Mtu akishakufa anatoa wapi power ya kufanya matukio?

Mtu akishakufa anatoa wapi power ya kufanya matukio?

Nafikiri NENO unalolitoa kwa kuumia na kudhamiria (tuseme kwa msisitizo wa uchungu na kumaanisha) huwa lina nguvu. Tunasoma Mungu aliumba dunia na vitu vilivyomo kwa neno.... alitamka tu. Nasi tuna uwezo na tuna siri ya Mungu ndani mwetu... inawezekana ndio maana tukitamka wakati mwingine hutokea. Hivyo nguvu ya NENO lililotamkwa hutenda kazi na si kwamba mtu au roho yake huja kutenda.

Km napata kitu vile??
 
naendelea kusoma comments zenu wakuu,naona leo mmeandika bila masihara.
_asanteni sana.
 
Pole sana kwa kutatizika na matukio uliyoelezea. Sasa ondoa shaka kabisa, nakupa majibu ya uhakika kabisa kulingana na Biblia:
1. Mtu akifa hawezi kufanya kitu chochote kile, hana uwezo wa kufanya jambo lolote linalofanyika chini ya jua. Swali. Hayo matukio uliyosimulia yaliwezaje kutimia?
2. Shetani ibilisi ni muongo (tapeli) na anaitwa baba ya uongo. Alimdanganya Hawa kwamba hatakufa bali eti kitendo cha kufa ni kubadilika na kufanana na Mungu!
3. Shetani anachezea akili za wanadamu kwa kuwafanya waamini kwamba wakifa hawafi kabisa na wanaweza kutekeleza mambo kadhaa. Matukio uliyosimulia ni baadhi ya mazingaombwe yanayofanywa na shetani ili kutufanya tuendelee kuamini kwamba tukifa hatufi kabisa
4. Mungu alishasema "utakufa hakika". Utarudi kwenye udongo alikokutoa. Roho (yaani nguvu ya uhai iliyo ndani yako) itamrudia yeye aliyekupatia.
5. Ukiujua ukweli utakuwa huru na mbinu mbaya za shetani!
Sina pingamizi na maelezo haya kwa suala nyeti na gumu kama hili la kiroho, ila ningekushauri kuchambua na kunyumbua zaidi maneno ya mwenyezi mungu katika vitabu vitakatifu ambavyo ndivyo vinatuweka mbele yake Daima.



Tumwache Mwenyezi Mungu aitwe Mungu, Kumbuka Mwenyezi Mungu anajibu maombi kwa wanaomkiri na kumwamini kwa Imani iliyokamili.

Na anaejua imani ya binadamu ni Mmoja tu ni Yeye Mola wetu mwenye sifa lukuki nisizoweza kuzitaja mimi nikazimaliza na asiyefanana na binadamu aliemuumba kwa kuona kusikia na kujua na kutoa hukumu au kujibu maombi.

Binadamu akifa, kinachoishi hapo, ni Neno kwa maneno mengine nafsi, na siyo mwili. Kwa imani hiyo.
Kwa maelezo yanayojengwa na Imani ya uwepo wa Mwenyezi Mungu.
Sasa kama binadamu alimwomba Mwenyezi Mungu kwa Imani, na mwenyezi Mungu akapokea maombi yake, kwa kuzingatia fundisho ambalo litatolewa au ujumbe ambao utatolewa kwa wanadamu katika JIBU HILO LA OMBI LA BINADAMU HUYO KWA MTU ANAMWONA AMEMKOSEA NA KUMWOMBA MWENYEZI MUNGU AMHUKUMU BAADA YA KUFA KWAKE ni dhahiri atajibu maombi ya nafsi hiyo baada ya kurudi kwake.

Hapa siyo maiti aliefanya miujiza, kwani maiti imeoza, na wala siyo nafsi ile, kwani nayo mbele ya mwenyezi Mungu haina nguvu ya kuendelea kutenda.

Ila huko Mbinguni inafaidi matunda ya yale iliyoyatennda wakati ikiwa na mwili Duniani, na miongoni mwa matendo hayo ni kuwalea watoto wake kwa njia ya matendo ya kumpendeza Mwenyezi Mungu kwa kumshuhudia na kumkiri kuwa ndiye Muumba mwenye mamlaka na mwili na maisha ya Binadamu.

