Unaijua diwani ya amani?

Unaijua diwani ya amani?

dawambili

Member
Joined
Nov 28, 2024
Posts
34
Reaction score
20
Miongoni mwa vitu ambavyo unapaswa kufahamu kuhusu Diwani ya Amani ni kwamba hiki ndio kitabu pekee kilichochanganya aina zote za washairi wa zama hii waliohai.

Humu ndani kuna wale washairi wakongwe wa A-list kutoka nchini Kenya kama Mzee Thomas Koskei, Mzee Mohamed Khamis wa Takaungu, Mzee Ludovick Mbogholi na Mahmoud Sharifu almaarufu Swahibul Iman, lakini pia kuna washairi mahiri damu changa wanaofanya vizuri na kuvuma sana kwa sasa kwenye ushairi wa Kiswahili nchini Kenya kama Swalehe Hussein (Mzora), Valentine Omondi, Halili Malenga, James Obiero ,Mwalimu Oyugi Stephen, Moses Chesire na Kezia Macharia.

Kabla sijawataja baadhi ya wakongwe na washairi chipukizi wa Tanzania bara na visiwani ambao kwamba wino wao umehusika kikamilifu katika kutengeza Diwani hii ya kihistoria hebu tazama shairi hili namba 58 la gwiji wa Ushairi wa kiswahili Tanzania ambaye kwa hakika yeye ndiye miongoni mwa kile kizazi cha kale kilichobahatika kupata barka ya umri hata siye vijana wa kisasa kuweza kumuona na kunufaika naye, huyu ndiye yule gwiji aliyetunga shairi maarufu la Mvaa koti si lake na mashairi mengine mengi yaliyovuma miaka ya themanini wakati wa kizazi cha dhahabu cha Ushairi wa kiswahili nchini Tanzania.

Huyu mwamba ni Rakhisi Filisi anayetambulika pia kama Nassor Mohammed ama Mzee wa Khairati kutoka Uvumba Kibada, na shairi lake laitwa "Kwanza Tuchunge Amani"


SHAIRI Namba 58
KWANZA TUCHUNGE AMANI

Kama huchungi amani, japo unadai haki,
Kwa fujo na tafarani, kwako amani hutaki,
Iwe fujo mitaani, ndio njia ilobaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Amani haki huzaa, mtakapo hamtaki,
Hili mkilikataa, hali mbaya tutabaki,
Haki kama mshumaa, kwenye fujo hauwaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Amani kwetu muhimu, tuache ubaramaki,
Amani inaghalimu, ikienda haibaki,
Hukaribisha mabomu, likirushwa hulidaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Haki kwenye mtihani, zinaporushwa fataki,
Ataijadili nani, watu wa kwenye handaki,
Amani ina thamani, wote tuombe ibaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Amani natuitunze, kama kinywa na mswaki,
Wasojua wajifunze, nakumuomba Razaki,
Na nchi tusiiponze, sisi watu si samaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.



Baada ya hapo tusonge mbele kwa kuangalia shairi la Mwalimu wa Sanaa aliyewahi kufundisha chuo cha Sanaa Bagamoyo gwiji wa Ushairi Mzee Mustafa Merere liitwalo Ibilisi wa Imani.

SHAIRI Namba 59
IBILISI WA IMANI
Akili tuliza moyo, woga wangu ni Manani,
Tabia mbaya uchoyo, kizazi cha mumiani,
Watu leo koyokoyo, hawakumbuki hisani.
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Vurumai ya amana, utu hauna thamani,
Chuki mzazi na mwana, japo yumo mwanandani,
Njozi naota laana, gharika lenye tufani,
Mali nguvu la shetani, ibilisi wa imani.

