VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,489
- 1,465
Bwana huyu pichani, kakumbana na vibaka waliomjeruhi na mpaka sasa yupo mahututi hospitalini.
Miji mingi nchini Rwanda, imekuwa ikikumbwa na wingi wa vijana wasio na kazi, na hutegemea maisha yao kwa kuibia watu, kuwapora walivyoo navyo(mara nyingi simu na pesa). Watu hao hujeruhiwa kwa viwembe na mapanga.
Polisi inajitahidi kukabiliana nao, lakini huongezeka kila kukicha, na matukio yanazidi kushamili, ambapo raia huliona kama jambo lisilo na madhara mbele ya vyombo vya usalama. Matukio haya, huambatana na wizi wa majumbani, ambapo vitu vya kielektroniki ndo hupendelewa zaidi.