BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
Ushahidi gani tena wanaokusanya toka kwa wananchi!? Wananchi wasiokuwa waajiriwa wa BoT hivi wanaweza kujua ushahidi wowote kuhusiana na ufisadi uliofanywa ndani ya BoT!?
Wataufahamu vipi ushahidi huo wakati mafisadi wameweka mapesa hayo katika bank accounts za nje ya nchi!? ushahidi wa kutosha upo tunachotaka kuona ni kufanyiwa kazi kwa ushahidi huo
Ama kweli Kikwete ni msanii wa hali ya juu!
Dk. Slaa ashtukia Kamati ya Kashfa ya EPA
==
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, ameeleza kushitushwa kwake na utaratibu wa kukusanya ushahidi unaotumiwa na Kamati ya Kuchunguza Kashfa ya EPA inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mwanyika.
Dk. Slaa, mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika na kinara wa harakati ya kuuanika ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katikati ya mwaka jana, aliyasema hayo jana kupitia katika ujumbe wa maandishi alioutuma kwa Tanzania Daima.
Kwa mujibu wa Slaa ambaye dhamira yake ya kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka kuundwa kwa Kamati ya Bunge kuichunguza BoT ilizimwa na Spika wa Bunge, utaratibu mzima uliotangazwa na kamati hiyo ya Mwanyika ni wa kutia shaka.
"Kamati ya Mwanyika, IGP Mwema na Hosea isifanye kiinimacho. Nimeshangazwa na utaratibu waliotangaza wa mtu kupeleka ushahidi kwa mjumbe mmoja mmoja wa kamati.
"Nikipeleka taarifa zangu, nina uhakika gani kama zitafikishwa kama zilivyo? Mimi nadhani kamati ilipaswa kufanya kazi kwa pamoja kama timu na si mtu mmoja mmoja," alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye hoja yake bungeni ilisababisha serikali ilazimike kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kuipa kampuni ya kimataifa, kazi ya kukagua upya hesabu za BoT za mwaka 2005/2006 alisema uchunguzi wowote katika sakata hili hauna budi kuanza kufanyika baada ya aliyekuwa gavana wa BoT, Daudi Ballali kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa.
Mbali ya hilo, alisema kwa kufuata utaratibu huo huo, aliyekuwa Waziri wa Fedha mwaka 2005, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja nao wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa.
"Siri zote za EPA na ufisadi wote wa BoT anazo Ballali. Kwa utaratibu huo huo wakamatwe Mramba na Mgonja na wahojiwe. Ndio waidhinishaji wakuu wa malipo yote ya serikali na wasimamizi wakuu. Serikali isiendelee kutufanya Watanzania wendawazimu," alisisitiza Dk. Slaa.
Akitoa mifano mingine kuhusu ufisadi ndani ya BoT, mwanasiasa huyo alieleza kushangazwa na kuendelea kusuasua kwa serikali katika kuchukua hatua katika masuala mengine ya ufisadi yaliyo nje ya EPA.
Alisema katika taarifa yake kuhusu ufisadi BoT, alishapata kuwasilisha tarehe na kiasi cha fedha kilichohamishwa kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwenye kampuni nyingine inayolalamikiwa ya Deep Green na namna zilivyopelekwa katika Benki ya NBC tawi la Corporate.
Slaa alisema, alitaja hata namba ya hundi iliyolipia malipo hayo na jinsi fedha taslimu zilivyochotwa.
"Bila hatua ya kuwakamata kwanza na kuwahoji wahusika hao, ni usanii. Ushahidi wa kwanza uko BRELA (wakala wa usajili wa makampuni) na pia katika taarifa ya Ernst & Young (taasisi ya ukaguzi wa kimataifa iliyogundua upotevu wa shilingi bilioni 133 kupitia akaunti ya EPA)," alisema Slaa.
Slaa anatoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Kamati ya Kuchunguza Ubadhirifu BoT inayoongozwa na Mwanyika, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuanza rasmi kwa uchunguzi wake.
Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa juzi na kuchapwa katika magazeti mbalimbali jana, kamati hiyo iliwaomba wananchi wenye taarifa zaidi zinazowezesha kusaidia uchunguzi kujitokeza na kutoa taarifa ama moja kwa moja kwa kamati au kwa kuwasiliana na mjumbe mmoja mmoja binafsi.
