Mzee Es,
Umesema kweli sana tu isipokuwa dhana za Mkapa siwezi kuzisikiliza. Kwa sababu mkosa hawezi kumtoa makosa mtu.. Ikiwa kweli mtu anaamini 2+2 ni 22 na mbishi kukubali jibu la @ kwani haoni uhusiano kati ya 2 na 4, huyu mtu hawezi kabisa kutoa ushauri wa maana. Mkapa bado anaamini jibu ni 22 na anachotegemea JK kufanya ni kuleta hilo jawabu ambalo kwa eli yake Mkapa haliwezekani na mtu isipokuwa yeye mwenyewe.
Tukirudi kwa JK mimi hofu yangu kubwa ni hawa jamaa wa mnadani ambao hawana sheria zaidi ya utajiri na hasa one way traffic ya biashara!..Hii ni kamali ya biashara inayotuhusiwa, utalishwa zako kwanzaaa kisha watafumua na tutarudi watupuuu!
Jasusi,
Mshikaji umesema yote!... Hii ndio hofu yangu kubwa na wala sio sisi hata mabepari wenyewe wanayaogopa mashika haya ya Mnadani tena toka nchi za nje, kwa sababu kazi yao kubwa ni kuvunja nguvu vijikampuni vyote vidogo nchini humo na kuushika uchumi wa nchi. Kazi yao kununua makampuni dhaifu hali makao makuu yapo US na soko lao lipo Nasdac - Marekani. JK aulize Canada wanavyolia, leo hii hawana hata sauti na hata serikali yao sasa hivi hawana budi kumsikia Marekani.
Sasa hiyo Dar stock exchange itakuwa na kitu gani? maanake nina hakika kitu cha kwanza kabisa watu hawa watayapigia speed mashirika yanayozalisha na yenye faida kubwa. Mafahari wengi watageuza TZ uwanja wa mapambano na sisi nyasi sijui kama tutabaki salama...
Naukubali sana ubepari iwapo sisi wenyewe tupo tayari na hasa ikiwa sisi ndio tutakao endesha mfumo huo yaani kuwepo na two way traffic ya kibiashara na nchi za nje. Na hii mikakati ya kuinua miradi midogo midogo (small business) ina mwisho mbaya sana kwa wananchi, tumewashindwa wahindi ambao ukifungua kitu tu wao wanajaza duka... Ebu angalia biashara ndogo ya muziki tu ambavyo wanawanyanyasa vijana. Master tape inanunuliwa kwa elfu 20 lakini hao wahindi wanatengeneza faida mara 1000 hali Bamuta wanao mtambo mzima wa ku - record na kufyatua toka enzi ya Mwalimu. Wamehakikisha haufanyi kazi za biashara zaidi ya mazoezi kwa Twanga pepeta.
Labda Jk kaona dawa ya moto ni moto!... ili kuwaondoa hawa wahindi na vitu vyao feki bora kumleta mnyonyaji na mwizi mwingine ambaye ataiba sawa na mhindi lakini tumebakiwa na majumba kama Maputo huko Msumbiji.