Imepotea huruma, mja nusu punguani,
Mgonjwa hana huduma, roho kaweka rehani,
Utiriri wa dhuluma, umeshika usukani,
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Upweke ni ukafiri, undugu una nishani,
Dini haina kadiri, utashi wa upagani,
Njia panda ya fakiri, mkabala wa jirani,
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Hatima mchuma janga, mwiko kula na mtani,
Mchamungu au mwanga, lishe dua na ubani,
Kirago chako mchanga, joho vazi la kafani.
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Kwa mwenye kupenda na kuujua Ushairi ataelewa ukubwa wa mtifuano wa hoja, ulumbi na ujagina uliomo kwenye kitabu, kupitia mashairi haya mawili yaliyopakana kwenye mpangilio wa kurasa za kitabu cha Diwani ya Amani.

Ajabu ilioje kitabu kama hiki kuwa ni bure kabisa sababu pekee ikiwa ni mapenzi na uzalendo uliomo kwenye vifua vya washairi hawa 63 wa Afrika Mashariki waliojitoa kukamilisha kazi hii.


Tukipata wasaa katika makala ijayo tutawataja wakongwe wakubwa migogo ya ushairi na vijana mahiri malenga wasifika kutoka Tanzania bara na visiwani walioshiriki katika Diwani hii.

Kwa mawasiliano, maoni na ushauri wasiliana na
+255689969098.
 

Attachments

  • IMG-20261016-WA0112(2).jpg
    IMG-20261016-WA0112(2).jpg
    465.7 KB · Views: 15
Katika makala iliyopita tuliangazia majina makubwa ya washairi kutoka Kenya ambao wameshiriki katika Diwani ya Amani, tukatazama na mashairi mawili ya washairi nguli kutoka nchini Tanzania mashairi ambayo kwa hakika ni kielelezo tosha cha ubora na ukubwa wa Diwani ya Amani.

Kabla ya kuendelea mbele kwanza niwashukuru wale wote ambao kwamba mmewasilisha maoni pongezi na mitazamo yenu kuhusu Diwani ya Amani.

Sikutarajia mapokezi yangekuwa makubwa kwa kiwango hiki cha sasa, nimeshuhudia mapenzi makubwa ya fasihi andishi kutoka kwa wadau wengi kutokea nchini Kenya, jambo linalotia moyo na kuchagiza ari ya kuendelea kusonga mbele katika mradi huu wa kujitolea utakao weka historia katika tasnia ya fasihi andishi Afrika Mashariki.

Mmoja kati ya watu aliyetoa maoni alioneshwa kushangazwa na aina ya uandishi wa magwiji wale wawili yeye alifananisha uandishi wao kama munyu na sukari.Upande mmoja kukiwa na mwandishi mwenye lugha laini ya mnato, nyepesi yenye utoshelezi na muwala wa hali ya juu upande wa pili kukiwa na nguli wa utunzi wa tashbihi, falsafa, ufinyazi wa maneno wa hali ya juu na naahau.

Habari za magwiji hawa ni kubwa na nyingi tutosheke tu kwamba wao ni waalimu wa washairi wengi yaani katika kila washairi kumi wa Tanzania bara basi hakukosi washairi watano ambao watakuwa wamepita kwao au wamepita kwa wanafunzi wao au wamepita kwa wanafunzi wa wanafunzi wao.
Ushiriki wao katika Diwani ya Amani ni uthibitisho wa kwamba Kupitia kitabu hiki fasihi imefika kwenye kilele chake.

Kila ninapotaka kutaja majina ya washairi nguli wa Tanzania bara na visiwani walioshiriki katika Diwani hii na kuangazia kwa uchache ukubwa wa kazi waliyofanya napata tabu sijui nimtaje nani na nani nimuache hebu vuta taswira hata ingekuwa wewe ndiye Mimi ungafanyaje pindi unapotakiwa kutaja watu wachache kwenye orodha ndefu iliyosheheni wakongwe wengi kama wakina Hamis Kissamvu Mkanyaji, Suleiman Kissamvu (Mzee wa Changamoto), Dk.Mwanahija (Malenga wa Ndijani), Mzee Shaibu Hundi, Mzee Jamal Ponera(Kikorombo), Amiri Amri Abeid Kaluta, Maimuna Hashim, Bi Sikudhani Jalala, Hamad Alli Kombo (Dk.Mshiko), Mzee Hassan Msati(Hubatine almaarufu Chamtungi Hakilawa), Francis Kaswahili na Idd Mwimbe na wengineo.

