Ondoka Dar, unapoteza muda!

Ondoka Dar, unapoteza muda!

Tupo Dom hapa
Na tunafunga zaidi ya laki,na sio Dom tu,usikariri Maisha

Nyie ndio mnaoaminisha watu upuuzi kua ukitaka kufanikiwa lazima uende dar,ndio maana mji mmejazana mpk taabu

Maisha ni popote Mungu alipokuweka,juhudi ndio mafanikio sio jina la Mkoa
Nimekuuliza kingine umeishia kubwabwaje mara dodoa mara sio Dodoma.
Nani aliekuambia kuwa uende Dar?
 
Ushauri mujarabu kabisa kwa walugaluga na waporipori
Warudi vijijini kwao watuachie Dar yetu tuanze usafi iwe kama zamani pale Kariakoo ilikuwa familia nzima mnaeenda shopping
 
ONDOKA DAR, UNAPOTEZA MUDA!

Vijana wengi tunakimbilia Dar es Salaam tukiamini kwamba ndipo maisha yanapojengwa. Tunatumia miaka mingi kutafuta riziki kwenye jiji ambalo gharama za maisha ni kubwa, huku tukisahau fursa zilizopo mikoani.

Wenzako waliobaki mikoani wanakamata heka za viwanja, wanajenga nyumba, wanawekeza kwenye mashamba na kuanzisha miradi ya muda mrefu.

Wewe umeng'ang'ana Dar, kila siku unapambana kuuza karanga, kulipa kodi, nauli na gharama nyingine za maisha. Miaka inapita, lakini huna hata kipande cha ardhi cha kuwarithisha watoto wako.

Dar es Salaam ni mji mzuri wa kutafuta biashara, kutumia vipaji na kutengeneza connection, lakini si lazima uwe sehemu bora ya kujenga utajiri wa muda mrefu kwa kila mtu.

Jiulize maswali haya:
  • Unafanya kazi kwa bidii, lakini unawekeza wapi?
  • Miaka 10 ijayo utakuwa na nini cha kuonyesha?
  • Watoto wako watarithi nini kutoka kwenye juhudi zako?
  • Kwa nini usitumie kipato unachopata mjini kuwekeza mkoani?

Ndiyo maana unaona watu wengi wakistaafu wanarudi mikoani. Wengine wakipata changamoto za kifedha wanarudi nyumbani kwa sababu huko wanaweza kuwa na ardhi, familia na gharama nafuu za maisha.

Ukweli ni kwamba, si lazima uishi mjini ili uwe tajiri. Wakati mwingine, utajiri wako unaweza kujengwa sehemu ambayo wengine wanaikimbia.

Vijana, tusikimbilie maisha ya mjini bila mpango wa maisha ya baadaye. Tafuta kipato mjini kama kuna fursa, lakini usisahau kuwekeza nyumbani.

Mimi ni kijana wa mkoani, na naamini fursa za kujenga maisha hazipo Dar es Salaam pekee.

Mkoani pia kuna maisha, ardhi na fursa kubwa za uwekezaji!

NB: MKOANI SIO KIJIJINI mkoani kuna maeneo yanayokua kwa kasi sana ambayo yapo mjini
Dar maisha aghari kakudanganya nani?
Supu ya maharagwe jero, supubya mapupu, kolomero, kichwa jerojero, maandazi mia, chapati 300, chai 300, btreakfast ya asubuhi buku jero inatosha.

Usitufatishe tunaokuka supu ya sato 10,000/= wenzio hatuna hata kibarua ni watu wa mifumo hapa mjini.

Chakula cha mchana kuanzia buku mpaka 2000 msosi wa maana kabisa, achana na sisi muda tunachoma kitimoto na bia ukijilinganisha na sisi kweli Dar pagumu.

Usisahau wakati unajitafuta kuwa na heshina kwa wakali wa donta, kuwa mwaminifu basi hata weekend kama hizi utabebwa tu maeneo ya kujidai upoteze mawazo.

Ukishindwa kuishi Dar huwezi kuishi sehemu yoyote Tanzania.
 
Mtu anaweza kufikiri mleta mada yuko sahihi ila ukweli ni kwamba, ukishindwa maisha dar hutafanikiwa popote labda kama ni mwajiriwa.

Kuna jamaa yangu alikuwa na salon huku dar kwa siku hakosi 15. Miezi 4 iliyopita akaaga eti anaondoka anaenda kagera kuanzisha maisha mapya nikamsihi sana nikamwambia huko unapotea.
Akanibishia eti huko kuna mashamba ntalima huku nanyoa. Nikamwambia sawa.

