Majini & Mapepo 👻🤔

Majini & Mapepo 👻🤔

Kwanini Mungu alimuacha shetani atushawishi

Swali langu ni moja shetani aliacwa kwa sababu gani?

Yaani shetani kaumbwa kwa ajili ya kutushawishi?
Kama sio hivyo kwanini anacwa na anaonekana kua mharibifu?
Kwanza hakuna kiumbe kilichoumbwa chenye kuitwa shetani bali shetani ni jina la sifa kwa kiumbe mwenye kutenda matendo maovu, hivyo hajaumbwa shetani ili kushawishi watu bali huyo anayeitwa shetani amekuja kuitwa hivyo baada ya uovu wa matendo yake. Kama ulivyoelezea kuwa huyo shetani kwa mujibu wa ukristo alikuwa ni malaika na kwa mujibu wa uislamu alikuwa ni jini tena mchamungu.

Turudi kwenye kile nilichoeleza kwamba shetani hana nguvu ya kumlazimisha mtu kufanya maovu, kwa maana hata kama asingekuwepo shetani bado watu wangefanya maovu maana shetani ni mshawishi tu.
 
Ni kweli Mungu ndiye Muumba wa vyote, lakini kuumba uwezo wa kuchagua si sawa na kumchagulia mtu kila tendo. Muumba wa uwezo wa kuchagua si lazima awe msababishaji wa kila uchaguzi unaofanywa.

Asante , nitafurahi tuendelee na mjadala huu. Lengo ni kutafuta uelewa, si kushindana. Hii iwe separate topic

Mungu ndiye aliyeumba uwezo wa mwanadamu kutenda, lakini si lazima awe ndiye anayechagua matendo yake. Kujua mwanzo na mwisho hakumaanishi kulazimisha matendo hayo. Uwajibikaji unatokana na uchaguzi wa mwanadamu, si uwezo aliopewa na Mungu.

Si kila ombi hupewa. Katika kisa cha Shetani, Mungu alimpa muda kwa hekima na kusudi lake, si kwa sababu anakubaliana na maovu yake. Lakini swali la kwa nini Mungu aliruhusu hilo licha ya kujua matokeo yake ni mjadala mpana unaostahili kuchambuliwa. nao tuupe topic yake pia

Ndilo swali muhimu . Katika Uislamu, kuruhusu jambo litokee hakumaanishi kulikubali au kulisababisha. Hata hivyo, sababu ya Mungu kuruhusu Shetani apewe muda licha ya kujua madhara yake ndiyo hoja tunayopaswa kuichambua pia

thanks

Kwa mtazamo wa Kiislamu, dunia si mahali pa ukamilifu bali ni mahali pa mtihani. Udhaifu unatupa nafasi ya kuchagua, kujifunza, kutubu na kutenda mema. Hata hivyo, kwa nini Mungu alichagua mfumo huu badala ya mwingine ndilo swali la hekima yake

Kuruhusu jambo litokee hakumaanishi kulifurahia au kulikubali. Mzazi anaweza kuruhusu mtoto apitie changamoto ili ajifunze, bila kufurahia maumivu yake. Swali letu ni kwa nini Mungu anaruhusu maovu, si kama anayafurahia

Ni kweli mkuu, madai yanahitaji ushahidi. Lakini katika Uislamu, majini ni viumbe wa ghaibu, si viumbe ambao binadamu wote wanaweza kuwaona. Ushahidi wao katika imani ya Kiislamu unatokana na Qur'an. Hoja yetu ni kama unakubali Qur'an kuwa chanzo cha ushahidi au la.

Hata Wakristo wanaamini uwepo wa viumbe wa kiroho wasioonekana kwa macho, kama malaika na mapepo. Kwa hiyo, kutokuonekana kwa kiumbe si uthibitisho kwamba hakipo. Tofauti ni kwamba Uislamu unawaita majini, huku Ukristo ukizungumzia zaidi roho na mapepo.