Ni dhahiri kwamba kwenye kazi hii Kuna kazi ngumu sana ambayo mtu yeyote mwenye kuujua Ushairi atapata tabu kama niipatayo Mimi.
Hapo bado kuna kundi la Malenga vijana na wale vinara wa nyakati ambao nikisema niwataje itanibidi nitajie orodha yote iliyobakia ya washairi walioshiriki.

Ili unielewe vizuri ninachomaanisha nitakuleta mashairi mawili ya washairi ambao sijawataja hapo Ili uelewe ukubwa wa hao niliowataja yaani ambao sijawataja kama wamefanya kazi hiyo utakayoina vipi kwa wale wakongwe niliowataja unajua watakuwa wamefanya nini?

Shairi la kwanza ni la Mbaruku Alliy Mohamed (Jasho Tamu) kijana mahiri kutokea kule Moa Tanga Tanzania aliyewahi kushika nafasi ya kumi katika Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi bunifu kwa kitabu chake cha Utenzi wa Nana Mkombozi.
Shairi lake linaitwa Amani Usitoweke

SHAIRI namba 37
AMANI USITOWEKE
Niliulizwa ni nini, njiani nilipopita,
Ndipo nashika sukani, niseme bila kusita,
Niliyofunzwa nyumbani, tungoni ninayaleta,
Maana yake amani, ni kukosekana vita.

Jamii huwa mwanana, mambo yenda kwa muwala,
Watu hufurahiana, hakiwi ghali chakula,
Ndiposa tuombe sana, iwepo kila mahala,
Vita ikiwa hakuna, kheri nyingi hutawala.

Jamii huwa salama, nyoyo za watu hutua,
Wenda shamba wakulima, wavuvi wenda kuvua,
Afiya huwa ni njema, vifo navyo hupungua,
Amani ikituama, uchumi nao wakua.

Vivile ikiandama, waja huzifanya kazi,
Na wanafunzi husoma, elimu kwa zote ngazi,
Hakuna mtu kuhama, kuyakimbia makazi,
Amani ikisimama, hatokei mkimbizi.

Amani kitu muhimu, hakuna anayepinga,
Sote inatulazimu, kutoyafunga maninga,
Ndiposa kwetu idumu, wala isijejitenga,
Ikiwa nasi dawamu, hatutopata majanga.

Mwisho amani mwendani, nchini ulojikita,
Upo mwetu akilini, kama sita mara sita,
Kisha tunayo yakini, ukenenda tutajuta,
Usitoweke amani, hapa naweka nukta.

Shairi la pili nitakalolieta ni la kwangu Mimi mwenyewe Daruweshi Mkuluwanyika mwandishi wa makala hii na Mratibu Mkuu wa mradi huu wa Diwani ya Amani, mwanzilishi wa Tuzo ya Ushairi Chaguo la Wasomaji Afrika Mashariki (Tuchawa), Mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi bunifu mwaka 2025 na mshairi Bora wa Mwaka 2026 Kupitia Tuzo ya Mashairi Festival.
Kama ilivyo ada yangu kupita katika bahari ngumu na kubadilikabadlika katika uandishi, hali hizo zote zinaonekana wazi kwenye shairi hili nitakalolileta.
Shairi hili pia linaakisi namna mtifuano wa hoja kati ya haki na amani ulivyochukua nafasi kubwa katika kitabu hiki cha Diwani ya Amani.


SHAIRI namba 24
KWELI NA GHALATI

Ai kweli na ghalati, pale vikifungamana,
Unapotea umati, pasiwepo muamana,
Kupata huwa bahati, na umahiri fitina
Ai haki na batili, vinapotumikiana.

