Kwanza kabisa nawasalimu wana JF mwenzenu ndio nimetoka KARATU JUZI NAISHI JIRANI NA DR Wilbroad Slaa, nimevutiwa sana na ujumbe uliotolewa na Mzee wetu Alhaji A. Mwinyi kwamba tusifanye makosa ya kumchagua Slaa au upinzani, kwa kweli ni kweli tupu kwani pale kanisani alipokuwa anapaongoza pamevurugika, ukoo umesambaratika hawajui anataka mchumba wa aina gani mwenye heshima kama Rose Kamili, lakini wengi wanahoji juu ya mali za kanisa, wengi wasema hata angegombea ubunge safari hii wasingempa amekosa sifa ya maadili , kiongozi lazima awae mfano wa kuigwa kwa tabia na matendo na hasa kauli zake, huyu bwana Slaa atatufikisha pabaya.
Usifanye makosa chagua KIKWETE 2010
Kutenda kosa si kosa kosa kurudia kosa. Najua utanielewa ila sina hakika kama utajirekebisha.
1. Kiongozi huongoza watu si mapenzi. Ndani ya miaka 15 ya uongozi wa Dr. Slaa Karatu linganisha na miaka aliyoongoza JK Bagamoyo (tembelea na Bagamoyo).
2. JK tulimpa miaka mitano, akasema alikuwa anajifunza Urais. Tukumbushe Nyerere, Mwinyi na Mkapa walijifunza wapi urais? Pia muulize baada ya kujifunza kagundua nini?
3. Katika kipindi cha kujifunza urais, JK alisema hajui kwanini watanzania ni masikini. Je, sasa amepata jibu la kwanini watanzania ni masikini.
4. Tulipompa JK nchi kwa mara ya kwanza alisema urais wake hauna ubia. Je, sasa urais wake una ubia? Ni wa familia? Ama ni wa marafiki?
5. Miaka 5 ya kazi yake JK alikuwa anazunguka duniani kutafuta wafadhili (Matonya), je, kopo lake limeingiza kiasi gani?
6. Uchumi wa nchi umeanguka, pesa ya Tz imeanguka, ndani ya miaka mitano ya JK Shilingi ya Tanzania imeanguka kwa Shilingi ya kenya kwa karibu shilingi kumi (Ksh. 1 = Tshs. 18), huoni kama ni tatizo?
7. JK alikupa kamsemo, akili za kuambiwa!!!!!!!!! Leo sukari ni 1800 kwa kilo, huwa Mzee ruksa anakupatia pesa ya sukari?
8. Hakukosea Mkapa aliposema watanzania ni wavivu wa kufikiri. Fikiria kidogo, hayo maisha ya kutojua kesho utakula nini ndiyo unayopenda.
Kiongozi asiye na vision hatufai, kiongozi anayehonga ili kwenda ikulu ni sawa na ukimwi.