JF Kuwa Chama Tishio Cha Siasa?

JF Kuwa Chama Tishio Cha Siasa?

Jamiiforums Kugeuzwa Chama?

  • Yawezekana

    Votes: 44 71.0%
  • Haiwezekani

    Votes: 19 30.6%

  • Total voters
    62
  • Poll closed .
Mkuu X-Paster;

Sijakuelewa . . . . Unaweza kufafanua usemi wako?
 
Mimi mbona nisingekinyima hicho chama kura yangu, maana nisingedhubutu kutupa karata yangu ccm tena, "inafu izi inafu"

Shida yangu tu, ingebidi sasa kuwe na JF ya hiki chama kipya. Au makada ya ccm wangekiundia sasa JF yake, japo wao wasingedhubutu kama ilivyo kawaida yao kuongea openly, wangeendelea kulindana.

Shida nyingine ingekuwa "nguruwe wengine sasa wangekuwa more equal" hapa hapa JF.

Chama chochote kwa mwendo huu kinaweza kuendesha nchi, nilishasema zamani sana kuwa kumbe kuwa president ni jambo rahisi sana kama ninavyowaona marais wetu.

Viongozi wanafaya kama wanaoongoza kindergarten. But the end has come.
 
Nina pledge dollar 1000, za kuchapishia katiba na ilani ya uchaguzi watakazoandaa MKJJ na Rev.Kishoka.

Kama hayo machapisho yataandikwa kwa lugha za Kiswahili, Pundit na Nyani Ngabu tunawaomba msaidiane na waandishi ili ziende kwenye lugha ya dunia, I mean kiinglish!

Shy, Yo-yo, Yeboyebo, tunaomba nembo ya chama hiki.

Jmushi, Invisible, Maxcence na FMES, tunaomba muwe idara ya intelijinsia, hakikisheni katika member wa JF; EL, RA, BWM, Chenge,n.k hawaexist, la kama wamo wakubali tuwatume kazi yeyote! hasa za usafi wa ofisi yetu ambayo makao yake makuu yako Kigoma mjini! BMW atakuwa akishusha na kupandisha bendera ya chama kila siku asubuhi na jioni!

Nziku , Mkandara na MIMI waweka hazina

Kwanza tuanze kuunda kamati .......

Please propose jamani watu wengi sana humu na kila mtu anafaa!

waberoya
 
Kaka Allien,

Sijui wakati unapost hii thread ulikuwa serious kiasi gani au ulikuwa unatesti zali uone reaction. Basically, Inawezekana hakika inawezekana. Nakupongeza kwa wazo hili kwani tayari lishaanza kuchemsha damu za wanaJF. Target ya 2015 imetulia lets dare is very very possible.
 
JF kuwa chama cha siasa ni kupoteza mwelekeo. Wengine wetu sio washabiki wa siasa kihivyo, hivyo tutawapoteza. Wengine wetu tayari wana vyama vyao pia tutawapoteza.

Tayari JF imeshajijengea heshima ya aina yake. Tusijioneshe tumeanza kulewa heshima tuliojijengea kwa kutaka kujiaibisha na uchafu wa siasa. Politics is a dirty game!.

Kitu ambacho JF tunaweza kufanya ni kujigeuza kuwa Taasisi. Yaani Organization. Tumiliki magazeti yetu, redio zetu na televisheni zetu. Wana JF tusaidie kuijenga jamii kwa motoo ile ile " Where we Dare to Speak Openly.

Amini usiamini, hayo magazeti, Redio na TV zingekuwa funika bovu kwa Tanzania na ikipigwa media campaign kali kuwa JK mwisho wake, 2010, ukaleta wachambuzi wakachambua weakneneses zake na kusugggest mgombea mmbadala huku ukiwahakikishia umma, JK hafai na kama CCM itamkumbatia, nchi inakwenda kwa wapinzani, hata CCM, watamtosa na kumtafuta mwana CCM mwingine safi wa kuinusuru nchi na huku yakitimia yale maneno ya Baba wa Taifa " Rais bora ni lazima atatoka CCM".
 
