Hiyo lebo ya conservative kuwa siasa kali mimi naikataa. Ni kali kivipi na kwa kipimo gani? Kwa sababu hata mimi conservative nawaona maliberali wa mlengo wa kushoto kabisa kuwa na siasa kali. Sasa kwa nini ukiwa Conservative unabatizwa kuwa na siasa kali? Hizo siasa kali ni zipi?
Nyani,
Naomba nijisahihishe kidogo kuhusiana na hivi viraka na vipachikwa vya Conservative, centrist na liberal.
Hizi ni kanuni kuu za ama itikadi au falsafa na zinaweza kuwepo katika chama kimoja chenye Itikadi moja.
Mfano, enzi za enzi, Kingunge na Paulo Sozigwa (pamoja na wengine) walijulikana kama conservatives wa CCM. Katika CCM kuna pande zote hizi tatu, wenye siasa kali (wakifuatia kila kitu kiimla na kwa nguvu za msukumo wa kijamaa), wenye siasa za kati (kina Mr. Win-Win situation), na kuna liberals (wanaokubaliana hata na vyama au siasa ambazo si za kimsingi za CCM kwa kutumia Itikadi na Falsafa).
Sasa basi, kwa kuwa sisi bado tunajijenga katika mchepuo wa vyama vingi, mfano wa Kitila wa Chadema ya Mtei, haukifanyi Chadema kuwa mlengo wa Kulia (Conservative) kwa kuwa msimo wa Chadema nyakati za Mtei, zilikuwa ni kupingana na CCM kwa kusema kuwa kama CCM ni wajamaa, basi wao Chadema ni Mabepari au Makabaila.
Sasa utakuta labda Mtei alikuwa ndio mwenyewe conservative, akisema watu binafsi washikilie uchumi, kodi za matajiri zipunguzwe, Makani akawa ni wa Kati akisema, no tuendelee kuwa na mashirika ya Serikali na kodi ziwe sawa kwa wananchi wote, then anakuja Kitila ambaye labda alikuwa akiegemea sana kufanana na CCM au kuwa the other extreme ya Mtei kwa kudai kodi ziongezwe, Serikali na watu binafsi wafanye ubia kuendesha uchumi.
Hivyo hakuna dhambi au kosa kwa mtu kuegemea upande ambao anauamini.
Swali langu la Mirengo enzi zile ilikuwa ni kujua, je kama tumekulia katika Ujamaa na KUjitegemea, je hivi vyama vipya vina siasa gani ambazo ni tofauti na CCM? je ni vya Kikomunisti, Kijamaa, Kibepari, Kikabaila au Mambosasa kama Kitila alivyosema kuwa Chadema ya Mbowe ndivyo ilivyo?
Sasa tukishabaini hivyo, ndipo unakuja kwenye sera, kama mfano wa kodi, je Chadema sera zao kwa mambo ya Ushuru na Kodi yatakuwa tofauti kabisa na CCM? je wataongeza viwango vya kodi, kufuta misamaha ya ushuru na kodi na kuhakikisha watu binafsi wanachangia kwa dhati ujenzi wa Taifa, au watafuata blue print ya CCM kwenye Uwekezaji?
Je Chadema, CUF au mwingine atakayechukua nchi ambaye si CCM (Hata kama itakuwa kutoka CCM) atakuwa na sera gani kuhusu masuala ya uwekezaji, mazingira, kilimo, biashara na madini?
Je watakuwa ni wenye mwamko wa kusema soko huria au soko dhibitiwa?
Sasa kutoka hapo, ndio tuanze tena kunyumbulisha ni nani katika chama au vyama ambavyo vinafanana kifalsafa na kiitikadi, ndiye conservative, centrist na liberal?
Its all about win win situation
😉