HOJA TRA Audits zimegeuka KERO

HOJA TRA Audits zimegeuka KERO

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

saudiasahara

New Member
Joined
Nov 8, 2026
Posts
1
Reaction score
3
Makundi tofauti ya ukaguzi wa TRA yamekuwa kero kwa wateja. Kila baada ya muda mfupi linafika kundi jipya, kila moja likisema linatoka kitengo tofauti. Haiwezekani kazi ya mteja iwe kuhudhuria vikao na maafisa wa TRA na kuwasilisha nyaraka zilezile kila mara, badala ya kuendesha biashara.

TRA iratibu vitengo vyake ili ukaguzi ufanyike kwa pamoja na kuhusisha maeneo yote yanayohusika, pale inapowezekana. Tofauti za vitengo hazipaswi kuwa mzigo kwa mteja.

Kinachokera zaidi ni baadhi ya maafisa kufika bila kusoma taarifa za ukaguzi uliotangulia, kurudia maswali yaliyokwisha kujibiwa na kuonekana kutokuwa na maandalizi ya kutosha.

Wengine, kwa kauli na mwenendo wao, wanaacha hisia kwamba tayari wanawachukulia wamiliki wa kampuni kuwa wezi kabla hata ya kuchunguza nyaraka.

Mteja akihoji, anajibiwa kwa ukali kana kwamba kuuliza ni kosa. Ukaguzi unapaswa kuongozwa na ushahidi, si dhana kwamba kila mwenye biashara anaiba kodi.

Tunataka ukaguzi wenye uratibu, maandalizi na heshima. Muda wa mteja una thamani; mapungufu ya uratibu ndani ya TRA yasigeuzwe kuwa usumbufu wa kudumu kwa wateja.
 
Pole sana Kwa Kupigwa TUKIO na wakusanya Mapato wa Bi Msumi! zote hizo anapeleka DUBAI na ZNZ
 
Watumishi wa TRA na serikali kwa ujumla hasa hawa wapya vijana wajengewe uwezo wa kutambua kuwa nafasi waliyonayo wamepewa kwa mujibu wa sheria na wanatakiwa wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria. Mteja au mkaguliwa ana haki zake pia, kwa hiyo asitendewe kama mtoto mdogo au mhaini kwa kufokewa au kutwezwa utu wake.​
 
Makundi tofauti ya ukaguzi wa TRA yamekuwa kero kwa wateja. Kila baada ya muda mfupi linafika kundi jipya, kila moja likisema linatoka kitengo tofauti. Haiwezekani kazi ya mteja iwe kuhudhuria vikao na maafisa wa TRA na kuwasilisha nyaraka zilezile kila mara, badala ya kuendesha biashara.

TRA iratibu vitengo vyake ili ukaguzi ufanyike kwa pamoja na kuhusisha maeneo yote yanayohusika, pale inapowezekana. Tofauti za vitengo hazipaswi kuwa mzigo kwa mteja.

Kinachokera zaidi ni baadhi ya maafisa kufika bila kusoma taarifa za ukaguzi uliotangulia, kurudia maswali yaliyokwisha kujibiwa na kuonekana kutokuwa na maandalizi ya kutosha.

Wengine, kwa kauli na mwenendo wao, wanaacha hisia kwamba tayari wanawachukulia wamiliki wa kampuni kuwa wezi kabla hata ya kuchunguza nyaraka.

Mteja akihoji, anajibiwa kwa ukali kana kwamba kuuliza ni kosa. Ukaguzi unapaswa kuongozwa na ushahidi, si dhana kwamba kila mwenye biashara anaiba kodi.

Tunataka ukaguzi wenye uratibu, maandalizi na heshima. Muda wa mteja una thamani; mapungufu ya uratibu ndani ya TRA yasigeuzwe kuwa usumbufu wa kudumu kwa wateja.
Nimeona watu 5 wakilalamikia juu ya jambo hili, ni wapangaji wenzangu jengo flani hapa sinza.
Kwa sasa kufanya biashara kama kampuni ni Hatari kubwa, madeni ya kodi ni makubwa kuliko mitaji ya kamouni zenyewe!.
Watatu wamefunga biashara
 
Back
Top Bottom