Mkuu X-Paster;

Sijakuelewa . . . . Unaweza kufafanua usemi wako?


Unategemea nini...! kianzishwe chama sehemu ambayo watu ni wadini!?

Si kila siku kutakuwa ni magomvi na kushikana uchawi! We subiri utawaona tu, kama si kuwasoma...!
 
Tuweke tofauti za itikadi zetu ili tuweze kujadili hoja hii kwa mtizamo wa maslahi ya kitaifa.

Kwa hakika,JF ni mkusanyiko wa Watanzania lukuki wenye uchungu na nchi ya😵f course kuna wenzetu wanaokuja hapa kutekeleza majukumu ya KIKAZI lakini hata hao pia wamekuwa resourcefull kwa JF hasa pale wanapochokoza mada kwa ajili ya kupata data zaidi.

Hili la JF kugeuzwa chama cha siasa linawezekana,kinachohitajika ni utashi tu wa kisiasa na kuachana na pessimists ambao kwao kinachowezekana ni kile kilichopo tu i.e. vyama vilivyopo ulingoni hivi sasa.

Mtoa mada,uskiatishwe tamaa na pessimists,I do second your proposal na naamini kanisa we can do it.Tunaweza kukesha hapa for ages lakini tusibadilishe mambo huko nyumbani.It's high time now we act as a team.

Kuunga mkono mada pekee hakutoshi,and for that matter namwomba Invisible aangalie uwezekano wa kuwasiliana na Msajili wa vyama vya hiari,for a start,ili kui-register JF as a civil organisation,with a view to becoming a political party.

It can be done if we all play our parts.

If Obama could,in a racist Western world,why couldnt we in our own country?I say,YES WE CAN!
 
JF kuwa chama cha siasa ni kupoteza mwelekeo. Wengine wetu sio washabiki wa siasa kihivyo, hivyo tutawapoteza. Wengine wetu tayari wana vyama vyao pia tutawapoteza.
Tayari JF imeshajijengea heshima ya aina yake. Tusijioneshe tumeanza kulewa heshima tuliojijengea kwa kutaka kujiaibisha na uchafu wa siasa. Politics is a dirty game!.
Kitu ambacho JF tunaweza kufanya ni kujigeuza kuwa Taasisi. Yaani Organization. Tumiliki magazeti yetu, redio zetu na televisheni zetu. Wana JF tusaidie kuijenga jamii kwa motoo ile ile " Where we Dare to Speak Openly.
Amini usiamini, hayo magazeti, Redio na TV zingekuwa funika bovu kwa Tanzania na ikipigwa media campaign kali kuwa JK mwisho wake, 2010, ukaleta wachambuzi wakachambua weakneneses zake na kusugggest mgombea mmbadala huku ukiwahakikishia umma, JK hafai na kama CCM itamkumbatia, nchi inakwenda kwa wapinzani, hata CCM, watamtosa na kumtafuta mwana CCM mwingine safi wa kuinusuru nchi na huku yakitimia yale maneno ya Baba wa Taifa " Rais bora ni lazima atatoka CCM".

Pasco,are you happy kuingia JF kila siku na kukuta mafisadi wametenda hili au lile kuifilisi nchi yetu?Unadhani kelele pekee zinasaidia kuikomboa nchi yetu?Sikuelewi unaposema "wengine sio washabiki kihivyo"!Wewe na mimi ni Watanzania,and kuikomboa nchi yetu is not about being a shabiki or not,ni jukumu letu sote.

Two wrongs do not make a right.Media zikiboronga sio sababu ya sisi kama wana-JF kuchelewa kuleta mabadiliko ya kweli kwa nchi yetu.

Sababu tunayo na uwezo tunao,kinachohitajika sasa ni NIA tu.Trust me,kuna watu hapa wana uchungu wa dhati na nchi yetu.Tukiweza kukubaliana katika tofauti zetu za kiitikadi,na kufanya kila jitihada kudhibiti infiltration ya vibaraka,I'm 99.9% sure kwamba tunaweza kuunda chama cha kuleta mapinduzi ya kweli.Wengi wa tunaokuja hapa ni wahanga wa ufisadi,kwa namna moja au nyingine.Na ndio maana ukisoma reactions za members mbalimbali kuhusiana na ufisadi wa huko nyumbani,utagundua kwamba kuna watu wana uchungu kweli (na sio HASIRA pekee).

