Kikwete Urais hawezi, anaharibu kila kukicha. Mnyonge mnyongeni.
Na haki yake mpeni. Historia na wasifu wake kabla ya kupewa Uwaziri Mdogo ilikuwa tosha, na ya kupendeza.
Kwanza, alikuwa ni askari wa mguu katika ngazi za chini kabisa za uongozi wa CCM alipokuwa wilayani huko. Kwa hiyo, alivijua vichochoro na uongozi wa mikoani Tanzania kabla ya kuwa Waziri mdogo.
Pili, kwa mujibu wa Wikipedia (wenye ukweli zaidi wakosoe) Kikwete ndio alitumwa na CCM kwenda kukijenga CCM visiwani siku ASP ilipoungana na TANU. Unaweza kusema hii kazi wakati ule itakuwa ilikuwa rahisi na shwari kwa sababu Bara na Zanzibar tulikuwa tuko likizo baada ya harusi. Lakini itakuwa ilimsaidia kuzijua siasa za chama za Zanzibar, na kujenga mahusiano kule. (Na hu mtaji ameutumia kwa uwezo wa hali ya juu sana juzi Bungeni alipobuni hoja ya asili kuliko zote ambazo zimewahi kuzungumziwa - Zanzibar si Nchi kimataifa, ni nchi Kitaifa. Hoja ya ajabu, ya kuchekesha, ya kutunga, lakini imetuliza Wazanzibar!
Lingine, alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Ulinzi cha Chama mwaka 1980. Na wakati ule chama kilishika utamu, kwa hiyo yeye na kina Kitine na Mahiga walikuwa wanafanya kazi zile zile. Yani alikuwa ana nishani katika Usalama wa Taifa.
Jeshini, alikuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa Monduli. Alikuwa anawaandikia wanafunzi wa Kijeshi dossier za Siasa za chama, yaani za nchi, kwa sababu wakati ule Chama ndicho kilishika utamu. Kwa hiyo, ana nishani za Siasa za Kijeshi, mahusiano na uongozi jeshini, kitu muhimu labda kuliko kuwa askari ambae hajawahi kuongoza kitu. (Kutoka hapo akaenda CCM Masasi huko, sijui ilikuwaje hapo.... ???)
Kwa hiyo, kwa kweli, Kikwete alistahili kupewa uwaziri Mdogo kwa sababu alishashika kazi muhimu sana.