Vita ya 2 ya Congo(DRC)

Willy NGOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,431
Reaction score
5,978
VITA YA PILI YA KONGO, VITA MBAYA ZAIDI AFRIKA ILIYOBATIZWA JINA LA "VITA YA DUNIA YA AFRIKA"

Bomengo oyo ezali elakeli mabe “Utajiri huu ni laana.”.....

Kule Mbandaka kuna msemo maarufu wa Kilingala usemao, "Bomengo oyo ezali elakeli mabe yani “Utajiri huu ni laana.” msemo huu unaeleza namna utajiri wa Kongo DRC ulivyo na laana.

Msemo huu unahusiana na hali ambayo nchi ya Kongo DRC ina utajiri mkubwa wa madini na rasilimali, lakini wananchi wake wanaendelea kukabiliwa na umaskini, migogoro na ukosefu wa maendeleo.

Ndipo hapo wafaransa husema "malédiction des ressources au la malédiction des richesses".

Turudi Kwenye Hoja....

Vita ya Pili ya Kongo, inayojulikana pia kama Vita ya Dunia ya Afrika (Africa's World War), ilikuwa vita kubwa iliyopiganwa ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuanzia Agosti 1998 hadi 2003, vita hii ilihusisha mataifa kadhaa ya Afrika, majeshi ya serikali ya Kongo na makundi mbalimbali ya waasi.

Vita Ilianzaje....

Chanzo chake kinahusiana na matukio yaliyotokea baada ya Vita ya Kwanza ya Kongo ya 1996 mpaka 1997, mtakumbuka Kuwa Laurent-Désiré Kabila aliiondoa serikali ya Mobutu Sese Seko madarakani kwa msaada wa Rwanda, Uganda na makundi ya waasi.

Lakini ghafla uhusiano wa Kabila na washirika wake wa zamani ulizorota, Kabila alitaka majeshi ya kigeni yaondoke nchini Kongo, Rwanda na Uganda zilikuwa na wasiwasi kuhusu makundi yenye silaha yaliyokuwa yakitumia maeneo ya mashariki mwa Kongo kushambulia nchi zao.

Agosti 1998, uasi na mapigano mapya vilianza, vikapanuka hadi kuwa vita ya kikanda, ili kuelewa hili ni muhimu kuelewa mambo muhimu sana, nitakurudisha nyuma kuangazia mambo kadhaa kisha utaelewa kwa kina hiki tunacho kujadili leo.

Simulizi Inaanzia Hapa...

Katanga ni jimbo lililopo kusini mwa nchi ya DRC, na kiufupi tu ndio eneo lenye utajiri mkubwa sana wa madini DRC na liliwahi kuchangia 80% ya bajeti ya serikali ya DRC kila mwaka.

Katanga pekee Inazalisha madini kama dhahabu, almasi, shaba, fedha, cobalt, platinum, nickel n.k. Wakati vita ya tatu ya Kongo inaanza mwaka 1998, DRC ilikua inazalisha Almasi yenye thamani ya Tsh 1.2 Trillion kwa mwaka achilia mbali zilizokuwa zinatoroshwa kifisadi mipakani.

Katanga ina 34% ya hazina ya madini ya Cobalt duniani ambayo hutengenezea battery za simu & Laptop, Engine za ndege, mashine za kuchakata gesi n.k. pia 10% ya hazina ya shaba duniani ipo Katanga.

Kwa utajiri huu makampuni mengi ya madini yalikua pale Lubumbashi kusafirisha madini dunia nzima, kiufupi walipaita Katanga ni ''Kitovu cha madini ya DRC''.

Sasa baada ya kukupa picha kuhusu eneo la Katanga sasa turudi kwenye kiini hasa cha vita ya pili ya Kongo.

Sababu ya vita hii kuitwa ''Vita kuu ya dunia ya Africa'' ni kutokana na kuhusisha nchi 13 za Afrika kwenye mapigano Ndani ya Kongo-DRC ambapo upande mmoja walikuwepo Burundi, Uganda na Rwanda dhidi ya DRC.

