JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

BNBM BUILDING MATERIALS INDUSTRY (T) LTD

TUNAAJIRI!

NAFASI: STORE KEEPER

Mahali: MLANDIZI KIBAHA

Sekta: Uzalishaji wa Gypsum

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe na Diploma ya Procurement, Stores Management au fani inayohusiana.
  • Awe na uzoefu wa kazi wa angalau mwaka mmoja (1).
  • Awe na ujuzi wa Microsoft Excel na computer.
  • Awe na uwezo wa kusimamia stock na kutunza kumbukumbu.
  • Awe mwaminifu, mchapakazi na mwenye nidhamu.
  • Wanawake pekee ndio wanaruhusiwa kuomba.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Tuma CV kupitia WhatsApp:

0713677831

Mwisho wa maombi: 16 Novemba 2026.
 
-Moja ya jambo ambalo linaweza kukuchelewesha sana kutimiza malengo yako, ni kuwa na tabia ya kutaka kuonewa huruma kila wakati unapopata changamoto fulani kwenye maisha yako.

-Kuna watu wakipata shida wanataka kila mtu aache anachokifanya aanze kuwazingatia wao tu, wanasahau kuwa kila mtu ana changamoto zake ambazo anapambana nazo kimya kimya.

-Huruma yako au kukaa chini na kulia hakutasaidia chochote bila kuchukua hatua, acha kupost status za kutia huruma na kuiambia dunia hali unayopitia kwasababu hakuna mtu atakayekuja kukuokoa.
(No one will come to save you)

-Utafiti kutoka chuo kikuu cha Harvard unaonyesha kuwa unapowaeleza watu ovyo matatizo yako, asilimia 80% ya watu huwa hawajali kabisa na asilimia 20% huwa wanafurahia.😥

-Ni kweli kwamba maisha yetu yanahitaji watu ili kutuvusha kwenye baadhi ya hatua za maisha yetu,lakini tunahitaji kuwajibika wenyewe kwa sehemu kubwa sana ili kufanikisha malengo yetu🏅

-Usipowajibika kwenye kutengeneza aina ya maisha unayoyataka hakuna muujiza wowote utakaotokea kuja kukutoa hapo ulipo.

-Kama unataka kujikomboa kiuchumi 💸 hakuna mtu atakayekuja kukuwekea akiba ni wajibu wako,jambo lolote ambalo unataka kufanya lazima ujue kuwa hakuna mtu atakayekuja kuwajibika kwaajili yako ni wajibu wako🫰

-Acha kuendelea kuishi maisha ya kutaka kuonewa huruma na kujiona huwezi kutoka hapo ulipo amini unaweza na unao uwezo wa kuchukua hatua ya a kutoka hapo ulipo,Ndio inawezekana!!...🤷

-Bila kujali kuwa unapitia katika hali ngumu kiasi gani, leo amua na amini kuwa wewe ndio mtu wa kwanza kuwajibika kwa maisha yako ili uishi maisha unayoyataka.
Chukua hatua leo usichelewe!!..

-Kama umeipenda makala hii weka reaction kisha mtumie kijana mmoja mpambanaji ili kumuongezea hamasa ya kupambania ndoto zake- 🏆
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
-Frank Snatra,mwimbaji na mwigizaji nguli kutoka nchini Marekani 🇺🇸 aliwahi kusema kuwa.

"The best revenge is massive success" akimaanisha kuwa "kisasi bora zaidi sio kugombana, bali ni kufanikiwa kwa kiwango cha juu zaidi kiasi kwamba hata waliokudharau wabaki wakishangaa."🤔

-Wakati mwingine katika maisha utakutana na watu wanaokudharau au kukuona hauwezi watakucheka, watakusema vibaya na watatamani uanguke.

Jambo la msingi ni kwamba...
-Badala ya kupoteza nguvu zako kuwajibu tumia nguvu hiyo kujijenga,Jifunze zaidi fanya kazi kwa bidii sana, songa mbele kimya kimya "mafanikio yako" ndiyo jibu kubwa kuliko kupoteza muda kubishana nao.

