Ondoka Dar, unapoteza muda!

Ondoka Dar, unapoteza muda!

Tafuta mtaji uoneshwe mashamba yasiyotegemea mvua 100% kama kweli una Nia.
Sio ukweeli km unavyosimuliwa mkuu hizo zipo kwenye PDF kwenye ground ni tofauti kabisa, nishawahi enda huko bush yes nikakuta wanakodi mashamba makubwa kwa bei ndogo sana ila kilimo ni cha kubet yaan ukiotea umeula ukikosea umeliwa, nilishauriwa hilo pia kabla sijaingiza miguu yangu na kweli kipindi nilichoenda kilikua cha ukame hakuna alielima mpunga na mashamba yalikua wazi nikaambiwa humu unamomuona mvua ikinyesha maji yanajaa sana na mpunga unastawi mno ila kipindi kile kulikua kukame kumekauka na hakuna anaelima sasa usishangae unapowaona wapo Dar huko shamba ni kukame unataka wakalime nini mawe?
 
Inategemea umewekeza nini hapo ulipo mtu mwenye ekari 500 za maparachichi ( kilimo Cha kisasa) yupo zake mkoani anapiga hela umwambie Dar Kuna fursa atakuelewa???
Hawezi kukuelewa, kama ambayo mtu yupo Kkoo ana mzunguko wake wa biashara hatakuelewa.

All in all Dar kuna diversification ya fursa nyingi kuliko Mikoani ndio maana watu wamejaza.

Mwisho kutoboa ni juhudi,Bahati ya mtu binafsi
 
Inategemea umewekeza nini hapo ulipo mtu mwenye ekari 500 za maparachichi ( kilimo Cha kisasa) yupo zake mkoani anapiga hela umwambie Dar Kuna fursa atakuelewa???
Wala sio nyingi kiasi hicho ,Kuna watu wana ekari tano TU za kilimo huku mikoani na wanapiga pesa mbaya, watoto shule ,nyumba zaidi ya moja magari nk.
 
Kama wapi?
Yapo mengi mkuu, Kaskazini Mashariki kuna Kikatiti, Meserani, Kisongo, kuna Lokii mbele ya maweni karibu na mererani, Manyara kuna Endagikot, Kuna centre karibu na Endasaki, Endagau, Idom, Dodoma kuna Bahi kama sikosei, Singida ipo Sepuka. Kanda ya ziwa kuna katoro, buzilayombo, Mwaloni, nyegezi N.k n.k n.k.........
Yapo mengi sana mengine nimefika mengine nayasikia tu.
 
Hivi watu huwa mnaandika vitu mnavovijua lakini?
Samahani mkuu Dodoma unaijua vizuri?
Umeshawahi kuishi Dodoma?
Ni biashara gani dodoma yakufanya ikakuletea faida ya laki kwa siku?
Tupo Dom hapa
Na tunafunga zaidi ya laki,na sio Dom tu,usikariri Maisha

Nyie ndio mnaoaminisha watu upuuzi kua ukitaka kufanikiwa lazima uende dar,ndio maana mji mmejazana mpk taabu

Maisha ni popote Mungu alipokuweka,juhudi ndio mafanikio sio jina la Mkoa
 
ONDOKA DAR, UNAPOTEZA MUDA!

Vijana wengi tunakimbilia Dar es Salaam tukiamini kwamba ndipo maisha yanapojengwa. Tunatumia miaka mingi kutafuta riziki kwenye jiji ambalo gharama za maisha ni kubwa, huku tukisahau fursa zilizopo mikoani.

Wenzako waliobaki mikoani wanakamata heka za viwanja, wanajenga nyumba, wanawekeza kwenye mashamba na kuanzisha miradi ya muda mrefu.

Wewe umeng'ang'ana Dar, kila siku unapambana kuuza karanga, kulipa kodi, nauli na gharama nyingine za maisha. Miaka inapita, lakini huna hata kipande cha ardhi cha kuwarithisha watoto wako.

Dar es Salaam ni mji mzuri wa kutafuta biashara, kutumia vipaji na kutengeneza connection, lakini si lazima uwe sehemu bora ya kujenga utajiri wa muda mrefu kwa kila mtu.

Jiulize maswali haya:
  • Unafanya kazi kwa bidii, lakini unawekeza wapi?
  • Miaka 10 ijayo utakuwa na nini cha kuonyesha?
  • Watoto wako watarithi nini kutoka kwenye juhudi zako?
  • Kwa nini usitumie kipato unachopata mjini kuwekeza mkoani?

Ndiyo maana unaona watu wengi wakistaafu wanarudi mikoani. Wengine wakipata changamoto za kifedha wanarudi nyumbani kwa sababu huko wanaweza kuwa na ardhi, familia na gharama nafuu za maisha.

Ukweli ni kwamba, si lazima uishi mjini ili uwe tajiri. Wakati mwingine, utajiri wako unaweza kujengwa sehemu ambayo wengine wanaikimbia.

Vijana, tusikimbilie maisha ya mjini bila mpango wa maisha ya baadaye. Tafuta kipato mjini kama kuna fursa, lakini usisahau kuwekeza nyumbani.

Mimi ni kijana wa mkoani, na naamini fursa za kujenga maisha hazipo Dar es Salaam pekee.

Mkoani pia kuna maisha, ardhi na fursa kubwa za uwekezaji!

NB: MKOANI SIO KIJIJINI mkoani kuna maeneo yanayokua kwa kasi sana ambayo yapo mjini
well done gentleman,
umepiga kwenye mshono kabisa aise 💪
 
Hawezi kukuelewa, kama ambayo mtu yupo Kkoo ana mzunguko wake wa biashara hatakuelewa.

All in all Dar kuna diversification ya fursa nyingi kuliko Mikoani ndio maana watu wamejaza.

Mwisho kutoboa ni juhudi,Bahati ya mtu binafsi

Wala sio nyingi kiasi hicho ,Kuna watu wana ekari tano TU za kilimo huku mikoani na wanapiga pesa mbaya, watoto shule ,nyumba zaidi ya moja magari nk.
Upo sahihi sana, alafu Sasa Hivi kila sehemu kumechangamka hata huko Kijijini kunakosemwa sijui ni wapi🤔 wiki iliyopita nilikuwa Mbeya nimeshangaa sana kulivyobadilika tofauti na zamani mwenye Uzi ana hoja ukiona sehemu haieleweki ondoka wewe sio mti.
 
Back
Top Bottom