Kamati hiyo iliwahakikishia wananchi kuwa, kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini kwa nia ya kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana na kuwekwa hadharani, ili kulinda heshima ya taifa.
"Ili kuiwezesha timu kufanya kazi yake kwa uhakika, wananchi wanaombwa kuwa na subira na kutoa kila ushirikiano utakaoiwezesha kukamilisha majukumu yake.
"Utaratibu umewekwa wa kupokea taarifa hizo kupitia Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wananchi wenye taarifa hizi wazipeleke kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema kwa simu 0754 785 557.
"Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba simu 0754 206 326, Edward Hosea, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 763 741 au Lilian Mashaka, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 336 116," ilisema taarifa hiyo.
Soma, Pia
Mwaka 2008
Mwaka 2016

- Ripoti ya EPA Usanii: Ni Mpaka kikao Kijacho
- Kashfa ya EPA: Mwanyika azidi kujichanganya
- Washitakiwa wa EPA ni WATU waaina gani haswa...?
- Mauzauza ya EPA
- Vyuo vikuu watoa tamko juu ya EPA, Richmond
- Siri mpya EPA: Vigogo BoT waliamua 'kufa na mafisadi'
- Mpya: Tume ya Rais ya EPA yalonga
- Serikali yajiandaa kueleza marejesho fedha za EPA
- Wezi wa BoT - EPA warejesha bilioni 50 hadi leo
- UTATA wa MABILLIONI ya EPA: Ni kiasi gani kilichorudishwa na mafisadi?
- EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (2)
- Ufisadi wa EPA, Richmond wadhalilisha Watanzania Marekani
- Sakata za Richmond, EPA sasa kuhamia katika vikao vya CCM
- Hakimu Kisutu azuia waandishi kesi ya EPA
- Watuhumiwa EPA warushiana mpira kuhusu mgao wa mabilioni
- Sh60bn EPA cash set for Budget inclusion
- EPA billionaires shocked banker
- EPA yaikoroga CCM
- CCM wagombania pikipiki za "EPA"
- Slaa: Fedha za EPA kiinimacho
- Usanii katika kesi za EPA
- Jailed Tanzanian car thief now linked to EPA scandal
- Jeetu Patel: Kutoka kuuza vipuri hadi kuwa bilionea fisadi
- Mtuhumiwa wa EPA aandaa Harambee CCM katika hoteli ya Kempisky
- CAG: Ukaguzi wa EPA ulininyima usingizi
- Maranda ajihalalishia fedha zilizoibwa EPA
- Fedha za EPA zilikorudishwa zaliwa tena; Peter Noni wa EPA, Simon Group wa UDA ndani.
- Ushahidi Kagoda waitikisa Serikali
- Hukumu Kesi ya wizi wa bilioni 1.8 EPA kutolewa Aprili 29
- Upelelezi dhidi ya kina Lukaza Kesi ya EPA wahusisha Interpol
- Siri kashfa ya EPA hadharani
- Mahakama ya Kisutu yawahukumu wezi wa EPA, Maranda na Farijala miaka 22 jela
- Gavana abanwa fedha za EPA; Adai serikali pekee ndiyo inajua matumizi yake
- EPA Will Bring More Costs than Benefit - Mkapa
- JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA
- Polisi wahangaika kushughulikia tuhuma za Msemakweli kuhusu EPA, Manji na DPP
- Dr. Slaa makampuni yasiyorejesha pesa za EPA hadharani
- Dr. Slaa athibitisha EPA ni ya Mkapa Arumeru.
- Maranda's EPA Case Adjourned to June 25
- Wakili maarufu wa 'epa' afariki ghafla
- Ushahidi wa Mwigulu Nchemba kuhusika na EPA huu hapa
- Mshtakiwa wa epa na mwenzake jela miaka 18
- Kikwete: Fedha za EPA zitatumika kuanzisha benki ya wakulima
- Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi
- Documents za EPA: Tujikumbushe
- Mkapa: EPA Pacts will derail Africa
- Nape Nnauye alinufaika na pesa ya EPA
- MAAJABU YA JK: Atoa msamaha kwa mfungwa mmoja wa EPA wakati wengine 5 kawatosa
- Magereza yatoa ufafanuzi kuhusu mfungwa wa EPA
- Slaa: Jakaya Kikwete ana mkono EPA
- CAG Ludovick Utouh: Kigogo Epa alitenga rushwa bil.30/-
Mwaka 2016