Siasa za big results now (BRN)

Siasa za big results now (BRN)

epigenetics

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2008
Posts
269
Reaction score
83
Nina swali wana-JF. Hivi kweli kuna manufaa yoyote yaliyopatikana sasa katika malengo ya BRN? Ingawa malengo ya mpango huo ni mazuri, kuna matatizo kadhaa kuhusu 'kweli' katika matokea ya huo mpango kwa sasa.



Katika hii video (ambayo binafsi nadhani ni propaganda) nadhani wame-overstate matokeo ya malengo yao. Kwa mfano, Elimu (kuanzia dakika ya 5). Naona hapa wanaonyesha jinsi wanafunzi (na walimu) wa Shule ya Sekondari ya Mikindani (Mtwara) wanavyonufaika na BRN. Ukitazama video unaona kabisa jinsi wanafunzi (walimu) walivyolishwa maneno. Tatizo linakuja tukiangalia matokeo yao ya mtihani wa taifa ya 'juzi'. Tunaona jinsi zaidi ya nusu ya wanafunzi wa shule hiyo walifeli. Hiki ni kichekesho, yaani, shule wanayosema ni ya mfano, ndio moja ya iliyoshika mkia. Mbona wanatufanya watanzania mambumbumbu?



Screen Shot 2015-03-13 at 09.04.29.jpg
Screen Shot 2015-03-13 at 09.01.30.jpg
 
Last edited by a moderator:
Ndg yangu Hii ni Nchi Ma-Slogan; Kwanza CCM na Serikali yake Walishatuona Watanzania ni Wajinga ndo Maana Kila Kukicha wanakuja na Mapambio; Maisha bora kila Mtanzania, Kilimo kwanza, Mkukuta, Mkurabita, Matokeo Makubwa sasa (BRN) na Mengine mengi...

Mwl.Nyerere alipata Kusema, kama mtu akijua unaifahamu vizuri Almasi, na halafu akaja na Kioo Kinachongaa Vizuri na Kukwambia hii ndio almasi , basi ukikubali hapo yeye anakuona Mjinga.

Vile vile CCM walianza zamani Kutuona Watanzania ni Wajinga; Kwa maana ile mara ya kwanza baada ya Kugundua kuwa Maisha bora kwa kila Mtanzania ilikuwa ni Kiini macho, basi tungechukua maamuzi ya Kuwakataa kwenye Sanduku la kura lakini tukakubaliana nao kuwa kila Matanzania ana Maisha bora."Wakatuona Wajinga na Kutudharau kabisa"

Big Results Now (BRN)= Mipango Mikubwa ya Kuchota Maela ya Walipa Kodi (Escrow); Zamani walikuwa waniba interms of Miliones lakini kwa sasa Ni Big Results Now wanapiga Billiones of Money.
 
Siasa porojo. Leo nimeona hii pia.

B_9XgC8WYAACDae.jpg

Yaani wanalinganisha takwimu za ufaulu wa Div 1-3 wa mwaka 2012, na ufaulu wa Div 1-4 wa mwaka 2013 na kudai ufaulu umeongezeka maradufu (kutoka 10% mpaka 58%)!

Isitoshe, matokea ya 2014 yamekokotolewa tofauti na miaka mengine, kwahiyo hayawezi kutumiwa moja kwa moja na kuyalinganisha na miaka mengine. Yaani, alama za Distinction, Merit, Credit, Pass na Fail, pamoja na mfumo wa GPA hautoi picha kamili jinsi gani BRN imefanikiwa!

Propaganda
 
BRN no mradi usio na tija ulianzishwa kishikaji na kikwete eti iwe ndio legacy yake baada ya kung'oka mwezi October !
 
BRN=(Brain Receive Nothing).... ha ha ha , afu wameweka kwenye elimu.., hawa jamaa wametuchezea kweeli
 
Back
Top Bottom