Dennis Robert Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 5,986
- 9,493
Kuna mtu atasema kwanini usiangaike na katiba ya nchi yako Tanzania bali unaangaika na katiba ya kenya ambayo haikuhusu
Jibu ni kwamba lazima tujifunze kwa wale ambao wamekuwa wakijisifu na kwenye hili ntaongelea katiba ya kenya
Kabla sijaendelea Kuna mtu anaitwa morara kebaso ni mkenya mara nyingi sana huwa anaelezea namna miradi mingi sana kenya imetengewa fedha na haifanyiki na fedha hazijulikani zilipo sasa unajiuliza nchi inayosifiwa kuwa inakatiba nzuri sana iweje iwe na uozo kama huu ambao morara kebaso anauonyesha na mwingine hauonyeshi
Turudi kwenye heading katiba ya kenya iko overrated sana na ntakupa mapungufu ya katiba ya kenya

- Katiba haina historia ya kumchukulia hatua mwanasiasa yeyote yule mla rushwa sasa huwaga nashangaa watu wanaoisifia katiba ya kenya
- Katiba ya kenya imeshindwa kuaddress swala la ukabila kwenye kuchagua nafasi mbalimbali serikalini
- Katiba ya kenya imeendelea kuipa nairobi nguvu kubwa sana ya kisiasa na matokeo yake serikali ya kenya imewekeza nguvu kubwa sana kwenye jiji la nairobi huku sehemu nyingine ya nchi kama kaskazini mwa kenya kukiwa kama kutelekezwa
- Katiba imeongeza ukubwa wa serikal maradufu nchi kama kenya huwezi kuwa na mabunge mawili
- Mfumo wa uchaguzi wa kenya wa kumpata Rais ni mbovu sana hasa ukizingatia kenya ni nchi ambayo ina-ukabila mkali na kwa sababu ni mbovu imepelekea wewe kama ni mkikuyu una mchagua mtu wa kalenjini kama makamu mpaka hapa unakua na asilimia karibia 40 za kura za urais hizi 10+ unabangaiza huko kwingine, mfumo wa kuchagua urais wa kenya unatakiwa usibase tu kwenye popular vote bali uangalie na factor nyingine ili kukabiliana na ukabila
- Mahakama ya Kenya inasifiwa sana ila bado iko mifukoni mwa wanasiasa ni sawa na mbwa anabweka sana na hana madhara