Kufanana kwa simulizi hakuthibitishi kunakili. Qur'an inasimulia habari za manabii hao kwa mtazamo wake na ina mafundisho tofauti. Kwa mfano, kuhusu uungu wa Yesu, Utatu na kusulubiwa kwake, kuna tofauti kubwa kati ya vitabu hivyo. Je, kufanana kwa baadhi ya simulizi kunatosha kuthibitisha kwamba kimoja kimenakili kingine? Tafadhali niwekee mfano japo mmoja wa hicho kilicho kopiwa kutoka biblia kwenda kwenye quran

Mkuu, umeonyesha kwamba Qur'an na Biblia zinatofautiana, lakini bado hujathibitisha kwamba Qur'an imenakili Biblia. Qur'an 4:157–158 inapingana wazi na madai ya kusulubiwa kwa Yesu. Kama Qur'an ni nakala ya Biblia, kwa nini inakataa baadhi ya mafundisho yake? Kutofautiana si ushahidi wa kuiga, bali ni ushahidi kwamba vitabu hivyo vinafundisha mambo tofauti.

Si kwamba dunia ni ya dhiki pekee mkuu. Uislamu haukatazi starehe na furaha, bali dunia ina raha na mitihani. Tofauti ni kwamba starehe za dunia ni za muda, wakati Akhera imekusudiwa kuwa makazi ya kudumu.

Qur'an inaeleza wazi kwamba starehe za dunia ni za muda mfupi na zinaweza kumdanganya mwanadamu.

1. Surat Aal-Imran 3:185

Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.

2. Surat Al-Hadid 57:20

Qur'an inaeleza kwamba maisha ya dunia ni mchezo, pumbao, pambo, kujifakhirisha na kushindana kwa mali na watoto. Mwisho wake ni starehe ya udanganyifu.

3. Surat Al-An'am 6:32

Na maisha ya dunia si chochote ila ni mchezo na pumbao, na nyumba ya Akhera ni bora kwa wale wanaomcha Mungu.

4. Surat Al-Kahf 18:45

Mungu anafananisha maisha ya dunia na mimea inayostawi kwa mvua, kisha hukauka na kutawanywa na upepo.

Uislamu haukatazi kufurahia maisha ya dunia, lakini unatukumbusha kwamba starehe zake ni za kupita na hazipaswi kutufanya tusahau Akhera.

Thanks
Mkuu Jagina asante kwa muda ulioutenga kujenga mjadala na mimi. Nashukuru sana kwa maoni yako na uchambuzi wako

Lakini niseme ukweli nimekosa majibu yanayoniridhisha

Nimeona kama tunazunguka na mwisho tunarudi pale pale,bila kupata majibu ya moja kwa moja.

So, napenda nikushukuru kwa hapa Karibu tena kwenye mijadala mingine zaidi na kama una jambo la kuongeza, karibu pia 🤝
 
Kwanza hakuna kiumbe kilichoumbwa chenye kuitwa shetani bali shetani ni jina la sifa kwa kiumbe mwenye kutenda matendo maovu, hivyo hajaumbwa shetani ili kushawishi watu bali huyo anayeitwa shetani amekuja kuitwa hivyo baada ya uovu wa matendo yake. Kama ulivyoelezea kuwa huyo shetani kwa mujibu wa ukristo alikuwa ni malaika na kwa mujibu wa uislamu alikuwa ni jini tena mchamungu.

Turudi kwenye kile nilichoeleza kwamba shetani hana nguvu ya kumlazimisha mtu kufanya maovu, kwa maana hata kama asingekuwepo shetani bado watu wangefanya maovu maana shetani ni mshawishi tu.
sasa inakuwaje shetani akushawishi wewe hili na yule lile? Kumaanisha kwanini waovu wote hawakamatiki katika ovu moja au kwa kiwango kilekile?
 