Hatuwezi kulazimishana lakini why dont we give this idea a chance?Tuna takriban mwaka na ushee wa kujiandaa.Pengine target isiwe kumwondoa JK bali kupata wawakilishi watakaotengeneza mazingira mazuri ya A GRAND REVOLUTION (sio coup d'etat) in years to come.
 
Nina pledge dollar 1000, za kuchapishia katiba na ilani ya uchaguzi watakazoandaa MKJJ na Rev.Kishoka.

Kama hayo machapisho yataandikwa kwa lugha za Kiswahili, Pundit na Nyani Ngabu tunawaomba msaidiane na waandishi ili ziende kwenye lugha ya dunia, I mean kiinglish!

Shy, Yo-yo, Yeboyebo, tunaomba nembo ya chama hiki.

Jmushi, Invisible, Maxcence na FMES, tunaomba muwe idara ya intelijinsia, hakikisheni katika member wa JF; EL, RA, BWM, Chenge,n.k hawaexist, la kama wamo wakubali tuwatume kazi yeyote! hasa za usafi wa ofisi yetu ambayo makao yake makuu yako Kigoma mjini! BMW atakuwa akishusha na kupandisha bendera ya chama kila siku asubuhi na jioni!

Nziku , Mkandara na MIMI waweka hazina

Kwanza tuanze kuunda kamati .......

Please propose jamani watu wengi sana humu na kila mtu anafaa!

waberoya

Wakuu . . . .

Hakuna lisilowezekana . . . . kama tu tukiamua

Mimi nashauri kwanza Kura ya Maoni ifanyike ili kujua kama wazo hili linakubalika.

Kisha likikubalika iundwe kamati . . . . .

Na hakuna kuonana kwanza . . . mambo yote online humu humu mpaka yawe yamekamilika . . . .

Viongozi wachaguliwewe humu humu, wauze sera zao na kuweka wazi records zao . . . .

Narudia, hakuna lisilowezekana kama tukiamua
 
Kaka Allien,

Sijui wakati unapost hii thread ulikuwa serious kiasi gani au ulikuwa unatesti zali uone reaction. Basically, Inawezekana hakika inawezekana. Nakupongeza kwa wazo hili kwani tayari lishaanza kuchemsha damu za wanaJF. Target ya 2015 imetulia lets dare is very very possible.

Hakuna cha utai hapa Mkulu . . . watu wamechoka na nyimbo za wanasiasa wetu . . . .

Watu wote makini kutoka kwenye vyama vya sasa vya kisiasa ambao wana uchungu na nchi hii wanakribishwa . . . No ubinafsi hapa. Masilahi ya taifa mbele . .

Wapinzani tumewaambia waungane . . . hawataki. Wanacheza Segere tu na sababu lukuki sizizo na maana wala tija.

CCM hawataki kujimegua . . . Mafisadi na Waoga wa mafisadi na hata mashujaa wachache wote wameamua kukumbatiana . . . kisa, wanaogopa kuloose . . . .

Sasa tumechoka!
 
Kitu ambacho JF tunaweza kufanya ni kujigeuza kuwa Taasisi. Yaani Organization. Tumiliki magazeti yetu, redio zetu na televisheni zetu. Wana JF tusaidie kuijenga jamii kwa motoo ile ile " Where we Dare to Speak Openly.

Amini usiamini, hayo magazeti, Redio na TV zingekuwa funika bovu kwa Tanzania na ikipigwa media campaign kali

Pasco . . . Groundwork kubwa imeshafanywa na kuna mambo yanatokea behind the curtains . . . .

Maelezo yote nayaunga mkono pia lakini hiyo haitoshi. Kuna taasisi zinafanya kazi nzuri sana kwa sasa hata media . . . But who cares?
 