-Bila kujali ni watu wangapi wanakukatisha tamaa au wanakuombea mabaya,leo amua kuwa mafanikio yako ndiyo yatakayokuwa kisasi chako kwao🏆
-The Power Is Within You-
💯🫵✨

(Yona Morice Yona)
 
Kwa mujibu wa utafiti wa kisaikolojia mtoto mdogo anapozaliwa hadi kufikia umri wa miaka mitano 5 anakuwa ameambiwa maneno HASI kama "Hapana,Hujui,Acha" takribani mara elfu 40.

Lakini anakuwa ameambiwa maneno CHANYA kama "Ndiyo, Unajua au Unaweza" takribani mara elfu 5 tu🤷

Hii maana yake ni kuwa...
Katika maisha utakutana na watu wengi sana wanaokatisha tamaa na kukuvunja moyo kuliko wanaokutia moyo,Jambo muhimu la kukumbuka kila wakati ni kuwa.

Sio lazima ushinde kila vita ya watu wanaokucheka au kukudharau wakati mwingine waachie ushindi ili wewe ubaki na AMANI❣️

Hatakama watu wasiokupenda wapo 78,721,054,206,41 achana nao wapuuzie kabisa kama ulivyopotezea kusoma hizo namba (Ndio mimi najua umeziruka tu😁)

-Hii itakupa utulivu mkubwa sana wa akili na kukufanya ubaki na nguvu za kuendelea kujijenga zaidi na kuongeza kasi ya kutimiza malengo yako🥇
-The Power Is Within You-
✨ 🫵

(Yona Morice Yona)
 
-Wanaume wengi huamka wakiwa wamechoka sana,usoni huonekana wako sawa ila ndani wamebeba hofu na mawazo mengi.

-Sio kwasababu wanapenda kuwa hivyo bali ni kwasababu hawataki watu wanaowategemea waone maumivu wanayoyabeba.

-Kuna wakati mwanaume anakata tamaa,anaugulia maumivu makali sana mithili ya simba aliyejeruhiwa lakini kila akikumbuka kuna watu nyuma yake wanamtegemea, anapata nguvu na ujasiri wa kuendelea kusonga mbele akiwa katikati ya maumivu😢

Mbaya zaidi ni kwamba...
-Jamii imemsahau mwanaume inaamini yeye ni JASIRI siku zote na hapitii magumu, kumbe kuna wakati analia kimya kimya moyoni mwake tu, Hata ukimuuliza "unaendeleaje" atasema "niko sawa" ili asiwavunje moyo wanaomtegemea💔

-Viktor Frankl, Mwandishi na mtaalamu wa saikolojia katika kitabu chake cha Man's Search for Meaning, anasema "When we are no longer able to change a situation, we are challenged to change ourselves"

Akimaanisha kuwa: "Tunaposhindwa kubadilisha hali inayotukabili,tunalazimika kujibadilisha sisi wenyewe ili tuweze kuimudu."

-Na hii ndio njia ambayo mara nyingi wanaume wengi hutumia anapoona hawezi kubadilisha hali fulani au changamoto inayomkabili basi yeye huamua kujibadilisha kuonekana yuko sawa ili asiwavunje moyo 💕 wale wanaomtegemea.

-Leo tafuta mtu mmoja unayemwamini ongea naye mweleze angalau kwa uchache hali unayopitia,Sio kwasababu ya kuzikimbia changamoto bali kwasababu akili yako inahitaji utulivu na uhuru ili uweze kufanya kazi zako kwa ufanisi mkubwa kutimiza malengo yako.

-Kama unamjua mwanaume mmoja ambaye ni mpambanaji weka reaction kisha mtumie makala hii ili kumponya maumivu anayopitia leo.
-The Power Is Within You-
✨🫵

(Yona Morice Yona)
 
☀️ UJUMBE WA MCHANA: USIKATE TAMAA, ENDELEA KUSONGA MBELE.