Mkuu Jagina asante kwa muda ulioutenga kujenga mjadala na mimi. Nashukuru sana kwa maoni yako na uchambuzi wako

Lakini niseme ukweli nimekosa majibu yanayoniridhisha

Nimeona kama tunazunguka na mwisho tunarudi pale pale,bila kupata majibu ya moja kwa moja.

So, napenda nikushukuru kwa hapa Karibu tena kwenye mijadala mingine zaidi na kama una jambo la kuongeza, karibu pia 🤝
Shukrani isipokuwa nasikitika hukuniwekea hizo hoja ambazo hukuridhika nazo . Mimi nipo wakati wote hata Kama kwenda kwa hoja moja moja.
 
Shukrani isipokuwa nasikitika hukuniwekea hizo hoja ambazo hukuridhika nazo . Mimi nipo wakati wote hata Kama kwenda kwa hoja moja moja.
Kaka niliweka kwenye quote zangu
Wewe ukawa unanijibu kwa mizunguko badala ya kua straight nimejikuta nikikosa majibu ya wazi naona kama ni kuzunguka zunga then tunarudi pale pale
 
Kaka niliweka kwenye quote zangu
Wewe ukawa unanijibu kwa mizunguko badala ya kua straight nimejikuta nikikosa majibu ya wazi naona kama ni kuzunguka zunga then tunarudi pale pale
Bado hujaniambia ni hoja ipi na jibu gani nilikupa ambalo hukuridhika nalo
 
Bado hujaniambia ni hoja ipi na jibu gani nilikupa ambalo hukuridhika nalo
Kwamba niandike tena aiseee
Angalia post niliyosema usinipe majibu ya AI maswali ni yale

Afya yangu haipo sawa sana naona uvivu kurudia kuandika kitu kile kile
 
Kwamba niandike tena aiseee
Angalia post niliyosema usinipe majibu ya AI maswali ni yale

Afya yangu haipo sawa sana naona uvivu kurudia kuandika kitu kile kile
Sasa naona umegeukia AI , sawa Kama nimekukwaza kwa majibu unayoyaona hayakakuridhisha. Usianze kurudi kuilaumu AI.
Ukipata nafasi Mimi nakuruhusu kuitumia dude lolote uniambie ni wapi majibu yangu hayakukuridhisha
 
Nimerejea hilo ili ukaangalie maswali yangu kwa sababu siwezi kurudia kuandika kitu kile kile mkuu

Sitaki kutumia dude lolote akili yangu inatosha
 
Hello great thinkers 🫡

Sometimes huwa najiuliza, hivi kweli majini na mapepo wapo, au ni chai tu? 🤔

Waislamu wanayaita majini, huku Wakristo wakitumia majina kama mapepo wanapozungumzia viumbe wa kiroho wanaohusishwa na uovu
(Nadhani hivi viumbe wanaviita vya kiroho kwa sababu havionekani sijui sana kuhusu hili)

Twende nalo sasa 👇

1. Majini kwa mujibu wa Uislamu

Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu majini ni viumbe ambao Allah aliwaumba
Baadhi yao ni Waislamu na wengine si Waislamu
Hii ni kwa mjibu wa Qur'an yenyewe

Qur’an, Suratul-Jinn 72:14 inasema:

Na hakika miongoni mwetu wapo Waislamu na miongoni mwetu wapo walio madhalimu
Basi wale waliosilimu, hao wameifuata njia iliyo sawa

Pia, Qur’an 55:15 inasema kwamba majini waliumbwa kutokana na mwali wa moto usio na moshi

Hivyo, kwa mujibu wa Qur’an, majini ni viumbe walioumbwa na Allah, na wanaweza kuwa na imani tofauti

Pia baadhi waislamu kuna wanaodai kwamba majini wanaweza kuwa marafiki wa binadamu, na wengine husema kwamba binadamu anaweza hata kushiriki nao ngono(Sex)

Hapo nimeweka rejea ya hizo Aya ili anataka akapitie mwenyewe kuona ukweli ulivyo

