Heri ya siku ya Wanaume Duniani!

Heri ya siku ya Wanaume Duniani!

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
7,812
Reaction score
20,004
Siku ya Wanaume Duniani ilianzishwa na Dr. Jerome Teelucksingh, mhadhiri kutoka nchini Trinidad and Tobago,nchi ya visiwa iliyoko Caribbean.

Ilianzishwa rasmi tarehe 19 Novemba 1999.

Aliona wanaume wengi wanapambana kimya kimya, wanabeba majukumu makubwa lakini hawatambuliwi, na wengine wanateseka na msongo wa mawazo bila kupewa nafasi ya kuzungumza.

Lakini pia aliona jinsi baba yake alivyokuwa mfano bora wa kuwa Baba, ndiyo maana alichagua tarehe ya kuzaliwa kwake. Alitaka siku ambayo wanaume watathaminiwa kwa mchango wao chanya.

Umuhimu wa Siku Hii

Siku hii ni muhimu kwa sababu inatukumbusha kuwa wanaume pia ni binadamu. Wanahitaji kupendwa, kusikilizwa na kuthaminiwa.

Inahimiza afya ya mwili na afya ya akili, kupinga dhana potofu kuwa mwanaume hasikii kulia au kuomba msaada.

Pia inahimiza usawa na heshima kati ya wanaume na wanawake, ili tuijenge jamii yenye upendo na amani.

Mwanaume ana jukumu la kuwa nguzo ya familia, kiongozi mwema, mlezi na mlinzi. Anatakiwa kuwa mfano bora kwa watoto na kizazi kijacho,

kuongoza kwa hekima, uwajibikaji na upendo. Anatakiwa kusimamia familia yake kiuchumi, kiroho na kihisia, na kuwa mwaminifu katika ndoa, kazi na huduma yake kwa Mungu na jamii.


Kwa wanaume wote, tunawatakia Heri ya Siku ya Wanaume Duniani! Mungu awape afya njema, hekima, nguvu na mafanikio katika kila hatua.

Msiogope kuomba msaada, msikate tamaa. Mnathaminiwa, mnapendwa na mna thamani kubwa.

Endeleeni kusimama imara, mkiwa baba, kaka, mume na kiongozi bora.

♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️♥️
 
Screenshot_20261110-150711~2.jpg
 
Back
Top Bottom