Mhdiwani
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 650
- 712
Tangu mpendwa wetu baba atutoke familia yetu ilianza kutawaliwa na ndugu wa baba,,,
tuliishi maisha magumu kiasi lakini sio kama hivi mjomba anavyotulea
nakumbuka mwaka juzi baba mdogo wakati anataka kutuachia mlezi wa familia hatujatarajia kama mjomba ndo angerithi familia kwasababu baba mdogo alikua na maswahiba zake ambao walionyesha nia ya dhati ya kutulea ,,
kila mtu aliamini baada ya baba mdogo kuondoka basi familia yetu ingepaa kiuchumi,,
kweli tulimchukia baba mdogo kwasababu alikua mwenye huruma hata pasipohitaji huruma ,,alikua mcheshi Alituruhusu kufanya vurugu zote lkn tusimtilie kitumbue chake mchanga,,tunakukumbuka sana baba mdogo,
Baba mdogo najua unanisikia na pia unaona haya tunayopitia mjomba anatutesa sana ,,chakula cha tabu tumekonda sana ,,
juzi nyumba eneo dogo la nyumba yetu lilibomoka kwa bahati nzuri majirani na wafadhili wakatuchangia ili tujenge palipobomoka ,,aaah unajua alichofanya mjomba. pesa zote kachukua na kuanza kutembea kwenye biashara zake na kuwauliza wasimamizi hapa kuna shida gani? basi akitajiwa anatoa pesa ,,wakati biashara inajiendesha yenyewe na inabajeti take,
sisi huku nyumbani tunalala nje chakula hakuna na ukimuuliza mjomba vipi mbona hivi lazima utafukuzwa nyumbani kilichobaki sasahivi ni kumsifu tu anko kwa nyimbo na mapambio ili tuendelee kuishi lakini baba mdogo kwanini umetufanyia hivi? nakuomba Tafadhali najua bado unaushawishi mkubwa kwenye familia yetu Fanya figisu zozote zile kipindi kijacho tusiendelee na anko ,,
najua unaweza we mtoto wa mjini pale unawatu wako baba mdogo,,mbona uliweza kwa yule swahiba wako japo wengi tuliamini ndo utatuachia huyo
Natanguliza shukrani kwa wanafamilia wenzangu popote pale walip.
Asanteni