Kottler Masoko
Senior Member
- May 28, 2010
- 193
- 28
KISIWA CHA MAFIA: NAMBA SITA DUNIANI, NAMBA MBILI AFRIKA.
Na Juma Salum
Licha ya kasoro zao ambazo kila jamii ina za kwake, kuna jambo moja zuri binafsi nalipenda kuhusu ndugu zetu wachaga toka mkoa wa Kilimanjaro, sio kiwango cha utajiri wao, si idadi kubwa ya shule, sio kina Manka wala si kuwahi kuijua pesa kuliko jamii nyingi za Kitanzania bali napenda namna wanavyoutumia mlima Kilimanjaro kujinufaisha wao kama watu ambao mlima upo kwao na kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa hususani mapato yatokanayo na utalii wa mlima Kilimanjaro.
Leo sisemi kuhusu hifadhi ya bahari Mafia inayotajwa kama hifadhi ya bahari kubwa zaidi Afrika ya mashariki ikiwa na upekee wa matumbawe, aina nyingi za samaki, nguva, kasa, mandhari na mengine mengi yasiyopatikana popote duniani lakini ukiambiwa mchango wake kimapato kwa watu wa Mafia au hata kwa taifa utaishia kusonya ama kutukana kwakua ni kitu ambacho wazungu wanasema ni 'NEGLIGIBLE' na hakiingii akilini hata kiduchu.
Tuyaache hayo bwasomo maana hifadhi hatujaianzisha mie na weye, huenda hayatuhusu!
Eneo la bahari magharibi ya kisiwa cha Mafia, kati ya rasi kisimani na rasi mbizi anapatikana samaki mkubwa zaidi duniani aitwae PAPA POTWE ama whale shark kwa kimombo. Yes namaanisha mkubwa kuliko samaki yeyote yule inaemjua duniani, tuheshimiane usinitajie NYANGUMI. Nyangumi ndio kiumbe mkubwa baharini na nchi kavu lakini kisayansi Nyangumi sio samaki bali ni malaria ohh nisamehe bwana namaanisha MAMMALIA.
Papa Potwe wanapatikana katika nchi tano Afrika miongoni mwao ni Msumbiji, Djibouti, Madagascar, na kisiwa cha Mafia Tanzania.
Papa potwe huweza kufika ukubwa wa zaidi ya mita 12 na uzito unaopita tani 20. Samaki huyu ni kivutio kwa watalii kutokana na tabia ya potwe kuogelea ya karibu na uso wa bahari alapo pia hulka yake ya upole inayoruhusu kuogelea nae kwa karibu sana (japo hairuhusiwi kumgusa) bila kumdhuru binaadamu.
Kwa mujibu utafiti wa WWF 2012/13, Kisiwa cha Mafia kina Potwe 87. Wakati 97% wakiwa ni vijana walio kati ya utoto na utu uzima yaani juveniles, 83% ni vidume. Utafiti huu pamoja na utafiti nyingine hazijabainisha Potwe wazee na majike wanakua wapi hasa.
Kuanzia mwezi wa kumi mpaka mwezi wa tatu huwa ndio msimu wa Potwe kuonekana katika kisiwa cha Mafia na mamia kama sio maelfu ya watalii kutoka pande mbalimbali za dunia humiminika Kilindoni Mafia kuwaona na kuogelea nao Potwe wetu.
Kulingana na taarifa katika mtandao wa Padi Travel (October, 2016). Kilindoni Mafia ni ya sita (6) katika maeneo kumi bora ya kuona Potwe duniani na ya pili (2) Afrika baada ya Tofo beach, Mozambique. Taarifa imezingatia urahisi wa kuwaona na kufikika tokea ufukweni.
Mawakala wa utalii na waongoza watalii humtoza mtalii mmoja kwenda kuwaona papa Potwe kati ya shilingi 130,000 mpaka 220,000 kwa safari moja.
Gharama hizi zinakaribiana na gharama ya kuingia kupanda mlima Kilimanjaro kwa siku ambayo ni 145,000 kwa mtalii mmoja toka nje ya Tanzania.
Kama viongozi wetu, hasa viongozi wetu wapendwa na wawakilishi wa watu wa Mafia katika ngazi zote za utawala wakiacha kufanya kazi yao ya kuongoza na kuwakilisha watu wa Mafia na maslahi yao, ni dhahiri utalii wa Potwe utakuja kua kama utalii usiwanufaisha watu wa Mafia wala serikali. Utakua mradi wa wachache wajanja wajanja waoweza kuwafikia wafadhili na kutegesha mirija ya kuchuma fedha kupitia miradi ya KIPUMBAVU kwa niaba ya watu wa Mafia na Potwe wao. Watu wa Mafia hawatakua kama Wachaga na mlima Kilimanjaro Kamwe!!!!!
.....................................................................
Haya yalikua sehemu ya mazungumzo yangu na bwana Mwichande Faki Kirobo tulipokutana kwenye Khitma ya mama yake mkulu Bi Mkunga Vikomba, Juani.
Copy & Paste.