Bado nakulilia Chacha Wangwe!

Bado nakulilia Chacha Wangwe!

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,080
Reaction score
3,771
Ulikuwa mwanasiasa hodari, ambaye usiyekuwa na habari,
Usiyekuwa na ufahali, wala usiyejilimbikizia mali,
Mwanasiasa uliyeona mbali, ila hukuona ile ajali,
bado nakulia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe

Zamani nilikutambua, kabla ya wengi kukujua,
Kabla mnyoa kipara hujakua, ila mfuga dreds ulikuwa,
Nyerere akakuumbua, nyoa nywele halafu ubunge utakua
Bado nakulilia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe

Safari yako ilikuwa na mengi, na iliwakasirisha wengi
Kifo chako kilishtua wengi, utakumbukwa na wengi,
Chama chako kina matatizo mengi, masalia wamekuaa wengi
Bado nakulilia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe

Hukumuogopa mtu, usoni uliwapa makavu
Ulijali utu, na kuwapa zao laivu
Ajali ilikuchinja kama kuku, bila ya wewe kula zako mbivu
Bado nakulilia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe

Huku tunaendelea, watu wanataka uraisi
Yale uliyoyakemea yanaendelea, wengine wanageuka mafisi
Kukulilia naendelea, uliowatetea wamekumiss
Bado nakulilia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe

Note
Sijafuata taratibu zote za uandishi wa shairi ila nimeweka katika mfumo wa shairi ili iwe na utofauti fulani
 
May God rest his soul in peace,huyu ndo angekuwa sokoine wetu,alikuwa ni jembe balaa,hakuwa na shobo wala makuu,yeye ni kazi,ulazwe pema mpiganaji
 
Bwana alitoa,bwana alitwaa,jina la bwana lihimidiwe!
 
Ulale pema Kamanda! uliipenda Chadema kweli kweli!
 
Nahisi Masalia wanaweza wakaaribu shairi lako mkuu... R.I.P Chacha Wangwe..
 
Kuna nini jamani, mbona mnatukumbusha machungu?
hii ni hoja ya masalia iliyowasilishwa kisanii!sisi wasanii tuliobobea tumeshajua itaishia wapi.funguka mkuu... Usigeuke panya Jimmy
 
Last edited by a moderator:
RIP shujaa.Alikuwa mpambanaji kama Mbowe,Dr Slaa na Lema.Unatukumbusha machungu.
 
unatukumbusha mbali.asante kwa ukumbusho wako na ushairi wako.tunachojali ni ujumbe.
 
nipo nasoma kitabu cha mauaji ya chacha wangwe na historia yake..hiki kitabu utamjua mnyika ni nani,mbowe na mrema.

Lakini soma signature yangu ipo siku utaniambia kitu
 
nipo nasoma kitabu cha mauaji ya chacha wangwe na historia yake..hiki kitabu utamjua mnyika ni nani,mbowe na mrema.

Lakini soma signature yangu ipo siku utaniambia kitu

Oooh!chacha mpiganaji ama kweli watetezi wetu huteketezwa kama uyoga wewe chacha na AMINA chifupa mlazwe pema peponi,
 
naona mnafufua mizimu xaxa....! unamlilia nini na wewe kama cio kamchezo kako tu hapo..? TANZANIA YAPO MENGI YA KULIA, umeona hilo tu mkuu c. t. u?
 
Too late!askari mmoja akifa silaga haziwekwi chini na kufanya maombolezo!songeni mbele na mapambano,watakumbukwa baada ya ushindi kupatikana.
 
nipo nasoma kitabu cha mauaji ya chacha wangwe na historia yake..hiki kitabu utamjua mnyika ni nani,mbowe na mrema.

Lakini soma signature yangu ipo siku utaniambia kitu

Najua una hasira sana baada ya Mbowe kusema Dr Slaa Tosha.Ndiyo mjue nguvu ya uchawi ni uchafu mbele ya Mungu.
 
RIP chacha wangwe even if that time nilkuwa si mwanachama bali mshabiki wa kijana aliyekuwa mpambanaji Zitto lakin sasa katusaliti na kutupa kisogo, BUT i thank God katupa tumaini jipya mkombozi Dr.Slaa.

R.I.P CHACHA WANGWE.
 
Ni pm nikupe copy ya kitabu chenye mpango mzima wa mauaji ya chacha wangwe kilichoandikwa na msaaidizi wa mwenyekiti wa chadema taifa Mbowe,Msaidizi huyo anaitwa deo meck.
Naye alisakwa kuuwawa lakini mungu wa mbinguni akamuokoa.Hiki chama kina wenyewe na wenyewe ni Mbowe mnyika,Mushi na Kimario
 
Back
Top Bottom