uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Nyamsusa JB

    JamiiForums Tanzania Ripoti kutoka Kijiweni kwako kuhusu Upepo wa Kisiasa na Uchaguzi 2020

    Wanajanvi Tupeane Ripoti ya Upepo wa Kisiasa unavyoendelea kijiweni pako kadri ya siku zinavyoenda. Hapa kijiweni pangu napocheza Drafti kila jioni hali kidogo imebadilika baada ya Tundu Lissu kuteuliwa kugombea Uraisi wa JMT. Sifa kidogo alizokua akipewa Mfarume wa Uajemi zimepungua sana. Na...
  2. kavulata

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi 2020: Ilani ya CCM inasema nini kuhusu kurejesha viwanja serikalini/TFF?

    CCM haiwezi kuinua Michezo nchini Kama itaendelea na sera yake ya kuvishikilia viwanja vya Michezo nchini na bila kuvifanyia matengenezo makubwa. Inasikitisha Sana wadau wa Michezo kuhusu hili kwasababu Michezo haina chama. Viwanja vinachangia timu zetu kuwa kichwa Cha mwendawazimu. Wapenda...
  3. feyzal

    JamiiForums Tanzania GE2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

    Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa...
  4. MAHANJU

    JamiiForums Tanzania GE2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

    Kama ambavyo siku zote nimekua nikisema kua mimi ni mkweli daima na fitina kwangu mwiko. Ni MwanaCCM hai niliyekitumikia muda mrefu na bado naendelea. Rais wangu ulikosea mambo machache sana pamoja na mengine mengi makubwa uliyofanya. MAISHA MAGUMU KWA WATANZANIA Mwenyekiti wangu, maisha ni...
  5. S

    JamiiForums Tanzania Viongozi wa CHADEMA Taifa mna uhakika kesho ofisi za Tume ya Uchaguzi zitafunguliwa?

    Kwakuwa kesho ni sikuku ya Nanenane (Public holiday), ofisi za serikali/ umma huwa hazifunguliwa isipokuwa kwa baadhi tu ya ofisi au Taasisi ambazo kulingana na nature ya kazi zao,ofisi zao huwa hazifungwi. Kwa msingi huo, NEC kesho watafungua ofisi zao? Au katika ratiba waliyotoa ya...
  6. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania RPC Muroto ni wajibu wako kumlinda Mgombea Urais Lissu atakapokuja Dodoma kuchukua fomu ofisi za Tume ya uchaguzi

    Nimeona nikukumbushe mapema kuhusu jambo hili kutokana na umuhimu wake . Lissu alishambuliwa mchana Dodoma , hatuna haja ya kukumbusha yaliyojili , bali itoshe tu kusema kwamba hakuna juhudi zozote zilizofanyika ili kuwabaini washambuliaji , bali sarakasi na danadana tu ndio zilizotamba , TUKIO...
  7. Q

    JamiiForums Tanzania GE2020 Angalizo Uchaguzi wa Mwaka huu; NEC/ZEC msicheze na sanduku la kura ni 'Bomu'

    Kwa hali ilivyo uchaguzi wa mwaka huu wa Oktoba ni kama bomu linalosubiri kulipuka, usipoendeshwa kwa tahadhari Tanzania inaweza kuandika historia mpya. Navikumbusha Vyombo vya Dola, Msajili wa vyama, Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC na viongozi wote wa vyama vya siasa na serikali kuepuka maneno...
  8. Q

    JamiiForums Tanzania GE2020 Mgombea Urais kupitia SAU, Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza wamewasili Ofisi za NEC peku kuchukua fomu

    #Uchaguzi2020 Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza Satia Musa, walipowasili hii leo Agosti 7, 2020, kwenye ofisi za NEC wakiwa peku bila Viatu kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ. Mwenyekiti...
  9. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Dar: Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi, Yeremia Kulwa Maganja ateuliwa kuwania Urais Tanzania

    Heshima kwenu Wakuu, Leo nccrmageuzihq Wanafanya MKutano Mkuu ambao unafanyikia katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar Es Salaam. Mwaka huu NCCR wamejipanga kushiriki Uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba kikamilifu. Dira na Madhumuni ya NCCR ni Kuwa chama chenye nguvu kinachofuata itikadi ya...
  10. T

    JamiiForums Tanzania GE2020 Tundu Lissu ana marafiki wa kificho, Rais Magufuli ana maadui wa kificho