Kwa maelezo hayo ninamjibu muuliza swali kuwa kinachotokea hapa ni majibu ya Mwenyezi Mungu kwa maombi ya Mzazi wake au hata mtu aliemtendea mabaya wakati wa Uhai wa mwili hapa Duniani na yeye akamkabidhi Mwenyezi Mungu amhukumu kwa Imani yake ya Uwepo Mwenyezi Mungu.

Tatizo kidogo ni kutokufahamu au kusikia hayo maombi yake wakati anafanya, kwa maana hiyo wewe ndiyo unamwona kuwa alimhukumu yeye muda uleule na kwamba sasa baada ya kufa anatekeleza. Hapana.

Na kwa wanaodai ni mazingaombe basi labda mtu huyo aliishi hivyo kimazingaombe au kwa Imani ya Mizimu, na kama ndivyo basi hiyo inaweza kuwa hukumu ya hiyo maiti kwani inawezekana hata huko kufa siyo kwa kweli ni kwa mazingaombe ili amkomowe mbaya wake.

Mkuu,

Tafadhali soma kwanza Mhubiri 12:7 na kisha Mhubiri 9:5. Utapata majibu ya maswali yako.

Barikiwa.
Haya ni majibu rahisi kwa maswali magumu hayasaidii.
 
naendelea kusoma comments zenu wakuu,naona leo mmeandika bila masihara.
_asanteni sana.

ni hivi, roho ina nguvu sasa inaona, inasikia, inaishi me sijui. mtu akisema nikifa nizikwe sehemu fulani then mazishi yanakuja kufanyika tofauti na wosia wa marehemu alioacha utaona timbwili litakalotokea hapo!
 
Pole sana kwa kutatizika na matukio uliyoelezea. Sasa ondoa shaka kabisa, nakupa majibu ya uhakika kabisa kulingana na Biblia:
1. Mtu akifa hawezi kufanya kitu chochote kile, hana uwezo wa kufanya jambo lolote linalofanyika chini ya jua. Swali. Hayo matukio uliyosimulia yaliwezaje kutimia?
2. Shetani ibilisi ni muongo (tapeli) na anaitwa baba ya uongo. Alimdanganya Hawa kwamba hatakufa bali eti kitendo cha kufa ni kubadilika na kufanana na Mungu!
3. Shetani anachezea akili za wanadamu kwa kuwafanya waamini kwamba wakifa hawafi kabisa na wanaweza kutekeleza mambo kadhaa. Matukio uliyosimulia ni baadhi ya mazingaombwe yanayofanywa na shetani ili kutufanya tuendelee kuamini kwamba tukifa hatufi kabisa
4. Mungu alishasema "utakufa hakika". Utarudi kwenye udongo alikokutoa. Roho (yaani nguvu ya uhai iliyo ndani yako) itamrudia yeye aliyekupatia.
5. Ukiujua ukweli utakuwa huru na mbinu mbaya za shetani!

MKUU ROHO HUENDELEA KUISHI,..USIMSINGIZIE SHETANI KILA WAKATI,MANENO ULIYOTAMKA KWA DHATI KABILA ROHO HAIJAACHA MWILI HUWA HUWA KWELI.
 
hizo story za wafu zipo sana na zinatokea sana kwenye jamii zetu lakini swala la msingi ni kuheshimiana na kumwamini Mungu pekee

Yeah,nikweli kuna 1 ameuliza kwanini Nyerere acwatokee hawa Jamaaa wanaopenda kujiita Viongozi wetu ikiwa ni maJIZI yanafilisi NCH kwakawaida ile inatokea kwa mtu ulie na NASABA nae2 cvinginevyo..!!
 
Sasa hata kama maiti inasikia, inatatua vipi hayo matatizo? Kama kuna ukweli sana kwenye hili la maiti basi ni bora tufe tu wote maana tunakuwa na nguvu zaidi kuliko kubaki hai tukiwa dhaifu dhaifu tu au wewe unasemaje?

Kinachokufa ni Mwili tu...! ROHO inaendelea kuwepo..!!
 
The Boss kwanini nyerere asiwauwe hawa mafisadi ikiwa roho inaishi?