2. Mapepo kwa mujibu wa Ukristo

Kwa upande wa Wakristo, tunasikia kuhusu mapepo (demons)
Shetani na malaika walioasi, ambao wanahusishwa na uovu, majaribu na kuwapotosha wanadamu

Kwa mfano, 2 Petro 2:4 inazungumzia malaika waliotenda dhambi na hukumu yao
Pia, Ufunuo 12:7–9 inasimulia kuhusu Shetani na malaika zake kutupwa duniani

Hata hivyo kitu cha ajabu na cha kushangaza
Dini hizi zina mitazamo tofauti kuhusu hawa viumbe wa kiroho
Unaweza ukagundua tofauti iliyopo kwa MAJINI wa Kiislamu na MAPEPO ya wa Kristo

Tena Muslim wao hao majini wana mpaka majina

Ex: kuna majina ambayo tumekuwa tukiyasikia, kama Jini Subiani, Makata, Daruweshi, Sultani na Maimuna nk....

Kama kweli majini wapo kama vitabu vya dini vinavyosena je, kuna namna binadamu anaweza kuwaona au kukutana nao ana kwa ana?

Sasa wana JF mjadala wetu upo hapa 👇

Kama Mungu ndiye aliyewaumba, hakujua kama wataasi?
Kwa sababu Mungu hupewa sifa ya kujua vyote

Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ndiye aliyewaumba majini. Qur’an 7:27 inawaonya wanadamu kuhusu Shetani na kabila lake ikisema kwamba wao wanawaona wanadamu kutoka mahali ambapo wanadamu hawawezi kuwaona.

Sasa, kama Mungu ndiye aliyewaumba majini na ana ujuzi wa kila kitu, hakujua kwamba baadhi yao wangekengeuka na kuja kuwapotosha binadamu?

Kama alijua hilo kabla hawajaumbwa, kwa nini aliwaumba akijua kwamba baadhi yao wangeasi na kuwa chanzo cha upotoshaji kwa viumbe wengine?

Na kama alikuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo lisitokee, kwa nini hakulizuia tangu mwanzo?

Kwa upande wa Wakristo, Biblia pia inazungumzia malaika walioasi. Katika 2 Petro 2:4, malaika waliotenda dhambi wanatajwa pia

Sasa mkanganyiko kama Mungu aliumba malaika na anajua kila kitu kabla hakijatokea, hakujua kwamba baadhi yao wangeasi?
Kama alijua, kwa nini aliwaumba akijua mwisho wao ungekuwa huo?

Na kama alijua kwamba Shetani angekuja kuwashawishi na kuwapotosha wanadamu, kwa nini alimruhusu aendelee kuwepo na kufanya hivyo?

Kwa nini Mungu aruhusu uovu, halafu aadhibu wanaoufanya?

Kwa mujibu wa mafundisho mbalimbali ya dini, mwanadamu akifanya maovu akatenda dhambi anaweza kuhukumiwa na kuadhibiwa adhabu ya Jahannamu au moto wa milele katika baadhi ya mafundisho

Mimi nazidi kujiuliza

Kama Mungu alijua tangu mwanzo kwamba Shetani, majini au viumbe wengine wangeasi na kujaribu kuwapotosha wanadamu, kwa nini aliruhusu mfumo huo uwepo?

Kwa nini atuache katika mazingira yenye vishawishi na uwezekano wa kupotoshwa, halafu atuhukumu kwa kushindwa kuvishinda?

Kama Mungu ana uwezo wa kuzuia uovu, kwa nini anaruhusu uovu huo uwepo na baadaye kuwaadhibu wale wanaoufanya?

Je, binadamu ni sahihii kuingizwa kwenye mtego mkali hivi?

Na kama Mungu alijua matokeo yote kabla ya kuumba viumbe hivi, kwa nini hakupanga mfumo ambao uovu huo usingetokea, au ambao usingewaweka wanadamu katika hatari ya kupotoshwa?

