Vyama vya upinzani vyapigwa marufuku huko DRC

Vyama vya upinzani vyapigwa marufuku huko DRC

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,475
Reaction score
5,980
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imevipiga marufuku vyama 13 vya kisiasa, vikiwemo Chama cha PPRD cha rais wa zamani Joseph Kabila, katika hatua inayozidisha mvutano wa kisiasa nchini humo.
Uamuzi huo unafuatia kikao maalum cha Baraza Kuu la Ulinzi kilichoitishwa na Rais Félix Tshisekedi mjini Kinshasa, kikihusisha viongozi waandamizi wa serikali pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kujadili hali ya usalama nchini humo.
Kikao hicho kililenga kutathmini changamoto za kiusalama pamoja na operesheni za kijeshi zinazoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, wakati serikali ikiendelea kukabiliana na hali ya kutokuwa na utulivu, hususan katika maeneo ya mashariki mwa Kongo.
Kupigwa marufuku kwa vyama hivyo ni hatua ya karibuni katika mvutano unaozidi kuongezeka kati ya utawala wa Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila, ambaye amekuwa na tofauti za kisiasa na serikali ya sasa. Hali hiyo imeendelea kuibua maswali kuhusu nafasi ya upinzani na mustakabali wa demokrasia nchini humo.
Miongoni mwa vyama vilivyotajwa kupigwa marufuku ni Emergence Trail (TRAIL-E), Alliance for Alternation and Progress (AAP), Original African Democratic Union (UDA Orgi), Congolese People's Movement for the Republic (MPCR), Labour Alliance for Development (ATD), National Party for New Energy of Congo (PNEL), Lumumbist Progressive Movement (MLP), Union of Congolese Patriots (UPC), Action for the Dignity of Congo and its People (ADCP), Convention of Federalists for Christian Democracy (COFEDEC) na Alternative Actions for the Renaissance of Congo (AARC). Chama cha PPRD cha Kabila pia ni miongoni mwa vyama vilivyoathiriwa na uamuzi huo.
 
Back
Top Bottom