It's just a matter of time, muda wao unakaribia sana kanuni za Muumba hazibadiliki kama ume prove kwa hiyo mifano miwili uliyotaja basi amini siku yaja....!
 
ni hivi, roho ina nguvu
sasa inaona, inasikia, inaishi me sijui. mtu akisema nikifa nizikwe
sehemu fulani then mazishi yafanyike tofauti utaona timbwili
litakalotokea hapo!
iko hivi kwenye utata shetani ndipo hujiinua palipo na amani shetani hapati nafasi, sasa mtu keshaanza utata hata kabla hajafa eti nikifa nisizikwe sijui wapi aah namwingine nikutoa laana tuu kwa watoto eti siku nikifa sijui itakuaje vile?! mimi navyoona hizo zote ni propaganda za shetani ilikukamata akili za wanadamu minavyojua aliekufa kukumbulake limekwisha ndio maana ya kifo sometimes ni majini yanakuja kuwachezea tuu ila kama unajua taratibu za Mungu wa kweli wala haubabaki
 
Karesearch kangu kakikamilika nitakua na la kujibu hapa!
 
[FONT=times new
roman]wakuu heshima kwenu.,

Kuna maswali huwa najiuliza sana.
Inakuweje mtu akishakufa anaweza tena kufanya matukio na laana ikafanya
kazi?

Mfano kuna jamaa mmoja alikuwa anaishi Canada na alikuwa na uwezo sana
sana ila huku Tanzania mzazi wake akawa anamuhitaji kuja kumjulia hali
na amletee na wajukuu zake jamaa akawa haji yeye ni kutuma pesa tu na
mzazi hakuwa na haja nazo kwani na yeye zilikuwemo .

Mzazi akamtumia ujumbe kuwa ukisikia nimekufa kabla hujuja tutazikwa
wote!

Jamaa akaone masihara, akapuuza siku ya siku mzee akafa,jamaa akafunga
safari na mke na watoto kuja kuzika kutua kia akapewa gari na rafiki
yake,hakufika home ajali,yeye na mtoto wake wakafa ikabidi msiba
usogezwe wakazikwa na baba yake.

Mwingine alikuwa anaishi Dar ni tajiri ajabu baba yake kijijini alikuwa
mgonjwa na jamaa hakwenda kumuona akawa anatuma tu pesa,mzee akasema
kama hauji ukisikia nimekufa HUTANIZIKA,haikupita muda mzee akafa jamaa
akaenda na mafaki kuzika kwa mbwebwe na magari ya kifahari.

Wakapewe mwili huko mochwari wakaenda wakazika baada ya mazishi na
matanga kuvunjwa wakaja MASAI kudai huo mwili kuwa wakikosea ni wa ndugu
yao,kweli kufukua kaburi kitizama ni masai kumbe baba alibaki mochori
kimiujiza tu!

Matukio hayo na mingine ni liyowahi kuyasikia ndio inanifanya najiuliza
inakuweje mtu akishakufa anakuwa na power ya kutenda matukio?

Niwie radhi nimeandika kwa simu,nimefupisha story
[/FONT]
kwasisi ambao hatutoki rohoni tunastukiaga mapemaa! umetangangaziwa kifo bila wewe kujijua halafu unakaa kimya, shetani huwa anataratibu zakumuingia mtu halafu yule mtu anaropoka maneno kwakutekwa ufahamu mnabakia kusema babake alisema akifa nayeye atamfata kumbe sio babayake aliesema ni shetani alitumia kinywa cha baba yake kuwatangazia kwamba atakapo kufa baba na mtoto namtoto naeatafuatia ukikaa kimya ndio imetoka hivyo unakujakufa kweli vivyo hivo anaweza kutumia maneno ya aina nyingine msipokuwa macho mikasa mingine tena, hizo zote ni mbinu za shetani, tena muwe macho mtu yoyote anapokuambia nikifa sijui utaona tangua hiyo kauli yake hapohapo siyo yeye ni lusfer anakutamkia mpinge hapohapo na futa maneno anayokutamkia
 
Umenikumbusha ASIEAMINI MAITI INASIKIA KILA KITU NI MUNAFIKI.

