Moto wateketeza hoteli 6 Zanzibar

Moto wateketeza hoteli 6 Zanzibar

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,234
Reaction score
7,417
Hoteli sita zimeteketea kwa moto katika eneo la Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar huku hoteli tatu kati ya hizo zikiripotiwa kuathirika vibaya katika tukio lililotokea leo, Novemba 21, 2026.

Akizungumza na AyoTV kwa njia ya simu, Katibu wa Sheha wa Nungwi, Khamis Kibata amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa moto huo ulizuka majira ya mchana, huku ukiwa umeathiri hoteli sita pamoja na maduka ya Wafanyabiashara Wadogo wanaouza vinyago, huku akisema baadhi ya majengo ya hoteli hizo yamejengwa kwa makuti, hali iliyochangia moto kusambaa kwa kasi na kusababisha uharibifu mkubwa.

Kibata amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanikiwa kuuzima moto huo na hadi sasa hakuna taarifa za Mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo, huku chanzo cha moto kikiwa bado hakijafahamika na uchunguzi ukihitajika kubaini iwapo ulisababishwa na hitilafu ya umeme au sababu nyingine.

 
Uhai ndio muhimu. Kama hakuna aliyepata madhara ni jambo jema. Hoteli zimekatiwa bima italipa
 
Nadharia mbili;-

1. Zimechomwa ili kupisha wawekezaji wapya wajenge hotel za kisasa zaidi kuliko hizo old fashioned!!?
2.Destabilization ya uchumi wa watu Fulani ,vita vya kiuchumi plus kisiasa kimedani,kukomoana kutiana hasara kumfilisi mtu fulani!kijasusi zaidi,kumtia simanzi kumuongezea msongo hatimaye frustrated then maturubai!!

Nawaza hivyo coz tupo kwenye zama ambazo ajali yoyote inatafsiriwa kivingine Kwa trend ya matukio ya amani tangu uchaguzi!

Nawaza!!
 
Back
Top Bottom