Mwanamke wewe; naongea na wewe hapo

Mwanamke wewe; naongea na wewe hapo

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,486
Reaction score
1,451
Wanaume wanaojitambua ni wachache sana siku hizi. Sio rahisi hata kidogo kumpata mwanaume anayejitambua siku hizi. Kumpata mwanaume anayejitambua kunakuja na gharama yake, lazima ukubali kulipa gharama ili kumpata na lazima ukubali kulipa gharama ili kudumu naye.
Unapomuona mwanaume anafanya kila awezalo na kila juhudi ili kuboresha na kuimarisha uhusiano au ndoa yenu usidhani kuwa yuko desperate, usidhani kuwa hawezi kuishi bila wewe.
Ni kwa sababu tu anataka kuwa mwanaume bora kwako na sio bora mwanaume.
Mwanaume huwa hapigi kelele anapoamua kuondoka na kukuacha. Alishapiga sana kelele ili mudumu pamoja lakini hukusikiliza, ulimpuuza.
Wapendwa wanawake, mwanaume anapoacha kuonesha dalili ya wivu kwako, ujue roho yake imeshaondoka kwako.
Usimchukulie poa mwanaume anayejitambua aliyeamua kukupenda kwa dhati.
Usidhani kuwa yeye kukupenda sana ndio udhaifu wake
Wanaume wema wanaojitambua sio rahisi kuwapata zama hizi, wako wachache sana na ili umpate na kudumu naye lazima ukubali kulipa gharama.
Na gharama yenyewe ni KUMHESHIMU, KUMTII, KUMTHAMINI na KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWAKO.
Mthamini mwanaume wako!
 
Back
Top Bottom