Na upande wa DRC ilikuwa na nchi kama Sudan, Chad, Angola, Zimbabwe, Namibia, Libya, CAR, Ethiopia, Eritrea n.k

Tuanze Sasa....

Majeshi ya Rwanda na washirika wao yalipovamia DRC ili kumtoa Kabila waliyemuweka madarakani kupitia ile iliyoitwa "operation Banyamrenge" takribani mwaka 1997, Majeshi ya Rwanda na washirika wake yaliteka haraka majimbo yote ya mashariki na kaskazini kuanzia Kivu zote mbili, jimbo la Oriental na Jimbo la Manyema hivyo walikua wanaelekea kuteka Jimbo la Katanga ili kupata nguvu ya kiuchumi ya kuwawezesha kuendesha vita, ili kuparalyse nguvu ya Laurent Kabila, na kuwapa njia fupi zaidi ya kufika Kinshasa.

Kabla ya kufika Lubumbashi ambapo ni makao makuu ya Katanga, mapigano makali yalizuka kwenye mji muhimu wa Kindu uliopo jimbo la manyema ambapo ndio geti la kuelekea kusini mwa DRC palipo na jimbo la Katanga.

Baada ya mtanange mzito kwa siku kadhaa Majeshi ya washirika wa Rwanda yalifanikiwa kuuteka mji huo October 1998, hivyo safari rasmi ya kuteka Hazina ya Congo-DR ilikua imeanza rasmi.

Alliance Inajengwa...

Kufuatia hofu ya Hazina ama Roho ya DRC kuishia mikononi mwa Paul Kagame, ilibidi Zimbabwe na Angola ziingilie kwa kumsaidia Laurent Kabila na serikali yake dhidi ya majeshi ya waasi na washirika wao wa Rwanda.

Vita Ikawa ya Ndege Vita...

Mpaka vita inaisha Zimbabwe na Angola zilitoa wanajeshi zaidi ya elfu 50, Kwa kufahamu askari wa wavamizi walikua wababe kwenye vita za ardhini, Mbinu mpya ilisukwa ambapo Zimbabwe ilipeleka ndege vita za kutosha huku Angola ikipeleka Helicopter ili kuweza kupambana nao kutokea angani.

Hatimaye mbinu hii ilizaa matunda ambapo majeshi haya yaliweza zuia nguvu ya waasi kuiteka miji muhimu kama Mbujimayi na Lubumbashi.

Licha ya kwamba walikuja kuteka mji muhimu wa Pweto uliopo mashariki ya Katanga ila majeshi ya Zimbabwe yalisimama imara mpaka mwisho ambapo walisaini makubaliano ya amani.

Swali la kujiuliza hapa ni Kwanini Zimbabwe na washirika wake waliingia kumsaidia Kongo-DRC?

Jibu ya Hili Swali Lipo Hapa....

Zimbabwe Kupitia vyanzo mbalimbali inaeleza kuwa katika vita ya kwanza ya Kongo-DRC ile ya kumng'oa Mobutu, Zimbabwe ilikua inaidai DRC $400 Million (Tsh 1 Trillioni ya sasa) kama gharama za kusaidia vita.

Hivyo Robert Mugabe aliogopa serikali ya Kabila ikipinduliwa atakosa malipo yake hayo mazito.

Sababu ya Pili ni kwamba Zimbabwe iliahidiwa kupewa migodi mikubwa huko Kasai, pia waliingia ubia na kampuni ya mabeberu ya ORYX ili watoe utaalamu wa uchimbaji na masoko, then wagawane faida Pasu kwa pasu.

Kampuni Mama ya OSLEG ikaanzishwa, Ukumbuke mkataba ulikua wa miaka 25 wa kuchimba kwenye migodi miwili mikubwa zaidi ya Almasi huko Katanga na kasai.

Hivyo Zimbabwe iliweza kufaidika zaidi na vita hii kiuchumi kuliko hata wavamizi wa kutoka Afrika mashariki.