Mimi naona labda sisi wana JF tungechagua chama kimoja au nyama tunavyoona vinafaa nn kuvi"endorse".....vikishaungana ili kuweza kukabiliana na CCM. Lakini endorsement iwe na "strings attached"......Ufisadi na Ubadhirifu ni mwiko na tamaa za kijinga jinga hazitokuwa na nafasi.
My Opinion.
 
Unategemea nini...! kianzishwe chama sehemu ambayo watu ni wadini!?

Si kila siku kutakuwa ni magomvi na kushikana uchawi! We subiri utawaona tu, kama si kuwasoma...![/SIZE]

Is the glass with water HALF EMPTY or HALF FULL . . . .

It is all in your mind.

You can decide to think positively or negatively . . . . If you want you can read Upinzani alioupata Mwl. Nyerere alipoanza harakati . . .

Tupishe Njia Tuupiteeee . . . . Tukishapita nyuma watajaza wenyewe . . .
 
Tuweke tofauti za itikadi zetu ili tuweze kujadili hoja hii kwa mtizamo wa maslahi ya kitaifa.

Kwa hakika,JF ni mkusanyiko wa Watanzania lukuki wenye uchungu na nchi ya😵f course kuna wenzetu wanaokuja hapa kutekeleza majukumu ya KIKAZI lakini hata hao pia wamekuwa resourcefull kwa JF hasa pale wanapochokoza mada kwa ajili ya kupata data zaidi.

Hili la JF kugeuzwa chama cha siasa linawezekana,kinachohitajika ni utashi tu wa kisiasa na kuachana na pessimists ambao kwao kinachowezekana ni kile kilichopo tu i.e. vyama vilivyopo ulingoni hivi sasa.

Mtoa mada,uskiatishwe tamaa na pessimists,I do second your proposal na naamini kanisa we can do it.Tunaweza kukesha hapa for ages lakini tusibadilishe mambo huko nyumbani.It's high time now we act as a team.

Kuunga mkono mada pekee hakutoshi,and for that matter namwomba Invisible aangalie uwezekano wa kuwasiliana na Msajili wa vyama vya hiari,for a start,ili kui-register JF as a civil organisation,with a view to becoming a political party.

It can be done if we all play our parts.

If Obama could,in a racist Western world,why couldnt we in our own country?I say,YES WE CAN!

You said it all . . . . Tuko pamoja!
 
Umenichekesha sana! Uzuri wenyewe, umesema kweli tupu!!


Your signature gives a different picture from your reaction . . . .

"Great spirits have always encountered violent opposition from mediocre minds...like you"

Kazi kwelikweli . . . bado tuna safari ndefu!
 
and I say YOU are DELUSIONAL! lol
tutakiitaje chama hicho
Chama cha Jamii Demokrasia, Maendeleo na Forums au?
 
Tumesikitishwa Sana . . . .
Tumenyanyaswa Sana . . .
Tumeonewa Sana . . . .
. . .

Rev. Kishoka . . . . tunaomba uanze kuandika rasimu ya katiba kisha tuletee hapa jamvini tuipitie . . . .

Mwanakijiji . . . . anza kutayarisha rasimu ya Ilani ya Uchaguzi

Kuhani . . . . Anza kuchambua chambua weaknesses za vyama vyote vya Kisiasa . . . .

Wana JF Wooote . . . . Tuanze kujiandaa kufanya kweli . . . . .

Tunahitaji mchango wa kila mwana JF ni nini hasa tufanye ili tufanikiwe kuunda Serikali Mwaka 2015 . . . . .

It reminds me of a Top Cat cartoon🙂 On a serious note, I'm pessimistic.
 
Wazo zuri sana kama litafanyiwa kazi.

Nashauri kupata jina la chama, katiba yake, na kuainisha organisation ya chama hicho kabla hamjachagua viongozi. Kuchagua viongozi iwe ni hatua ya kujaza nafasi zilizoainishwa. That is what I think should be a starting point.

Great Idea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom