Pinda, Wacha Mawazo ya Kikoloni

Pinda, Wacha Mawazo ya Kikoloni

Mentee

Senior Member
Joined
Jul 14, 2010
Posts
142
Reaction score
29
Hivi karibuni, wimbi la viongozi wa Serikali wamekuwa wakitoa matamko mepesi bila kufikiria.

Tamko la Waziri Mkuu, Pinda la jana kwamba watumishi wa Wilaya ya Bahi ni lazima wahamie Bahi na kwamba wasipotekeleza watachukuliwa hatua kali linashangaza sana. Mh. Pinda, kwani sheria au kanuni za utumishi wa umma hakuna?

Kama mtumishi anatakiwa kufika kazini saa 1:30 (saa moja na nusu ) asubuhi na anafika muda huo, kuna tatizo gani? Kwani watumishi wa Manispaa kwa mfano Temeke wanakaa Temeke? Je, Bahi kuna nyumba za kutosha watumishi wote?

Mh. Pinda, zungumza mambo ya maana na sio kulazimisha watu wakaishi mahali watakapolinda mizinga yako ya nyuki.
 
Ushauri wangu kwa Pinda ni kuwa asimamie kwa nguvu zote kuwa Serikali yote ihamie Dodoma, kwani ndio makao makuu ya nchi!

Kwanini mawaziri wanangangania DSM? Sababu zinazowafanya wanganganie DSM zinalandana na wale wa Bahi wanaokaa nje ya Bahi! Serikali itoe kwanza boriti kwenye jicho lake kabla ya kushughulikia kibanzi kwenye jicho la Wafanyakazi wa Bahi!
 
Mtu akiwa anaongea sana mfululizo huwa anakosa muda wa kutafakari na matokeo yake anaongea pumba.

Pinda ameongea pumba kama boss wake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Aanze yeye kuhamia dodoma aache kulialia watanzania waleo si wale waliodanganywa waende vijiji vya ujamaa viongozi wakabaki mijini wakila kuku.
 
Hili ndilo tatizo la viongozi wetu kukaa mbali na wananchi!
  1. Hawajui mazingira ya maeneo wanayoyaongoza;
  2. Hawajui matatizo ya wananchi wanaowaongoza;
  3. Hawajui haki za watumishi; na
  4. Hawajui mazingira wanayoishi watumishi.
Kwa kuwa viongozi wetu wanaishi peponi, wanadhani kila mtu yuko kama wao!
  1. Watumishi wa umma wanakopwa haki zao;
  2. Watumishi wa umma wanakopwa maslahi yao; na
  3. Watumishi wa umma wamekuwa kama nyenzo za kufanyia kazi na si binadamu.
 
Hivi karibuni, wimbi la viongozi wa Serikali wamekuwa wakitoa matamko mepesi bila kufikiria.

Tamko la Waziri Mkuu, Pinda la jana kwamba watumishi wa Wilaya ya Bahi ni lazima wahamie Bahi na kwamba wasipotekeleza watachukuliwa hatua kali linashangaza sana. Mh. Pinda, kwani sheria au kanuni za utumishi wa umma hakuna?

Kama mtumishi anatakiwa kufika kazini saa 1:30 (saa moja na nusu ) asubuhi na anafika muda huo, kuna tatizo gani? Kwani watumishi wa Manispaa kwa mfano Temeke wanakaa Temeke? Je, Bahi kuna nyumba za kutosha watumishi wote?

Mh. Pinda, zungumza mambo ya maana na sio kulazimisha watu wakaishi mahali watakapolinda mizinga yako ya nyuki.


......

Na viongozi wote wa serikali waamie Dodoma makao makuu.
 
Kwanza unapomuhamisha mtumishi wa serikali kutoka sehemu moja kwenda nyengine ni lazima umlipe gharama za kumuhamisha likiwemo suala la kumsafirisha yeye na familia yake na mali zake, na vilevile umlipe na posho ya usumbufu.

Je hawa wanaotakiwa kuhama wameshapewa stahiki zao?
 
Back
Top Bottom