leipzig
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 2,766
- 1,716
Nilikuwa katika safari zangu za kawaida mara tukakuta kundi kubwa la askari barabarani, wengine wamevaa nguo nyeupe na wengine kijivu. Tulikuwa watu wengi tuliosimamishwa kati yetu walikuwepo wenye asili tofauti tofauti.
Katika kuulizwa maswali nilishangaa kuona wale wenye asili ya kizungu, kiarabu na kihindi wakaambiwa waondoke katika muda mfupi tu tukabaki waswahili, tumeulizwa maswali ya kijingajinga na wengine waliokuwa na haraka wakawapiga sindano hao askari, nadhani mmenielewa. Mimi nilikomaa mpaka mwisho hatimaye wakaniruhusu niondoke ijapokuwa walinitukana eti mimi mshamba.
Katika kuuliza nikaambiwa pale wanachangisha michango ya vikao vya ofisi na binafsi. Hivi mbona hii nchi imekuwa hivi tofauti na wakati huo? Nani wa kulaumiwa?n Na atairekebisha hii hali ya wageni kuonekana ni bora zaidi kuliko wazalendo?
Ikishindikana ni bora nipake mkorogo hadi niwe mweupe ili niondokane na kero hizi kwani wageni wanathaminiwa kuliko wazawa, sina maana ya Xenophobia.