maandamano

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. GenuineMan

    Mkiandamana achaneni na kuharibu mali za umma au za watu

    Kuharibu Mali za Umma au za mtu yeyote sio njia nzuri ya kufanya demonstration. Hizi Mali za Umma, ni kodi zetu ndio zinatumika kujenga. KWa akili ya kawaida tuu kituo cha mwendokasi au kituo cha polisi hakuna faida yoyote ukikichoma moto, zaidi ya hasara. Maandamano kwa watu waliostarabika...
  2. Y

    Maandamano ni batili, vijana tusitumike

    Vijana wengi tunatumika kwa maslahi ya wengine,wengi walio poteza uhai niwale wafata mkumbo. kikundi Cha wezi walikua wanachoma sheli, wanavunjaa maduka ya watu wanaiba alafu wanakimbia vichochoroni wemfata mkumbo unabakii unatumika kama ngao yakuwazuia police bila kujua watu wapo kwenye misheni...
  3. Mshana Jr

    Uzushi uliozushwa katikati ya kilele cha maandamano

    Jioni ya tarehe 29. 10. 2025 Bali ilikuwa mbaya sana kwenye miji mingi mikuu Tanganyika.. Maandamano yaliyoambatana na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu yalikuwa yamepamba moto Mawasiliano yalikuwa ya shida kwakuwa mitandao ilikuwa imezimwa na mamlaka zikakosa kujua athari za ueneaji wa...
  4. Dalton Elijah

    Kipi Kifanyike Nchini Tanzania Baada ya Vurugu za Uchaguzi na Maandamano Yaliyosababisha Vifo?

    Kufuatia vurugu za uchaguzi na maandamano yaliyosababisha vifo nchini Tanzania, hatua madhubuti zinahitajika kuchukuliwa ili kurejesha amani, utulivu, na kuimarisha demokrasia. Hali kama hii mara nyingi huashiria mgogoro wa kisiasa na kijamii unaohitaji mbinu za kina na shirikishi kushughulikia...
  5. Bushmamy

    Tetesi: Arusha: Maandamano yaanza upya Leo

    Hali sio hali Kwa Sasa Maandamano yameanza upya Morombo, Ngaramtoni na arumeru. Ntaleta update ya kinachoendelea. Baadhi ya maeneo yenye vurugu wananchi wapewa amri ya kutoka kutoka nje . Madai ya wananchi ni kuhusiana na kupewa miili ya ndugu zao ambayo haijulikani ilipo Hadi Sasa.
  6. DuaZaMama

    PostGE2025 Video: Yaliyofanyika si maandamano ni uharibifu, jaribio la mapinduzi ni tafsiri ya UGAIDI

    Wakuu nimekutana na andiko hili... Ni nani aliwapa ujasiri wa kuchoma mali za watu wasio na hatia?Ni nani aliwapa moyo mgumu kiasi cha kufunga barabara ambazo hata mgonjwa aliyehangaika na pumzi yake ya mwisho alipitia? 🚑 Mamilioni ya jasho ya mtu mmoja yaligeuzwa majivu ndani ya dakika...
  7. M

    Barua ya wazi kwa shangazi Maria Sarungi: Ni makosa makubwa ya kimkakati kuitisha maandamano mengine hivi karibuni

    Shangazi wa Taifa Maria, pole sana kwa harakati zako za kupigania haki, na Tanzania yenye demokrasia ya kweli, maendeleo kwa watu na kupinga ufisadi na ubadhirifu na kila aina ya dhulma nchini. Nitoe pole nyingi sana kwa Watanzania waliofiwa na ndugu zao kutokana na yaliyojiri katika maadamano...
  8. Its Tesha

    Maskini: Mimi maandamano yananisaidia nini? Acha raia wapigwe shaba tu!

    Naomba tupate KOMENTS fupifupi juu ya uyu mwamba ambaye ameridhika na umaskini mpaka kufa kwake.
  9. The Burning Spear

    Maandamano yajayo hatushoboki na JWTZ. Wao ndo wataamua watuue au waungane nasi

    GT Tulijipa matumaini hewa kwamba tuna JW inayodhamin̈I maisha yetu kumbe ni wahuni wachumia tumbo. Amini nawaambia hawa jamaa walisaidia police kutuua 100%, JW walipiga san̈a risasi hasa nyakati za usiku mchana wanajifanya wapole. JW na Police lao ni moja kulinda.mafisadi ya CCM na wala siyo...
  10. M

    Kuelekea Maandamano endelevu mpaka uhuru

    Kuanzia sasa Gen-Z/Watanzania kwenye kila maandamano au tukio ambalo litawafanya washike Silaha hawatairudisha kwa mamlaka, Silaha zitatumika dhidi ya WanaCCM na wafuasi wao, polisi au mtu yoyote wa Serikali dhalimu atakayekuja kupeleleza hatopewa tena tena ushirikiano, effectively tunaondoa...
  11. Mangwea1900

    Maandamano au vurugu?