Leomimi
Umeanza vizur ume conclude vibaya,Maandiko yana tuambia kwamba mtu akifa basi hasikii jambo lolote wala haneni.Sikulaumu sana coz uelewa wako umeishia hapo.
Kama mait wangekuwa wanaskia,?
Mafarakano ya mirathi yasingekuwepo pia kama maiti wangekuwa wanaskia basi hata mimi ningeenda kumwomba marehem bab yangu aniombee huko kwa mungu nipate japo kausafiri kakutembelea,au ww ushawahi fanya kama navyo waza mimi na ukafanikiwa?
Manake ww unaamini maiti anaskia!
Ni ajabu.
Ukila fofofo husikii lolote wala hujitambui hata kama wakuguse namna gani,itakuwa kwa maiti ambae moyo umekata mawasiliano ya mifumo yoote ya fahamu?
Hebu tembelea Mahosptalini ukibahatika kuonana na mgonjwa aliefanyiwa oparesheni muulize alikuwa anaskia nn baada ya kupigwa sindano ya nusu kaputi.
Atakae kwambia alikuwa anaskia kilakiltu kinachoendelea,kama vile dk akiweka mkasi kwenye bakuli basi mikasi inagongana,yy akwambie aliskia sauti,Huyo ni Mzandiki mkubwa.
Waulize waliofanyiwa hiyo kitu.That is simple research do it.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wanaopinga wajiulize. Laana ni shetani? Maagizo ya mtu kabla hajafa nayo ni shetani? Ninavyojua, roho za watu wazima na roho zilizoacha mwili ni roho moja from one universal spirit. Kama roho inafanya evils au good ni swala lingine.
 
Umenikumbusha bibi yangu alikuwa hai akamwambia mdogo wake wa kiume tena anamtaja kwa jina fulani fulani fulani wewe nikifa hutaniona utashuhudia kaburi langu tu wewe endelea kunichezea yani huwa nakumbuka hata position aliyosimama akitamka hayo kweli babu yangu yule alisafiri ghafla tu huku nyuma bibi akafariki kwa kuanguka tu na mdogo wake alifika siku ya tatu baada ya kuzikwa dada yake kweli hapa kuna jambo nakubaliana na wewe lkb pia tujiulize kwa nini mfano mtu anapata matatizo huku duniani na akienda kuzuru makaburi ya wazazi wake au wazee wao kama walitangulia huwa yale matatizo yanaisha? Kuna jambo hapo ila ASIEAMINI MAITI INASIKIA KILA KITU NI MUNAFIKI.

Biblia inasema, `wafu hawajui lolote'
 
Kwa wanaopinga wajiulize. Laana ni shetani? Maagizo ya mtu kabla hajafa nayo ni shetani? Ninavyojua, roho za watu wazima na roho zilizoacha mwili ni roho moja from one universal spirit. Kama roho inafanya evils au good ni swala lingine.

roho inayofanya evils ndo shetani and vice versa is true!
 
Pole sana kwa kutatizika na matukio uliyoelezea. Sasa ondoa shaka kabisa, nakupa majibu ya uhakika kabisa kulingana na Biblia:
1. Mtu akifa hawezi kufanya kitu chochote kile, hana uwezo wa kufanya jambo lolote linalofanyika chini ya jua. Swali. Hayo matukio uliyosimulia yaliwezaje kutimia?
2. Shetani ibilisi ni muongo (tapeli) na anaitwa baba ya uongo. Alimdanganya Hawa kwamba hatakufa bali eti kitendo cha kufa ni kubadilika na kufanana na Mungu!
3. Shetani anachezea akili za wanadamu kwa kuwafanya waamini kwamba wakifa hawafi kabisa na wanaweza kutekeleza mambo kadhaa. Matukio uliyosimulia ni baadhi ya mazingaombwe yanayofanywa na shetani ili kutufanya tuendelee kuamini kwamba tukifa hatufi kabisa
4. Mungu alishasema "utakufa hakika". Utarudi kwenye udongo alikokutoa. Roho (yaani nguvu ya uhai iliyo ndani yako) itamrudia yeye aliyekupatia.
5. Ukiujua ukweli utakuwa huru na mbinu mbaya za shetani!

Ni kwa mawazo yangu tu lakini,, nadhani yote ulioandika ni ya ukwel but sio kwamba shetani ndo huwa hufanya hayo matendo kimiujiza ila hayo maneno yanayotolewa huwa ni kama nadhiri na huwa yanatolewa kwa hisia ya kweli toka ndani ya moyo,, hata katika kitabu cha neno la MUNGU imeandikwa "Wakajifunga kwa maneno ya kinywa chao" hakuna kitu chenye nguvu kama neno kutoka kinywani
Ref: Hata MUNGU aliumba kwa NENO so shetani hausiki hapo
 
Back
Top Bottom