Kumbuka, maisha hayahitaji uwe na majibu yote leo, yanahitaji uwe na ujasiri wa kuendelea hata pale ambapo mambo hayaendi kama ulivyopanga.

Usiruhusu changamoto za jana zikunyime nguvu ya kupambana leo. Usijilinganishe na wengine, kwa sababu kila mtu ana safari yake, muda wake na mapambano yake yasiyoonekana kwa macho ya watu.

Kama umechoka, pumzika, lakini usikate tamaa. Kama umeanguka, inuka tena. Kama umechelewa kufika unakotaka, usijione umeshindwa. Bado una nafasi ya kubadilisha historia yako.

Jiamini, kuwa mvumilivu na endelea kufanya kile kilicho ndani ya uwezo wako.

Kumbuka: Mafanikio si matokeo ya kutokutana na vikwazo, bali ni uwezo wa kuendelea mbele licha ya vikwazo hivyo.

Nakutakia mchana mwema wenye nguvu mpya, matumaini mapya na sababu nyingi za kutabasamu. 🌿

USIKATE TAMAA, BADO SAFARI INAENDELEA! 💪
 
Asababisha mwanamke mwenzake ajinyonge

Yeees! Ni kitambo kidogo hatujapitia haya mastory yetu ya mtaani,kwani kitaa ndio maisha halisi hupatikana huko

Home boy ndio kwanza kamaliza chuo huku bado maisha yakiendelea kupiga mtaani,anakutana na mwanamke wa maisha yake

Akiwa bado ana haso mtaani alijitahidi sana baby girl apate mahitaji muhimu, mwamba anakwambia ikafika wakati baby girl wake akataka home boy atimbe home akatambulishwe

Siku ikawadia home boy huyu hapa kwa wakwe zake, basi akiwa pale akaona baby girl akiitwa chobingo na mama yake

Bahati mbaya au nzuri home boy akasikia mazungumzo kati ya mama na binti yake,unaambiwa bimkubwa akamwambia mwanae "yaani katika wanaume wote hapa dunia hukuona mwanaume wa maana mpaka umemleta hiyu aliyepauka na mwenye chunusi?"

Unaambiwa home boy anasema nilisikia mazungumzo yote huku roho inauma lakini nikakaza tu,mwisho wa siku mapenzi yao yaliendelea kama kawa

Home boy anasema hakutaka kuona baby girl akiwa mnyonge hivyo akaanza kumpambania ili apate kazi,na kweli Mungu sio bey,akafanikiwa kupata nafasi ya kazi kutoka kwa rafiki yake James,tena unaambiwa mwamba alikuwa mgumu kutoa ushirikiano,lakini home boy anakwambia alipiga hadi magoti ili tu James ampatie nafasi ya kazi baby girl wake

Kumbe home boy hakujua hilo ni kosa la kiufundi ambalo lau angejua mapema wala asifanya hayo aliyoyafanya

Mwisho wa siku baada ya baby girl kuanza kazi in the name ya kupambana na maisha,baadae mambo yakaanza kubadilika, sababu nyingi za baby girl za kutokuwepo nyumbani,mara kuna shughuli tunaenda kufanya,mara sijui kazini kuna ishu gani itabidi niende ilimradi baby girl hakupatikana home kwa muda mrefu

Wapenzi wasomaji, huenda mmepata kitu hapa,jifunze kujua au kugundua changes ambazo mwenza wako ananza kuzionyesha hapa, ambazo zinatia mashaka, mfano mdogo tu,kama baby girl wako hapo awali alikuwa hajali sana kuhusu muonekano wake na sasa anaanza kujikwatua na kujali sana kuhusu urembo wake basi chukua kutoka kwa malegend, hapo kuna penzi jipya linachipua au anataka kumuimpress mtu fulani,got it right?

