Historia ya TANU Ilifichwa?

Historia ya TANU Ilifichwa?

Asante mzee Mohamed kwa maelezo yako. Nakuomba uziulize familia za wazee wa TANU na waasisi wa TANU kuhusu hilo , halafu utupe majibu, ikilazimika tutangalia ushahidi uliohifadhiwa kwani upo.
 
Misha,
Nimetafiti na kuandika kitabu: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," London 1998.

Kila kitu changu kuhusu historia ya TANU kimo kitabuni.
 
Mzee Mohamed Said, wanahistoria mna msemo unaosema " a text without context is pretext" na vilevile elimu haina mwisho. Umekiri kuwa huifahamu dhana ya Mwl. Nyerere kuwa alitabiriwa kuleta uhuru, na umeombwa uliulizie hilo kwa familia za wazee wa Kariakoo, Bagamoyo walioko kwenye maandiko yako je, hilo ni gumu? Kujua kitu gani kilifanyika ni vizuri, kujua kwanini kitu fulani kilitendeka ni muhimu zaidi, na ndiyo msingi wa historia, sasa tutajuaje kwa uhakika kwanini wazee wa Kariakoo na Bagamoyo n,k, walitenda walichokitenda bila ya kujua kwa undani kuhusu mtazamo na matarajio yao?
 
Shehe Ramia wa Bagamoyo alitabiri ujio wa uhuru na mtoto wake Shehe Mohamed Ramia alibaini kuwa ni Kambarage. Wangoni wa Kariakoo walikuwa na utabiri ulioelezea hata muda Kambarage atafika Dar kuleta uhuru. Wadau hawa walikuwa wanafanya mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si vinginevyo. Maneno ya kuwa dini fulani ilifanya makubwa zaidi na kuvuna kidogo yanatugawa bure! Mitihani ipo lakini Mwenyezi Mungu ananjia zake, tujitahidi kuwa wachamungu kama walivyofanya wakurugenzi wetu. Mimi nilikuwa napita, kila la heri.
 
Hapakuwa na wazee kutoka Bagamoyo wala kokote katika kuunda TANU 1954.

Hao wazee mimi nawasikia kutoka kwa Mwalimu Nyerere na wala hajapata kutaja majina yao wala hajawaadhimisha kwa kuwapa medali.
 
Shehe Ramia wa Bagamoyo alitabiri ujio wa uhuru na mtoto wake Shehe Mohamed Ramia alibaini kuwa ni Kambarage. Wangoni wa Kariakoo walikuwa na utabiri ulioelezea hata muda Kambarage atafika Dar kuleta uhuru. Wadau hawa walikuwa wanafanya mapenzi ya Mwenyezi Mungu na si vinginevyo. Maneno ya kuwa dini fulani ilifanya makubwa zaidi na kuvuna kidogo yanatugawa bure! Mitihani ipo lakini Mwenyezi Mungu ananjia zake, tujitahidi kuwa wachamungu kama walivyofanya wakurugenzi wetu. Mimi nilikuwa napita, kila la heri.
Misha,
Kuwa Sheikh Ramia alikuwa mtabiri hiyo ni kufru.

Hakuna mwenye elimu ya ghaibu ila Allah.

Hakuna binadamu ajuaye yatakayotokea kesho.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislamu.

Sheikh Ramiyya hakumjua Nyerere hadi alipopelekwa kwake na binamu zake wawili Iddi Faiz Mafungo (kadi ya TANU No. 24)na Iddi Tosiri (kadi ya TANU No. 25).
 
Mzee Mohamed Saidi, sijasema Shehe Ramia alikuwa mtabiri, kwenye you tube kuna video ambayo hata wewe umo inaitwa "karama na maajabu ya Shehe Ramia--kalamumedia" neno tabiri ujio wa uhuru lipo linahusishwa na Shehe Ramia, kutoka kwa wanafamilia. Neno tabiri siyo lazima litokane na kupiga ramli au vilivyoharamishwa kwenye Kurani. Kwa kiingereza ni prophecy nalo kwa kiislamu lina utata. Pengine neno ufunuo ndilo linalolenwa pale tunsposema utabiri. Kwa vyovyote vile maandiko mengi yaliyopo yanatumia neno tabiri na kuhusisha na uhuru na Mwl. Nyerere yakiwahusisha wazee wako wa Kariakoo, Bagamoyo,n.k. Kama ulikuwa hujaiona hiyo video, naomba uitazame na kuitolea maelezo ili usihusishwe na kitu unachopinga!
 
Naifahamu hiyo video.

Lakini mdomo haumkatai bwana wake.

Mimi nimekueleza niyajuayo kutoka utafiti uliomalizikia na kuandika kitabu.

Sijapatapo kusikia popote kuwa kulikuwa na wazee waliomtabiri Julius Nyerere.
 
Misha,
Sijapata kukutana na hii dhana ya kuwa Nyerere alitabiriwa wala hii historia inayoenezwa ya "wazee."

Haya ya wazee ni maneno ya Mwalimu Nyerere.

Nyerere alikuwa na wanasiasa vijana kote alikopita majimboni na wote wanafahamika kwa majina.

Ajabu sana awe hawakumbuki vijana wenzake mfano wa Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, Oscar Kambona, Steven Mhando, Ali Msham, Msham Awadhi, Salum Mpunga, Yusuf Olotu awakumbuke wazee ambao hata kwa majina yao hakupata kuwataja.