    Tuzungumze ukweli kuhusu kilichotokea ni maandamano au vurugu? Walipovunja maduka yetu na kutupora hela ilikuwa ni sehemu ya maandamano au vurugu? Kilichotokea nani alikuwa akiratibu na yeye alikuwa nasi road au? Tupeane pole ila majeraha yake yatadumu kwa muda mrefu
  12. Kitimoto

    Mashabiki wa Mpira Tugomee Kuhudhuria Mechi za Simba na Yanga kwa Kushindwa Kutoa Pole kwa Wafiwa Kutokana na Maandamano ya Oktoba 2025 ya Kudai Haki

    Katika tukio ambalo limegusa mioyo ya wengi, mashabiki wa soka nchini Tanzania tujipamge kuonyesha mshikamano na majonzi kwa wale waliopoteza maisha katika maandamano ya kudai haki yaliyofanyika kuanzia tarehe 29 Oktoba 2025 ambapo familia nyingi zimepoteza wapendwa wao katika mfululizo wa...
  13. Keynez

    Haya mambo yalitokea kabla tu ya maandamano ya kihistoria Tanzania ya MO29

    Niliwahi kuleta uzi kuelezea mambo kadhaa yaliyofuatana kabla tu ya Mapinduzi (kama unaweza kuyaita hivyo) yaliyomtoa Robert Mugabe madarakani. Nia ni kuonyesha kwamba kulikuwa na "clues" kama ungekuwa na jicho la tatu la udadisi. Leo nitatoa list ya mambo kadhaa yaliyotokea kabla tu ya...
  14. nzalendo

    Hawakuwa kwenye maandamano

    Lakini walipoteza maisha. ...1.... Alikuwa ni Daktari akajeruhiwa na risasi...akapata matibabu muhimbili...SIku ya 3 akafariki...nduguze walipofuata mwili...hawakupewa. ..2...Alikuwa mama wa nyumbani wa watoto wa 3...alikuwa anatoka gengeni...akapatwa na risasi na kufariki papo hapo...
  15. Damaso

    Ukweli mchungu wa vifo vya watu wasio na hatia wakati wa maandamano nchini Tanzania

    Ni huzuni kuu inayotanda mitaani. Machozi yanayodondoka kwenye nyuso za mama waliopoteza watoto wao, kelele za huzuni za ndugu wanaojaribu kuelewa kwa nini wale waliokuwa wakidai haki leo wamelala milele. Tanzania, nchi iliyojulikana kwa amani na utulivu, leo inajikuta ikitikiswa na maswali...
  16. Tajiri Tanzanite

    Hili swala la kuhusisha Kenya na maandamano hapa Tanzania linaweza kuzaa jambo kubwa mno

    Hapo vip!! Kama kuna ukweli juu ya hili basi kutakuwa upunguvu wa watu wenye akili na wanaoweza kufikiri sawa sawa. Kama kuna propaganda zinazoandaliwa eti kwa lengo la kuhusisha kenya au kuichafua kenye yakwamba wanahusika na haya maandamano Basi tukubalianane na haya. 1.Nchi yetu haipo salama...
  17. Genius Man

    Nampongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa na jeshi zima la mkoa huo kutokuwa na mauaji ya raia kwenye maandamano

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa ameeleza kuwa hakuna mwananchi au askari Polisi wa Jeshi hilo Mkoani humo aliyejeruhiwa au kupoteza maisha kutokana na Vurugu zilizotokea siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025. Hata hivyo nawapongeza kwa kuwaachia huru vijana mia 300...
  18. Analogia Malenga

    Waliokamatwa kwa maandamano waachwe huru

    Niliona polisi wakiripoti kuwakamata baadhi ya vijana kuwa walileta fujo siku ya uchaguzi. Kutokana na yaliyotokea, natoa wito kwa serikali kuwaachia huru vijana hao ili watu wapunguze maumivu
  19. H

    Ni ngumu kwa Afrika kuvitoa vyama tawala vikongwe kwa maandamano bali kwa mtutu wa bunduki

    Dawa ya moto ni moto ni ngumu kwa vyama tawala vikongwe Afrika kuondoka madarakani eti kwa maandamano na kelele za mitaani bali kwa mtutu wa bunduki na hujuma dhidi yao. Huwezi ukapambana na mafisadi wachache wenye nguvu na kumiliki jeshi kwa mawe wao wakiwa na bunduki mtakwisha! Ni bora sasa...
  20. H

    Nilishauri kuwa kabla ya maandamano ya NRNE muandamanie bima ya afya hamkunielewa!!

    Nilipotoa wazo hili watu walijibu kwa kejeli sana sasa leo mmeandamana kwaajili ya NRNE na mmekosa matibabu kwa haraka na kwa kiwategemea walewale waliowapiga risasi kuwatibu ambapo mngekuwa na bima labda mngeweza kutibiwa kwa haraka hata hospitali binafsi kwani watu wengi wamekufa kwa kukosa...
Back
Top Bottom