Upumzike kwa amani mwanamapinduzi wa kweli,walikuhujumu lakini wanaanza kuumbuka,kwenye chama chako umemuacha Kijana wa Kigoma Kaskazini pekee mwenye misimamo kama yako ila nayeye amekua akipigwa vita sana na chama,waliobaki wanawaza zaidi magogoni na sasa wanatumia mbinu chafu kama ile walioitumia kwako,ulikua mtetea haki uliyejali maslahi ya taifa na sio ya chama chako,uliyekua tayari kusema hapana kwa mabosi zako pale walipo toa maagizo yasio na dhamira njema kwa taifa,ulikemea ukabila,ukanda undugu na kujuana ndani ya chama.
Mkurugenzi wa usalama wa chama chako huku yupo matatani dola imemng'ang'ania na uchunguzi unaendelea. Watanzania wanasubiri ili wafaham ukweli wa muda mrefu uliokua kama vuguvugu juu ya maasi ya chama chako.
Unajua hata wewe ulipoondoka uliacha minong'ono mingi.
RIP sisi bado tupo ila tunakukumbuka kwa dhamira na misimamo yako ya kulitetea taifa.