..Historia na mchango wa Elias Kissenge kama Katibu wa Uenezi wa Tanu nayo imefichwa kabisa. Na kwa bahati mbaya Kissenge aliposhindwa uchaguzi wa Ubunge mwaka 1965 Tanu na Serikali wakamtupa kabisa. Lakini Kissenge naye ana historia yake ya kuacha kazi ktk serikali ya Kikoloni na kwenda kuwatumikia jamii yake, na baadae kujiunga na Tanu na kuwa Katibu wa Uenezi.
 
JK,
Elias Kissenge yeye alikuwa katika mpango wa Tanga wa kupambana na wajumbe wa TANU waliokuwa wanapinga TANU kushiriki katika Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958.

Nyerere alimchukua Amos Kissenge Tanga akiwa Deputy Secretary General wa TANU akimuacha General Secretary Zuberi Mtemvu Dar es Salaam, TANU HQ New Street.

Nyerere na Kissenge walifanya mkutano huu na uongozi wa TANU Tanga wa akina Hamisi Heri, Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Mwalimu Kihere na viongozi wengine.

Baada ya kufikia makubaliano waliamua kikao kihamie Mnyanjani ili kufanya tawasul (dua) kuomba msaada wa Allah TANU ivuke kizingiti cha Kura Tatu salama.

Historia hii nimeeleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
 
..mikutano ya siri ya Tanu ilikuwa ikifanyika ktk Bar ya Elias Kissenge ikiitwa Churchill iliyokuwa ktk mji wa Same.
 
Hivi ndivyo vitu muhimu kufahamika katika historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nilisoma na Hadi Kissenge mtoto wa Amos Kissenge St. Joseph's Convent School na nilifanya kazi na bint yake Rachael Kissenge East African Cargo Handling Services.
 
Mzee Mohamed Said, " mdomo haumkatai bwana wake"! Utafiti wako ulikoma pale ulipochapisha kitabu? Wewe huoni kinachoitwa reasonable doubt? Au umeziba masikio kabisa mkuu wangu? Medali wangepewa wangapi ndugu yangu? Nchi nzima walishiriki kwa hali na mali, na wengine waliathirika sana na ujio wa uhuru kiuchumu na kijamii, mfano ni watemi/ machifu, viongozi hawa wa kimila wengi wao walitambua fika uhuru ulimaanisha mwisho wa utawala wao hata kabla ya TANU/TAA kuanzishwa! Waliyafanya mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Hivi kuna struggle kama Bwana wa mabwana, Mwamba wa miamba, Mungu wa miungu akisema itakuwa?
 
Hivi unajua kama katika watafiti wa historia ya mwamko wa Waafrika kupelekea kuunda African Association mwaka wa 1929 historia yake inaanza na Dr. Kweggyr Aggrey na Kleist Sykes 1924.

Wasome Kweggyr Dr. Kweggyr Aggrey na Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography (DAB) 2011.

Historia hii ya wazalendo hawa sasa karne moja imepita.

Historia hii imeandikwa na Kleist Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Fika East Africana Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam utaipata historia hii iliyoandikwa 1968 na mjukuu wa Kleist Aisha Abdulwahid Sykes.

Mimi nimebahatika kuisoma historia hii na kusoma Nyaraka za Sykes.

Hakuna mtafiti mwingine aliyebahatika kusoma Nyaraka hizi ukimtoa John Iliffe ambae amesoma baadhi yake.

Hao unaowataja wewe walikuwapo 1924?

Hao unaowataja wewe umeona chochote kutoka kwao kuwa walishiriki katika kuunda African Association 1929, Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislamu wa Tanganyika) 1933, TAA Political Subcommittee 1950 na TANU 1954?

Ndugu yangu wewe unatamani kama na wao wangekuwa na mfano wa haya niliyoandika mimi kueleza ukweli wa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hao wote hawakuwapo na ndiyo màana hukuweza kuwataja kwa majina yao.

Mimi nina orodha ya machifu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Abdul Sykes kuanzia 1950 wakati wa harakati za kuunda TANU.

Mimi nizibeje masikio ilhali ndiye niliyoandika historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika?

Anaeziba masikio ni yule ambae hashangazwi na ukweli kuwa African Association iliasisiwa na Kleist Sykes na rafiki zake halikadhalika Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika.

Anaeziba masikio ni yule ambae hataki kusikia kuwa TAA Political Subcommittee iliundwa na Abdul Sykes 1950 na mmoja kati ya wajumbe ni Mufti Sheikh Hassan bin Ameir.

Anaeziba masikio ni yule ambae hashtuki kuwa Abdul Sykes kadi yake ya TANU ni No. 3 na hatajwi katika historia ya TANU.

Haya hayakuwako katika historia ya Tanganyika lakini hashtuki anataka tubishane kwa jambo ambalo mimi linawahusu wazee wangu.

Yapo mengi mfano wa haya.

Anaeziba masikio ni yule roho inamuuma kuelezwa kuwa Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi za TANU misikitini.

Umepata kusikia popote Sheikh Hassan bin Ameir katajwa?
 
Mzee Mohamed Said, asante kwa maelezo ya kina. Uliandika kuwa unaifahamu video inayomhusu Shehe Mohamed Ramia, je, hiyo video fake news au ni video halisia? Pili nakupa pole kwa msiba wa Prof. Iliffe.
 
Back
Top Bottom