    UCHAGUZI wa mwaka huu unatakuwa ngumu na wenye mvuto mkali. Hii ni sawa na pambano lililosubiriwa kwa muda mrefu. Mapambano kama haya yakitokea hulazimisha shughuli zingine zisimame ili kupisha mpambano mkali na wenye mvuto. Hivi ndiyo ninavyoona uchaguzi wa mwaka huu. Siyo uchaguzi wa CCM VS...
  11. Sophist

    JamiiForums Tanzania Benki Kuu ya Tanzania yatoa maagizo juu ya uendeshaji wa Fedha za Kigeni

    Benki Kuu imetoa dokezo la kisera (fedha) kudhibiti zaidi upatikanaji wa fedha za kigeni. Sera hii inapunguza upatikanaji wa fedha za kigeni kwa ajili ya miamala ya kimataifa (export revenue) na kitaifa au kuharamisha biashara za fedha za kigeni kuoitia mitandao kwa miezi sita (6) ijayo Katika...
  12. Masokotz

    JamiiForums Tanzania Wagombea wengi wazuri wanakwamishwa na gharama za Uchaguzi

    Ndugu wajumbe, Leo napendekeza tujadili hili suala gharama za Uchaguzi jinsi linavyosababisha viongozi wazuri na wenye maono makubwa kukosa nafasi za uongozi hata wa kata. Hili ni jambo ambalo linaleta ubaguzi,na wakati mwingine linasababisha rushwa wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi...
  13. Nzelu za bwino

    JamiiForums Tanzania GE2020 Uchaguzi wa October 2020, mtihani wa kwanza kwa Dk. Bashiru na Polepole

    Salaam wanajamvi, Oct 2020 kutakua na uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais wa nchi. Uchaguzi huu ni wa kwanza kwa katibu mkuu na katibu mwenezi toka wateuliwe, ni uchaguzi huu utakaoonyesha uwezo wao wa kupangua na kupanga hoja kwenye mikikimikiki ya kampeni. Tulizoea kuwaona...
  14. K

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kuna uwezekano wa nchi hizi zikatumika katika kudukua Mfumo wa Uchaguzi. Intel za Serikali kuweni macho

    Ndugu zangu, Napenda kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai na kutufanya tuione siku ya leo. Kuna jambo moja hapa nalileta kwenu wadau ili tulifanyie analysis kwa pamoja, ambalo linamhusu huyu dogo, I think you understand whom I'm referring to. Dogo kasema kazunguka sana katika nchi za Ulaya na...
  15. T

    JamiiForums Tanzania Kwa hija hizi CHADEMA ni afadhali msishiriki Uchaguzi Mkuu 2020

    Vitus Nkuna: Tumepata Shida Sana. Jibu: Hizi ni kelele na wala sio hoja. Hujasema wazi ni shida zipi, kwani zipo shida za uvivu, shida za ndoa n.k. Muungwana hasemi kama hana ushahidi wa kusema wazi. Mjinga anasema kwa kuwa ni kawaida kusemasema ovyo ovyo! Vitus Nkuna: Ndugu zetu wamepotezwa...
  16. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 NCCR yasema wako tayari kushirikiana na CHADEMA na vyama vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu!

    Mkurugenzi wa mawasiliano wa NCCR Mageuzi Dr Edward Simbeye amesema chama chake kiko tayari kushirikiana na vyama vingine vyenye mrengo wa demokrasia katika uchaguzi mkuu. Source: East Africa Radio
  17. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Fomu namba 8A ndiyo itakayombana Tundu Antipas Lissu, ni ya Maadili ya Uchaguzi

    Fomu hii namba 8A inatakiwa kujazwa na wagombea wa Urais mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu. Ni ya kuahidi kulinda, kuheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi na taratibu zake. Ukitenda kinyume cha maadili ya uchaguzi unaweza kuenguliwa kwenye uchaguzi wakati kampeni zikiendelea. Kwa hiyo wagombea...
  18. TODAYS

    JamiiForums Tanzania Wababe hawa wa mwaka 2015 watasaidia kupindua meza Oktoba 2020?

    Uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakisiwa kuwa ndiyo uchaguzi utakaokuwa na changamoto zenye hisia na usio lelemama. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kuna mambo yalifanyika kwenye kutuma na kupokea matokeo ya sehemu flani zilizoonekana kumbeba mgombea mmoja na baadae kura kuyumbishwa na kurekebishwa...
  19. Nyani Ngabu

    JamiiForums Tanzania GE2020 Tusemezane: Uhalisia wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

    Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi. Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla...
  20. Idd Ninga

    JamiiForums Tanzania Madhara ya Rushwa katika Uchaguzi

    #UchaguziMkuu2020Tz.
Back
Top Bottom