uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. The Watchman

    JamiiForums Tanzania GE2025 Stephen Wasira: Itakuwa jambo la busara kama CHADEMA watashiriki uchaguzi, tunasikitika wana matatizo mengi

    Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Stephen Wasira amesema Itakua jambo la busara kama CHADEMA watashiriki uchaguzi mkuu. Aidha Wasira amesema walikutana na chama hicho chini ya mwamvuli wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chini mwenyekiti wake Tundu Lissu ili kujadili tofauti zilizopo kati ya vyama...
  2. McLaren

    JamiiForums Tanzania Luguba na Kombani wang'ara kwenye Uchaguzi UWT Morogoro

    Wagombea wawili Kati ya wagombea 9 wameibuka Vinara Katika Mkutano Mkuu Maalum wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Morogoro Uliolenga kuwapata wawakilishi wanawake kutoka mkoani humo watakaoshiriki katika hatua ya kitaifa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Soma pia: Kuelekea Uchaguzi...
  3. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Richard Nzagi: Muhamiaji Haramu akiingilia Uchaguzi Faini Sh Milioni 5 au kifungo cha Miaka mitatu au vyote

    Mlishawahi baini wahamiaji haramu wakitaka kujihusisha na uchaguzi au amsuala ya kiasisa kiujumla mnafanyaje kwenye hili?? Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Richard Nzagi, akifanya mahojiano na Kituo cha Shamba FM Radio anajibu... Pia soma ~ Richard Nzagi: Mafinga ina Watoto wengi...
  4. R

    JamiiForums Tanzania Toa neno moja kwa wajumbe wa CCM kuelekea uchaguzi wa wagombea ubunge na Udiwani 2025 ndani ya CCM

    Kwangu mimi wale pesa kura wapeleke kwa mtu sahihi .
  5. Mohamed Said

    JamiiForums Tanzania Bongo Plus na Uchaguzi Mkuu 2025: Wanatafuta Historia ya Vijana wa Kale na Vijana wa Leo Katika Siasa

    Leo Maktaba ilitembelewa na Mtangazaji Victor Madaha wa Bongo Plus kutafuta historia ya vijana katika siasa kuanzia kudai uhuru wa Tanganyika hadi leo. Victor anasema kasukumwa kwa kuona wimbi kubwa la vijana kuingia kwenye kinyang'anyiro kuwania nafasi za uongozi katika taifa kwenye uchaguzi...
  6. S

    JamiiForums Tanzania Mchungaji Kimondo: Wanajua uchaguzi ukiwa huru, wa kifuata utaratibu na haki CCM hawawezi kupita

    Mchungaji mstaafu wa KKKT Dkt. Steven Kimondo amesema kuwa chama cha mapinduzi hakitaki kufanya mabadiliko/reforms zinazoombwa ni kwa sababu wanajua uchaguzi ukiwa huru na haki hawawezi kushinda. Mchungaji Kimondo amerejelea maneno aliyowahi kuyasema Balozi Humphrey Polepole kuwa CCM ikifanya...
  7. Genius Man

    JamiiForums Tanzania Kuvunja katiba za chama na nchi kwa kuvuruga utaratibu au kuiba kura ni uhaini na ukuwa unajaribu kuzuia uchaguzi

    Kuzuia uchaguzi ni pamoja na kuiba kura, kutoa rushwa na kuvunja mchakato wa kupatikana wagombea ndani ya chama na kuvunja katiba ya chama. Kuzuia uchaguzi sio kusema unataka mabadiliko au maboresho ya kiuchaguzi bali ni kile kitendo cha wizi, rushwa na uvunjifu wa katiba ya nchi na chama...
  8. Raia Fulani

    JamiiForums Tanzania GE2025 Wajumbe ni WATU NA NUSU. Hatima ya utawala bora iko mikononi mwenu kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu (Upande wa CCM)

    Ni nani wajumbe hao? Ni walioko kwenye Kamati Kuu ya CCM Taifa (National Executive Council – NEC), pamoja na wajumbe maalum wa kutoka mikoa (Wilaya/Mkoa) na vyama vya UWT, UVCCM, Wazazi nk, ambao wako kwenye ngazi za uchaguzi wa ndani. CCM imeongeza idadi na nafasi kwa wajumbe kutoka vikao vya...
  9. kavulata

    JamiiForums Tanzania Wapiga kura tusichague wacheza kamari uchaguzi ujao, watoto wetu wanaathirika

    Kamari zimetapakaa hadi kwenye vitongoji vya vijijini kila mahali penye umeme nchini. Redio zote kuanzia za umma na watu binafsi zote ni kamari tu. Kijijini nimeshuhudia kijana kauawa kwenye dubwi kwa kugombea TSH 4000 tu wakati wakibishana juu ya nani amekula, ni za nani. Wanafunzi wanabet...
  10. The Zanzibar Echo

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi Tanzania 2025: Kwa nini idadi ya wapiga kura Tanzania 'inazua maswali'?

    Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC) imejikuta katikati ya mjadala baada ya kutangaza kuwa idadi ya wapiga kura katika daftari la kudumu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imefikia milioni 37.6. Takwimu hizi zimezua maswali mazito kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati...
  11. Mpepetaji

    JamiiForums Tanzania GE2025 Kaliua yanunua mtambo wa shilingi bilioni 1.2 wa kutengeneza barabara, siku zote walikua wapi wanategea tukikaribia uchaguzi?

