anakumbuka hata binti yake amewahi kumfuma na picha za uchi kwenye laptop yake jambo ambalo lilimuudhi na alimkemea sana.
Lakini on other hand anakuja kubaini kuwa kuna siku yule mtoto wake mchanga alikosa kabisa maziwa na hawakuwa na option ila aliyemsaidia alikuwa ni binti ambaye ni mfanyakazi wa huyo Hwang Yoo, binti huyo alijitolea kwa kumnyonyesha huyo mtoto.
Mkuu naomba niishie hapa maana hapa nitakuwa naandika script sasa.