Wana jamvi.
Kwa wanaopenda kujisomea vitabu kwa wingi, sidhani kama watakua hawajawahi kupitia hadithi ya mfalme juha!
Kwa wale wavivu ngojq niwaandikie summary hapa harafu tuhusanishe ma siasa zetu hapa tanzania.
Mfalme juha alishonewa vazi zuuri la kufikirika, fundi mshonaji alimpa imani mfalme juha kuwa ati hilo vazi la kufikirika linampendeza saana mfalme. Bahati mbaya mfalme alimuamini saama fundi wake. Fundi alimaliza kushona vazi lake la kufikirika na akaenda kumvisha mfalme juha.
Mfalme juha alokuwa hataki kusikia la imamu wala la shehe, hivyo fundi alimvisha mfalme juha vazi baada ya kuchojoa nguo zoote! akalivaa vazi la kufikirika ila bahati mbaya hakukua na mtu yeyote aliyekuwa na uwezo wa kumuambia chochote mfalme juha, kumbe mfalme juha alikuwa mtupu kama alivyo zaliwa isipokuwa fundi wake tuu alimuambia kwa utupu wake huo anapendeza na vazi lake la kufikirika!
Akatokea maskini jasiri, aliye kata tamaa na maishayake, asiyogopa kufa akamuambia mbona mfalme wetu mtukufu uko uchiii! Mfalme mwisho wa siku alighadhabika ati kwa sababu wasaidizi wake hawakumueleza ukweli kuwa yu mtupu na hamna kitu kama vazi la kufikirika.
Tafakuri yangu ni kama huyo mfalme baada ya kuonyesha tupu yupo tayari kuendelea kuwa mfalme?
Tafakari hili.