GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,763
- 128,261
Natanguliza salamu zangu kwenu za dhati nikitumai kuwa wote ni wazima kuanzia kwa wamiliki au waanzilishi wa JamiiForums, Moderators na Members wenzangu. Kuna kitu nataka niwashirikisheni na nitawashukuruni kama mtanipatia ufafanuzi wa kina na wa kutosha.
Ni kwamba mwaka juzi 2013 mwezi November nilipeleka maombi yangu ya kazi katika chuo fulani kikubwa tu hapa jijini na Tanzania, na ndani ya wiki moja niliitwa kufanya interview ambayo hata hivyo sikuielewa kwani nilifanyishwa interview na mtendaji mkuu pamoja na mmoja na mhadhiri mmoja, na baada ya hapo tena nikaambiwa kuwa kesho yake niende kufanya interview nyingine ya darasani (ya kufundisha) ambapo nilipewa nifundishe somo ambalo sikuwa competent nalo, hivyo nilijitahidi tu kutiririka nalo japo kiubishi na kumaliza.
Nikaambiwa kuwa nisubiri majibu na hayo majibu niliyasubiri bila mafanikio nikajua tu kuwa nimeshachinjiwa baharini.
Sikuishia hapo au kukata tamaa, na mwaka jana 2014 mwezi October nilijisikia tu kutuma tena kwa mara ya pili maombi yangu na nikawaachia na CV yangu kuwa nilipenda kufanya nao kazi kwani kwa ubora wa hicho chuo nina uhakika nikiwa hapo hata cv yangu na ufanisi wangu utaongezeka maradufu, na isitoshe napenda pia mazingira yake na kubwa zaidi ni umakini wa kuanzia administration yao, walimu (wahadhiri) wake na other supporting staff.
Mwenyezi Mungu amenikumbuka, leo Gentamycine na hawa jamaa wamenipigia simu kuwa kesho Ijumaa natakiwa kwenda kufanya interview nao kwa nafasi ile ya uhadhiri niliyoiomba huko nyuma na binafsi nimefarijika tu kwa kukumbukwa huku ila nina maswali yangu haya kwenu ambayo nitashukuru mkinijibu;
1. Je wamegundua nini tena kwangu hadi wameniita tena kufanya interview nao kesho?
2. Je wameniita kunisanifu tu kisha kama kawaida yao wanichinjie baharini au kweli wananihitaji?
3. Je kwanini wameniweka mimi kuwa wa kwanza katika kufanyiwa interview hiyo kesho?
4. Je ni mambo gani yakuzingatia na kuchukua tahadhari ili kesho nami niibuke mshindi na nile shavu?
5. Je kwenu nyie mnaona hii ni dalili ya kufanikiwa sasa au nisiende tu kwani labda sitofanikiwa tena?
Nawasilisha hili jambo kwenu na michango yenu nitaiheshimu sana na mno............MBARIKIWE Nyote, Akhsanteni.