VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,488
- 1,465
MWANANGU kama umezaa na Mwanamke na mkatengana kisha mkakubaliana kumlea Mtoto au Watoto wenu, hakuna ubaya wakati unatuma hela kwa ajili ya Watoto wako basi tia busara kumkumbuka pia Mama yake pia kwa chochote kitu, amini kuna muda anashindwa kufanya mambo yake kwa ajili ya damu yako.
Mapenzi yanaweza kuisha ila tuthamini mwili wake, tuthamini utayari wake kubeba mimba yako, uthubutu wake kuingia Leba kupigania Uhai na Kifo, tukubali hakuna pesa inazidi alichofanya Mama wa Mtoto wako, tuwathamini sio kila Mwanamke anaweza.