ST farms agribusiness

ST farms agribusiness

Mhina Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Posts
214
Reaction score
263
KILIMO CHA TIKITI MAJI TANGA KOROGWE . 0716898393
St farms ilianza na maandazi ya shamba kama inavyoonekana.

baada ya kumaliza kulima tulianza mchakato wa kutengeza mifereji na matuta au majaruba kwa vipimo tuta hadi tuta umbali wa mita mbili mpishano wa mifereji ya kupitisha maji ni mita moja.

baada kumaliza kuchora majaruba shambani tulianza na zoezi la kuchimba mashimo kwa vipimo shimo hadi shimo mita moja na nusu.

baada ya zoezi la mashimo kuisha St farms tuliandaa mbolea ya samadi ya mavi ya ng'ombe na mbuzi ya kutosha so samadi hyo ilichanganywa na kuwekwa kila shimo shamba zima.

baada ya zoezi la mbolea kuisha tulinywesha shamba zima maji kwenye mashimo ili kuwe na unyevu mzuri ili kurahisisha mbegu ikipandwa iote bila kukwama na kwenye mifereji kuona uwezo wake wa kupitisha maji wakati wa kunyweshea ili kurekebisha kwenye changamoto.

baada zoezi la kumwagilia maji siku inayofuata ni upandaji ambapo St farms tulichagua mbegu aina ya SUKARI F1 500gram inapanda ekari moja na robo kila shimo tuliweka mbegu mbili mbili kwa kuwa kulikuwa na unyevu na tulifukia kwa mchanga mwepesi bila kukandamiza mbegu baada ya siku ya nne zote zimechomoza vizuri naendelea .

Tafadhali Naomba like,share na follow kwa kupata ujuzi,masoko , taarifa na dondoo za uhakika kutoka shambani ST FARMS
View: https://www.instagram.com/p/DfzlI_uoMTM/?dlrf=MXRyMXB3cDExd2U0eg==
 

Attachments

  • file_000000001ef08208b66ce97f72bd58c1.png
    file_000000001ef08208b66ce97f72bd58c1.png
    2.1 MB · Views: 2
  • FB_IMG_1794369194032.jpg
    FB_IMG_1794369194032.jpg
    520.1 KB · Views: 2
  • IMG_20260926_101748.jpg
    IMG_20260926_101748.jpg
    834 KB · Views: 2
  • IMG_20260806_140314.jpg
    IMG_20260806_140314.jpg
    1.1 MB · Views: 2
Follow
 
Back
Top Bottom