Mwisho akaahidi kutuchoma moto?

Je, huu ni mtihani wa haki?

Tuchukulie mfano halisi kwamba mtu ametengeneza mfumo, anajua kila kitu kitakachotokea ndani ya mfumo huo kabla haujaanza, na ana uwezo wa kubadilisha matokeo yake
Lakini anaamua kuuacha uendelee, huku akijua kwamba baadhi ya watakaokuwa ndani yake wataanguka na kushindwa

Sasa, ikiwa Mungu ndiye aliyeumba mfumo mzima alijua mwisho wake tangu mwanzo na ana uwezo wa kuzuia matokeo fulani yasitokee, kosa la binadamu liko wapi hasa?

Kwa nini tuwekwe katika mazingira yenye uwezekano wa kupotoshwa na viumbe ambao Mungu mwenyewe alijua wangekengeuka, halafu tuhukumiwe kwa matokeo ya maamuzi yetu?

NB :Kama kweli Mungu yupo kwanini akaumba dunia kwa namna hii
Kwanini atuahidi moto na ni yeye alianzisha
Kosa letu binadamu liko wapi?

ShesRise_1 ✋️
Nikuulize swali moja tu wewe kama ni mwalimu unapompa mtihani/maswali mwanafunzi wako waga unajua majibu na kama unataka majibu kwanini unampa mtihani ambao wewe una majibu yake?
 
Nikuulize swali moja tu wewe kama ni mwalimu unapompa mtihani/maswali mwanafunzi wako waga unajua majibu na kama unataka majibu kwanini unampa mtihani ambao wewe una majibu yake?
Huu mfano hauendani
Mimi mwalimu nakua najua majibu ya maswali ya mtihani

Ila sijui mwanafunzi wangu atajibu nini
Tofauti na Mungu yeye anasema ana jua kila kitu yaani kila kitu hata unachowaza
 
sasa inakuwaje shetani akushawishi wewe hili na yule lile? Kumaanisha kwanini waovu wote hawakamatiki katika ovu moja au kwa kiwango kilekile?
Ndio maana ya ushawishi, kwa maana ingekuwa shetani ana power ya kulazimisha watu kutenda maovu basi ndio pengine tungeona watu wote wakitenda maovu aina moja au kwa kiwango kilekile. Watu tunatofautiana mengi hivyo hata huo ushawishi utategemea na huyo mtu.
 
Huu mfano hauendani
Mimi mwalimu nakua najua majibu ya maswali ya mtihani

Ila sijui mwanafunzi wangu atajibu nini
Tofauti na Mungu yeye anasema ana jua kila kitu yaani kila kitu hata unachowaza
Sasa hayo ya Mungu kujua kila kitu si ni ujuzi wake yeye ambao sisi hatuna, sasa sijui kwanini huwa mnajichanganya na hili jambo.
 
Sasa hayo ya Mungu kujua kila kitu si ni ujuzi wake yeye ambao sisi hatuna, sasa sijui kwanini huwa mnajichanganya na hili jambo.
Sasa Mungu analaumu nini na kuahidi kuwachoma moto kwa matokea ya vitu alivyounda mwenyewe?
 
Ndio maana ya ushawishi, kwa maana ingekuwa shetani ana power ya kulazimisha watu kutenda maovu basi ndio pengine tungeona watu wote wakitenda maovu aina moja au kwa kiwango kilekile. Watu tunatofautiana mengi hivyo hata huo ushawishi utategemea na huyo mtu.
unapojaribu kuelezea maadili kwa kuchomeka neno "shetani" utaishiwa maelezo hatua mbili tu.
mfano; wewe mwenyewe unajua kuna vitu huwezi shawishika kufanya hata aje "shetani" wa rangi gani. lakini pia anajua kuna wanaofanya hivyo. je unaweza kutuambia huyo shetani aliwashawishije hao ?
 
Back
Top Bottom