Ai batili na haki, pale vikibabatana,
Izaliwayo nifaki, na waja kutumiana,
Launyofu halibaki, palipomea hiyana
Ai wema na uovu, pale vinapochuana.

Ai uovu na wema, ja wembamba na upana,
Alo mahiri hupima, pimo linotakikana,
Inapofika hatima, hiyari hupatikana,
Ai kiza na mwangaza, daima hufarakana.

Ai mwangaza na kiza, ja upara na kitana,
Kimoya kikatokeza, nakingine huagana,
Lau ije miujiza, sirahisi kufatana,
Ai ghalati na kweli, sawa ndio na hapana.

Baada ya kutazama mashairi haya mawili kwa jicho la kisomi ni lazima utajiuliza swali, ikiwa vijana wamefanya kazi kubwa kama hii vipi hao wakongwe?


Tutaendelea kuwaletea dondoo za yaliyomo katika Diwani ya Amani Kila tutakapopata nafasi..



Kwa maoni na ushauri kuhusu Diwani ya Amani wasiliana nasi kupitia +255689969098
 

Attachments

  • IMG-20261031-WA0000.jpg
    IMG-20261031-WA0000.jpg
    232.3 KB · Views: 14
Miongoni mwa vitu ambavyo unapaswa kufahamu kuhusu Diwani ya Amani ni kwamba hiki ndio kitabu pekee kilichochanganya aina zote za washairi wa zama hii waliohai.

Humu ndani kuna wale washairi wakongwe wa A-list kutoka nchini Kenya kama Mzee Thomas Koskei, Mzee Mohamed Khamis wa Takaungu, Mzee Ludovick Mbogholi na Mahmoud Sharifu almaarufu Swahibul Iman, lakini pia kuna washairi mahiri damu changa wanaofanya vizuri na kuvuma sana kwa sasa kwenye ushairi wa Kiswahili nchini Kenya kama Swalehe Hussein (Mzora), Valentine Omondi, Halili Malenga, James Obiero ,Mwalimu Oyugi Stephen, Moses Chesire na Kezia Macharia.

Kabla sijawataja baadhi ya wakongwe na washairi chipukizi wa Tanzania bara na visiwani ambao kwamba wino wao umehusika kikamilifu katika kutengeza Diwani hii ya kihistoria hebu tazama shairi hili namba 58 la gwiji wa Ushairi wa kiswahili Tanzania ambaye kwa hakika yeye ndiye miongoni mwa kile kizazi cha kale kilichobahatika kupata barka ya umri hata siye vijana wa kisasa kuweza kumuona na kunufaika naye, huyu ndiye yule gwiji aliyetunga shairi maarufu la Mvaa koti si lake na mashairi mengine mengi yaliyovuma miaka ya themanini wakati wa kizazi cha dhahabu cha Ushairi wa kiswahili nchini Tanzania.

Huyu mwamba ni Rakhisi Filisi anayetambulika pia kama Nassor Mohammed ama Mzee wa Khairati kutoka Uvumba Kibada, na shairi lake laitwa "Kwanza Tuchunge Amani"


SHAIRI Namba 58
KWANZA TUCHUNGE AMANI

Kama huchungi amani, japo unadai haki,
Kwa fujo na tafarani, kwako amani hutaki,
Iwe fujo mitaani, ndio njia ilobaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Amani haki huzaa, mtakapo hamtaki,
Hili mkilikataa, hali mbaya tutabaki,
Haki kama mshumaa, kwenye fujo hauwaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Amani kwetu muhimu, tuache ubaramaki,
Amani inaghalimu, ikienda haibaki,
Hukaribisha mabomu, likirushwa hulidaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Haki kwenye mtihani, zinaporushwa fataki,
Ataijadili nani, watu wa kwenye handaki,
Amani ina thamani, wote tuombe ibaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.

Amani natuitunze, kama kinywa na mswaki,
Wasojua wajifunze, nakumuomba Razaki,
Na nchi tusiiponze, sisi watu si samaki,
Amani huzaa haki, kwanza tuombe amani.



