Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,756
- 31,233
David Kafulila bado ni kijana mdogo, anaweza kuwa na nia njema kabisa lakini hana uzoefu namna serikali inavyoenda na inavyoendeshwa.
Ndoto zake za PPP ni nzuri kwenye makaratasi, lakini utekelezaji wake ni wa kufikirika.
PPP ni Public Private Partnership, yaani serikali na wawekezaji kukaa pamoja kwenye miradi mikubwa(hata midogo) kwa manufaa ya huduma za jamii.
Binafsi naona ndoto za Kafulila ni za Alinacha, kujenga hekalu hewani, bila msingi wowote.
Au kwa lugha za wasela , kumpigia mbuzi gitaa.
Siyo kwamba napinga kuwa PPP haiwezekani, lakini katika serikali SIWAONI watu wa kukubaliana na PPP.
Na sababu zipo wazi
1. Mifumo ya kodi bado haieleweki kuhimiza uwekezaji katika miradi mikubwa kwa ubia. Hata kwa miradi iliyosamehewa kodi, kodi inakokotolewa hadi wawekezaji wanakimbia nchi. Mfano mzuri miradi ya JICA-kampuni zote zimekimbia nchi.
Na hakuna mtu serikali inalisemea hili au kulitatua, maana hawafaidiki binafsi.
2. Viongozi wengi ni walafi, na wangependa miradi hiyo waingie wao binafsi na kampuni zao na watoto wao. Mifano ipo mingi, hasa kwenye uuzaji wa mashirika ya umma.
3. Urasimu wa kutisha uliopo, hata kama unawekeza kwa mtaji wako, upande wa pili kimsingi watu wanataka kunufaika kibinafsi.
Kwa hiyo Kafulila aelewe kuwa , sisi ni watanzania , siyo watu wenye uchungu mkubwa sana wa maendeleo kwa kujitoa kama wachina au South East Asians, au Tigers kama walivyokuwa wanajulikana.
Hivyo David Kafulila atabaki kuwa kama Yohana Mbatizaji anayetengeneza mapito ya Messiah.