Kumbe bwana James alikuwa anamchukua baby girl na kwenda kusmashi nae home kwake,hapa napo James alifanya kosa kubwa la kiufundi,sijui kama hakujua kama home kuna cctv kamera au labda aliizoea mpaka akasahau kama kuna kitu kama hicho

Mke wa James akawa anajionea porn za bure kati ya mumewe na baby girl,ndio ikafika kipindi akamtext baby girl kumwambia kama haitoshi umeamua kuja nyumbani kwangu na kulala na mume wangu "nina video zenu za kutosha tu"

Hapo baby girl akaomba msamaha,lakini mke wa James akamwambia "utakuja kujua kwanini nina hispi na ambazo sizipendi"

Baadae ikaja kuonekana kwamba yule mke wa James alikuja kujiua,lakini haikujulikana kama ni stress za mapenzi au ndio baby girl na mume wa James walipanga ule mchongo ili wabaki wenyewe wale mema ya dunia


View: https://youtu.be/f7UNv9uVbGI?si=2LUXtUpXL-RWBHoU

Hapo ndio home boy akamwambia baby girl, "kama umeamua kumuua mwanamke mwenzako inamaana next ni mimi"

Nomaaaa!

Adios!
 
Screenshot_20261115-152446_Google.jpg


### Busara za Michelle Obama

Michelle Obama

Michelle Obama ni mwanamke anayejulikana kwa hekima, ujasiri, kujithamini, elimu na msimamo wa maisha. Maneno yake mengi yanahamasisha watu kujiamini na kutokuruhusu mazingira yaamue thamani yao.

Hizi ni baadhi ya busara na mafundisho yanayohusishwa na falsafa yake ya maisha, zikiwa zimefasiriwa kwa Kiswahili.

### Busara 10 za Michelle Obama

1\. Usishuke kiwango chako kwa sababu wengine wameamua kuwa watu wasio na heshima. Tabia yako inapaswa kuongozwa na misingi yako, si tabia za watu wengine.

2\. Usiruhusu maneno ya watu yakukengeushe kwenye malengo yako. Jifahamu, jiamini na endelea na safari yako.

3\. Elimu ni silaha muhimu ya kujenga maisha bora. Usiache kujifunza kwa sababu umemaliza shule.

4\. Ujasiri hauji kwa siku moja. Unajengwa kwa kuendelea kukabiliana na mambo yanayokutisha.

5\. Usiogope kuwa wewe mwenyewe. Huhitaji kujibadilisha ili kukubalika na kila mtu.

6\. Hadithi yako ina thamani. Usione aibu kuhusu ulipotoka, kwa sababu historia yako ni sehemu ya utambulisho wako.

7\. Matumaini ni muhimu katika nyakati ngumu. Usikubali changamoto za sasa zikufanye upoteze imani na kesho.

8\. Mafanikio yako hayapaswi kuwa sababu ya kuwadharau wengine. Unapopanda, saidia wengine nao wapande.

9\. Kuwa na nidhamu hata pale ambapo hakuna anayekuangalia. Tabia zako za faragha zina mchango mkubwa katika maisha yako.

10\. Usipime thamani yako kwa maoni ya watu wengine. Thamani yako haitegemei kila mtu kukuelewa au kukukubali.

### Nukuu maarufu ya Michelle Obama

### “When they go low, we go high.”

"Wanaposhuka chini kwa tabia zao, sisi tunapaswa kupanda juu kwa tabia zetu."

Michelle Obama, hotuba ya Democratic National Convention, 2016. 2016 DNC Address.doc +1

Funzo kubwa: Usiruhusu hasira, chuki, kejeli au tabia mbaya za watu wengine zikubadilishe na kuwa mtu ambaye hukupanga kuwa.

Kuwa na msimamo, heshima na utu. Si kila vita unapaswa kupigana, na si kila jambo linahitaji majibu.

Wakati mwingine ushindi mkubwa ni kubaki mwaminifu kwa misingi yako hata pale dunia inapokupa sababu za kuiacha.

Unaweza kusoma zaidi katika kitabu chake The Light We Carry na Becoming.
 
Back
Top Bottom