Hapa ninapoongea juzi nmemtukia nauli yuko njiani anarudi dar 😀😀😀 kapigwa na kitu kizito
maisha yameshamshinda anakwambia hata mia mbovu alikuwa anakosa.

Watu wa huko vijijini wana
 
Nimekuuliza kingine umeishia kubwabwaje mara dodoa mara sio Dodoma.
Nani aliekuambia kuwa uende Dar?
Wewe nani aliekuhakikishia ukiishi dar utakua na pesa?ungekua umefanikiwa kiuchumi ungekua hapa unabishana kuishi Dar?

Maisha popote acha ulimbukeni

Kwanza rudini kwenu?acheni ushamba
 
Ya
Ushauri mujarabu kabisa kwa walugaluga na waporipori
Warudi vijijini kwao watuachie Dar yetu tuanze usafi iwe kama zamani pale Kariakoo ilikuwa familia nzima mnaeenda shopping
Yani na wewe mkigoma unakataa kwenu?
 
Nimefatilia mwanzo mpaka mwisho. Na naomba nikwambie tu usikae ukasikiliza ushauri wa mtu yeyote ikiwezekana hata wangu puuzia.

Dar, kuna mzunguko mkubwa wa watu na watu ndio fursa, unaweza kujitafuta na ukajipata mapema.

Mkoani kuna mzunguko mdogo wa watu, na kwenye mzunguko mdogo itategemea unafahamiana na nani au wewe una nini, so kama wewe upo kwenye 0 kabisa na bado unategemewa sehemu/ulikotoka, mkoani itabidi uangalie mkoa wenye pesa za papo kwa papo (Mikoa yenye madini/dhahabu, ndio inaongoza kwa pesa za papo kwa papo).

Kwa ushauri wangu, nashauri Kijana anaeanza kujitafuta aanzie Dar. Faida zake ni kwamba ataijua pesa kwa haraka, na akiwa na juhudi anaweza kupata ahueni mapema, lakini haitakiwi kuishia hapo na kulowea starehe au maisha ya mjini. Ukijipata tu Dsm, haraka anza uwekezaji mikoani, Dsm itakupa pesa ya kila siku ila mikoani patakupatia pesa za kukutajirisha na kukufutia umaskini kabisa, usiangalie na shauri za humu uhangaike uende huku ama kule.

Jiangalie wewe unaweza nini, una watu? una elimu? una mtaji wa pesa? upo tayari kujishusha kwa kiasi gani? baada ya kujitathmini yote hayo tafuta unapopaweza na sio penye pesa au fursa, kwasababu tuna watu wa aina 2, wanaoanzisha fursa na wanaofata fursa, pengine wewe ndio mwanzilishi, hivyo tafuta unapoweza na watu wako watakufata, iwe Dar iwe mkoani.

Hata ukijipata mkoani, hakikisha unaenda kutoa wenge Dar, sababu Dar itabaki kua Dar tu, itabaki kua changanyikeni na itabaki kua sehemu ambayo mtu anaweza kuishi bila kunyenyekea mtu, kwa mikoani kuna namna inabidi uwe humble, na baadhi ya mikoa ukipiga hatua ndefu ndefu za maendeleo kwa haraka kuliko wazawa wanapita na wewe wima wima.

Halafu Dar inaweza ikawa inaonekana ni mkoa mmoja, ila amini nakwambia ndani ya Dsm kuna Dsm nyingi sana, kuna dar za kiwaki, na kuna dar ya dili pesa za chap, kuna dar ya mafanikio, kuna dar ya kulala njaa na nyumba zilizo dampo. Ukikuta mtu anazungumzia Dar muulize Dar ipi ya maisha anayoishi kabla hajakuvuta kwenye maisha yake ya njaa, humu unasoma ID tu, mmoja ana tweet kutokea Ghorofani pale Goba, na comment inayofata yupo kwa shangazi yake Buza kwa mama kibonge analala sebleni. wote watakuambia kuhusu Dar na kila mtu picha anayoichora ni tofauti kabisa.

Mwisho kwa kijana mpambanaji kokote unakoenda hakikisha unaepuka Pombe na Uzinzi, ukiviepuka hivi nakuhakikishia popote unafanikiwa hata kwa kuchelewa.
 
Back
Top Bottom