Baada ya hapo tusonge mbele kwa kuangalia shairi la Mwalimu wa Sanaa aliyewahi kufundisha chuo cha Sanaa Bagamoyo gwiji wa Ushairi Mzee Mustafa Merere liitwalo Ibilisi wa Imani.

SHAIRI Namba 59
IBILISI WA IMANI
Akili tuliza moyo, woga wangu ni Manani,
Tabia mbaya uchoyo, kizazi cha mumiani,
Watu leo koyokoyo, hawakumbuki hisani.
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Vurumai ya amana, utu hauna thamani,
Chuki mzazi na mwana, japo yumo mwanandani,
Njozi naota laana, gharika lenye tufani,
Mali nguvu la shetani, ibilisi wa imani.

Imepotea huruma, mja nusu punguani,
Mgonjwa hana huduma, roho kaweka rehani,
Utiriri wa dhuluma, umeshika usukani,
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Upweke ni ukafiri, undugu una nishani,
Dini haina kadiri, utashi wa upagani,
Njia panda ya fakiri, mkabala wa jirani,
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Hatima mchuma janga, mwiko kula na mtani,
Mchamungu au mwanga, lishe dua na ubani,
Kirago chako mchanga, joho vazi la kafani.
Mali nguvu ya shetani, ibilisi wa imani.

Kwa mwenye kupenda na kuujua Ushairi ataelewa ukubwa wa mtifuano wa hoja, ulumbi na ujagina uliomo kwenye kitabu, kupitia mashairi haya mawili yaliyopakana kwenye mpangilio wa kurasa za kitabu cha Diwani ya Amani.

Ajabu ilioje kitabu kama hiki kuwa ni bure kabisa sababu pekee ikiwa ni mapenzi na uzalendo uliomo kwenye vifua vya washairi hawa 63 wa Afrika Mashariki waliojitoa kukamilisha kazi hii.


Tukipata wasaa katika makala ijayo tutawataja wakongwe wakubwa migogo ya ushairi na vijana mahiri malenga wasifika kutoka Tanzania bara na visiwani walioshiriki katika Diwani hii.

Kwa mawasiliano, maoni na ushauri wasiliana na
+255689969098.
Malenga wa kichawa wanaotumiwa na wauaji kuhubiri amani na sio haki.

Tunataka haki itendeke, serikali haiwezi kujichunguza yenyewe
 
Malenga wa kichawa wanaotumiwa na wauaji kuhubiri amani na sio haki.

Tunataka haki itendeke, serikali haiwezi kujichunguza yenyewe
Kwanza ungesoma kitabu Kisha ndio ulete hoja hiyo.
Ndani ya kitabu haki imezungumziwa kwa upana wake na Viongozi wa kisisasa wamekosolewa kwa upana wake.
Ni ajabu mtu mwenye akili timamh kuchukia neno amani linapotajwa.
 
CHAI YA ASUBUHI.
JE, UNAIJUA DIWANI YA AMANI?

Na Mkuluwanyika.

Laiti kama Diwani ya Amani ingeandikwa kwa maandishi ya nathari, ingehitajika vitabu zaidi ya mia mbili ili kutosha kubeba maudhui yaliyomo, lakini jambo linalotofautisha ushairi na aina nyingine za maandishi ni kwamba ushairi huchukua maneno, fikra, na mitazamo mipana kisha kuifinya katika maneno machache yenye vina na mizani.

Uandishi wa mashairi ya ushairi aghalabu huwa ni tofauti na mashairi ya nyimbo, kwani mashairi ya nyimbo huhitajia maneno mepesi na machache tu yenye kuelezea kitu au jambo alilolikusudia mtunzi. Lakini mashairi ya ushairi huwa yanabeba mambo mengi ndani yake, ikiwemo majazanda, umbuji wa lugha, balagha, nahau, udamisi, falsafa, bila kusahau vina na mizani kulingana na bahari husika.