    Wakuu Hii mitambo ya kutengeneza barabara inanunuliwa sana kipindi hiki kuelekea uchaguzi, siku zote wanakuwa wapi? au ndo kura zinatafutwa kwa kuhadaa wananchi. Alafu mtambo huo huo baada ya uchaguzi utakuta unaharibika:AAAA: ===== Mbio za Mwenge wa Uhuru umezindua mtambo wa kutengeneza...
  12. Idugunde

    JamiiForums Tanzania Kwa huu mnyukano ndani ya CCM kama CHADEMA Ingeshiriki uchaguzi ingeshinda kwa kishindo kama uchaguzi wa 2010

    Uchaguzi wa 2010 CHADEMA ilipata matokeo mazuri sababu CCM ya wakati huo ilikuwa imepoteza imani kwa wananchi. Na kulikuwa na mpasuko na makundi makubwa. Mwaka huu kwa CHADEMA hii ambayo inakubalika na huu mparaganyiko ndani ya CCM CHADEMA wangeshinda kwa kishindo na kupata viti vingi zaidi ya CCM
  13. OleWako

    JamiiForums Tanzania Tufanye Mahesabu ya waliojiandikisha kwa Uchaguzi Mkuu: 37.7M - 35.3M = ?

    Watu Milioni 2.6 Zaidi? Hebu Tuchambue Kwa Kina.. Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilitangaza kwamba jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha kwa uchaguzi mkuu ujao. Kwa mujibu wa Sensa ya 2022, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ilihesabu kuwa Watanzania 35,341,132 waliokuwa na umri wa zaidi ya...
  14. Son of Israel from Africa

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi wa Mwaka huu hauna mvutooo

    Wanajumuia . Salamu kwenuu Leo nimetafakari sanaa. Lkn mwisho wa siku nikagundua UCHAGUZI WA MWAKA HUU HAUNA MVUTOO KABISAAA . NAONA TUME INAFANYA TUU ILIKUFATA UTARATIBU NA MAELEKEZOO. HUKO CCM UNAONA WENYE MAAMUZI WENYEWE HAWANA NURU WAPO TUU WAMEPOWA KAMA PIRITON WAPO TUU KUTIMIZA WAJIBU
  15. SSH2025_2030

    JamiiForums Tanzania GE2025 Uteuzi wa Wagombea CCM ndio Uchaguzi Mkuu wenyewe!

    Kama ulikua hujui kwenye uchaguzi wa Wagombea CCM ndio Uchaguzi wenyewe sasa. Mengine NI kukamilisha ratiba. Asanteni. Lucas Mwashambwa
  16. K

    JamiiForums Tanzania Kama Mfaume Mfaume kashinda hilo pambano na mmalawi, tusilaume tume za uchaguzi Afrika kupanga matokeo

    Kwa aliye angalia pambano la Mfaume dhidi ya mmalawi atakuwa alipigwa na butwaa kwa kile kilichoamuliwa na majaji. Kwa kuwa tunapenda uzalendo kuliko uhalisia basi tusahau maendeleo ya mchezo wa maswimbi Tanzania .Ni aibu. Mfaume alipigwa mpaka ukumbi ulikuwa kimya wakati wote wa mchezo...
  17. N

    JamiiForums Tanzania GE2025 Afrika ukifanyika uchaguzi wa uhuru ni Marais wachache watabaki kwenye viti vyao kina Ibrahim Traoré wa Burkina Faso na Hichilema wa Zambia

    Hali ya demokrasia imekuwa ni mbaya kupitiliza kila kukicha Viongozi sio chaguo la wananchi na wanafanya kila namna kuhodhi madaraka kwa dola na yeyote anaekuwa tishio kwenye nafasi zao hushughulikiwa
  18. L

    JamiiForums Tanzania DOKEZO Wilaya ya Kondoa Rushwa ya Uchaguzi inagawiwa nje nje. TAKUKURU mko wapi?

    Tulisikia kuwa TAKUKURU watakuwa macho sana na vitendo vyaRushwa wakati hiu wa uchaguzi. Inawezekana hili likawa kweli au siyo kweli. Huku kwetu Rushwa inagawanywa waziwazi mchana kweupe. Katika kura na maoni za UWT, mbunge wa Kondoa alipewa kazi ya kusafirisha wajumbe kutoka maeneo yote kwenda...
  19. The Zanzibar Echo

    JamiiForums Tanzania Uzi wa ushauri, mapendekezo, maoni, ujumbe, changamoto, masuali, na duku duku kuhusu siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu.

    Kila mwenye maoni ushauri changamoto mapendekezo duku duku suali kuhusu kinachoendelea katika siasa za Tanzania na kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu aje hapa
  20. Dalton Elijah

    JamiiForums Tanzania Admin wa Tume Huru ya Taifa Uchaguzi amefanya kwa Makusudi au ndio ukweli? Chapisho lililopo kwenye tovuti lina makosa ya uandishi!

    Tume huru ya uchaguzi wametoa chapisho ambalo lina makosa ya kiuandishi jambo ambalo sio la kawaida kwa taasisi.. kwanza kabisa mwanzoni linasomeka hivi.... Tume Huru ya Taifa ya Uchafuizi imetangaza kuwa Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Siku ya Jumatano ya tarehe 29 Oktoba, 2025...
Back
Top Bottom