Hivyo Zimbabwe kuingia kwenye hii operation ilikuwa ni kuokoa masrahi mapana ya taifa lake.

Naposemaga masrahi mapana namanisha mpango mkakati wa kiuchumi na kisiasa, katika hii "hii vita ya Africa ndani ya Kongo" masrahi ya Zimbabwe ni Kongo-DRC, yani Kongo ilikuwa eneo la kimkakati.

Kwaiyo Zimbabwe iliingia kutetea masrahi yake sio kutoa msaada wa kindugu kama ilivyo fahamika kwa wengi.

Angola Nayo...

Angola nayo iliingia kwenye Vita hii ya Pili ya Kongo kwasababu zile zile kama za Zimbabwe, isipokuwa tofauti na zile za Zimbabwe Angola ilikuwa na sababu za ziada.

Angola iliingia Vitani kwasababu mbili ambazo ni kama ifuatavyo.

Sababu ya kwanza ya kuingia kwenye Vita...

Kwanza ni hofu ya Angola dhidi ya Kagame kushirikiana na UNITA ya Savimbi kuivamia Angola.

Ikumbukwe kwenye ile iliyoitwa "Operation Kitona" nilieleza jinsi Savimbi alivyoshiriki kusaidia majeshi ya Kagame kutoroka Angola kwa kuwapa ground cover kuingia nchini humo, hivyo kama Jimbo la Katanga lingeangukia mikononi mwa waasi basi Savimbi naye angepewa migodi na ukizingatia Jimbo hilo linapakana na Angola basi usalama wa nchi hiyo ungekuwa shakani.

Ndio maana mpaka sasa nchi ya Angola ina ushawishi mkubwa kwenye migogoro ya Kongo-DRC na Rwanda, mara kadhaa inahofia usalama wa Angola kwa waasi kuangukia kwenye mikono isiyo salama.

Sababu ya pili...

Kama wenzao wa Zimbabwe, nao walipewa migodi kadhaa huko Tshipaka ya kuchimba Almasi na dhahabu.

Achilia mbali walipewa kitalu Huko pwani ya DRC (eneo la Kabinda) kutafiti mafuta kwa sharti watagawana faida, Kiufupi wanadiplomasia na majenerali wa Angola waligeuka wafanyabiashara wa kuuza madini ulimwenguni.

Na ziliendesha mpaka bajeti za wizara za ulinzi kwa malipo ya kuilinda Katanga isiangukie mikononi mwa Kagame, Hivyo wao Katanga ilikuwa muhimu mno kimkakati, ilitakiwa ilindwe kwa nguvu zote.

Nchi hizi mbili za Zimbabwe na Angola waliweka pesa nyingi sana na nguvu kubwa mpaka vita inaisha kwa madhumuni ya kuvuna madini ya DRC.

Nchi zote zinazoizunguka DRC zinanufaika na raslimali za DRC kwa mgongo wa waasi hasa hasa mashariki mwa Congo-DR Rwanda na Uganda kuna wakati zinapigana zenyewe kwa zenyewe ndani ya nchi ya DRC ili ziwe na udhibiti wa raslimali zinazopatikana.

Mpaka asubuhi ya tarehe 27 November 1998 Majeshi ya Rwanda na Uganda yalikuwa yamechapika vibaya mno, yakarudi nyuma mpaka Kindu jimbo la Manyema.

Herkopta za Angola zikaanzisha mashambulizi huko Kindu na majimbo ya Kivu zote mbili, Rwanda kuona hivyo wakasalimu amri na kukubali mapatano, vita ikaisha, ila Kagame hakukubali akaanzisha mpango mkakati mpya wa kumuua Laurent Kabila.

Kuna taarifa zinaeleza kuwa kifo cha Laurent Kabila ni mpango wa Paul Kagame, ntaeleza hili siku nyingine.

Pia makundi yote ya Watutsi kule mashariki ya Kongo DRC yana mkono wa Kagame, hili nimeeleza kwa kina kwenye ile Makala yangu ya "Kiini na chimbuko la migogoro mashariki mwa Kongo DRC "
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…