Niliwahi kusema pahala fulani, endapo vitabu vya dini vitaondolewa vyote duniani, basi vitabu pekee vitakavyobaki kuleta ustawi wa fikra, tabia, na uongofu kwenye jamii ni vitabu vya ushairi.
Ama kwa hakika, jambo hilo ndilo limefanya ushairi kuwa maandishi yanayopendwa na watu wenye hekima na upeo mkubwa wa kufikiri, mtu pite asiyeweza kushughulisha ubongo wake daima huwa hapatani na Ushairi.

Kwa hivyo, ushairi si sanaa ya kuunganisha maneno pekee ili kupata vina, bali ni sanaa ya watu wenye fikra pana, maono, na hekima ya hali ya juu. Na hilo linadhihirika kupitia washairi wenyewe; ndipo ikawa wengi miongoni mwa washairi ni wasomi wa dini, watu wenye adabu, busara, na hekima, na watu wenye misuli katika ulimwengu wa kiroho, tazama mifano halisi kwa watu kama vile Ibn Arabi [mwanafalsafa na mshairi mkuu wa Kisufi kutoka Andalusia], Shaaban Robert [ baba wa fasihi ya Kiswahili, mfalme wa hekima na mwanafalsafa wa lugha kutokea hapa kwetu nchini Tanzania], Jalalal Din Rumi [ Mfalme wa hekima wa Persia], Al-Mutanabbi [mshairi mkubwa wa historia ya Kiarabu], William Shakespeare [Baba wa fasihi ya Kiingereza na mshairi nguli aliyetumia kazi za kishairi kubadili fasihi ya dunia]) na wengine wengi miongoni mwa washairi wakubwa waliowahi kuwepo na waliopo duniani ambao kwamba kama ingenilazimu kuwataja wote basi ingenichukua miaka na mikaka kumaliza orodha hiyo.

Baada ya mukadima mrefu, sasa turejee katika Diwani ya Amani. Katika makala iliyopita tuliangazia majina ya washairi wakubwa kutoka Tanzania Bara na Visiwani, na nikasema ni ngumu kwangu kuelezea baadhi na kuwaacha wengine, lakini nikatoa mfano wa washairi damu changa waliyoonesha umahiri wao. Nikasema, kama wao wamefanya kazi bora kwa kiwango kikubwa namna ile, je, wakongwe watakuwa wamefanya nini?

Leo nataka nikujuze jambo ambalo najua ya kuwa hulijui. Miongoni mwa mambo yanayoipa hadhi Diwani ya Amani ni utajiri wa bahari, ndanimwe kuna mitindo mingi sana ya ushairi wa Kiswahili. Kama nilivyotangulia kusema, ushairi ni sanaa inayohitaji ufundi na si kuunganisha tu maneno. Kwa kuwa malenga walioshiriki Diwani ya Amani ni mafundi, basi bila shaka wameonesha ufundi wao na namna wanavyoweza kuogelea bahari tofauti-tofauti.

Hebu vuta taswira namna unavyoburidika ukishika kitabu cha mshairi mmoja chenye bahari moja tu ya tarbiya, kisha waza burudani itakayopatikana utakaposhika kitabu cha washairi sitini na watatu chenye bahari nyingi zaidi.

Ili unielewe ninachomaanisha tutazame shairi la tathlitha la Mzee Ludovick Walele Mbogholi (Ngariba Mlumbi) kutokea nchini Kenya:

SHAIRI NAMBA 03: AMANI NA UTULIVU

Amani mwenzie haki, chambilecho waerevu,
Na pindi isipobaki, ni vidonda na makovu,
Shuti hayo tuafiki, pasizuke upotevu.

Popote palipo haki, ni mahali patulivu,
Hapana mikikikiki, ngondo na upeketevu,
Huwa kunatamalaki, amani na utulivu.

Si mabomu na bunduki, huleta unyenyekevu,
Watu wapatapo haki, na uongozi sikivu,
Hawaleti taharuki, za kedi na ushupavu.

Penye haki hata chuki, huwa inakosa nguvu,
Hutoweka uzandiki, na tawala za mabavu,
Moliwa hupabariki, pasiwe na maonevu.

Baada ya kutazama shairi hilo, tutazame shairi la Malenga wa Mrima kutokea Mkwaja, Pangani, Tanga. Huyu ndiye mwanamke aliyembeba mwandishi wa makala hii na Mratibu Mkuu wa Diwani ya Amani miezi tisa tumboni; yeye ushairi ameurithi toka kwa baba yake Mzazi, Mheshimiwa Akilimali Ramadhan Kayumbo.
Malenga huyu ni Mswahili wa asili na ni miongoni mwa kile kizazi cha wasanii wakongwe wa sanaa za maigizo nchini Tanzania kilichofungamanishwa na maadili.

Shairi lake hili liitwalo "Pasipo Amani" alilotumia bahari ya kikai pia linatuonesha mtifuano wa hoja tulioutaja tangu awali, kwamba kinyume na baadhi ya watu wazaniavyo, Diwani ya Amani si kitabu cha uchawa chenye kusifu watu au kundi fulani la kisiasa (ingekuwa ajabu washairi wasomi wenye maarifa mengi, busara, na hekima wawe machawa wa kusifu-sifu tu watu).

Ukweli ni kwamba Diwani ya Amani ni kitabu kinachoeleza kwa upana umuhimu wa amani, wajibu wa kila mtu katika kulinda amani, viashiria na visababishi vya uvunjifu wa amani, madhara ya uvunjifu wa amani, na namna ya kukabiliana na uvunjifu wa amani.

Hivyo, mtifuano tunaouzungumzia humu ni kupingana kwa mitazamo, maoni, na hoja, lakini lengo halisi likiwa ni moja tu: ni namna gani tunu yetu ya amani itabakia nchini.

Mfano halisi ni kama tulivyoona katika shairi la awali, yeye Mzee Mbogholi kutoka Kenya anaamini haki ndiyo inaleta amani, lakini upande wa pili tutaona shairi la Bi. Mwanafaki A.R. Kayumbo (Anti May) akiuliza, pasipo amani hiyo haki atatupa nani?

SHAIRI NAMBA 2: PASIPO AMANI
Amani na haki, sawa honi na sukani,
Hasama na chuki, faraka ya ikhiwani,
Utengano dhiki, waungwana huulani,
Pasipo amani, haki atatupa nani?

Upendo ni tunu, tulojaliwa nchini,
Fitina ni mbinu, wafanyazo wahaini,
Huleta sununu, ije tabu na huzuni,
Pasipo amani, haki atatupa nani?

Uzalendo vazi, asolivaa kaini,
Walo mabazazi, kukicha waturubuni,
Pa utandawazi, tukalitupe jaani,
Pasipo amani, haki atatupa nani?

Umoja ni nguvu, ya ushindi duniani,
Hila na mabavu, si sumaku ya amani,
Subira werevu, ndivyo vitatuauni,
Pasipo amani, haki atatupa nani?

Tamati dunia, huwa sawa machungani,
Vita ni hatia, kwa wale wenye imani,
Tukivikimbia, tutakuwa salamani,
Pasipo amani, haki atatupa nani?

Kwa leo nikomee hapa, tukutane wiki ijayo panapo majaaliwa ya Rabuka, ambapo tutakuwa na ziara ya kusambaza nakala za kitabu cha Diwani ya Amani kwa wadau, jamii, na taasisi
Kwanza ungesoma kitabu Kisha ndio ulete hoja hiyo.
Ndani ya kitabu haki imezungumziwa kwa upana wake na Viongozi wa kisisasa wamekosolewa kwa upana wake.
Ni ajabu mtu mwenye akili timamh kuchukia neno amani linapotajwa.

za serikali.

Kwa maoni na ushauri, wasiliana nasi kupitia: +255689969098
 
Back
Top Bottom