Grace Room Ministries yafungiwa

Grace Room Ministries yafungiwa

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,487
Reaction score
1,451
Kanisa la mchungaji maarufu Pastor Julienne Kabanda lafungiwa na RGB(Rwanda Governance Board).
Sababu zilitajwa kufutiwa vibali, kulitokana na kuendesha shughuli zisizoendana na zilizokuwa zikiendelea.

Inasemekana aliomba kuanzisha kituo cha kutoa misaada kwa wasiojiweza, na badae kuanzisha huduma za maombi.
Imebainika baada ya kuwa kituo hicho kiligeuzwa kanisa, mhusika alikuwa anakodi ukumbi, jambo ambalo kwa sasa, ni kinyume na taratibu za uendeshaji wa kanisa au sehemu ya maombi;

Amekuwa akituhumiwa kupotosha umma, baada ya kubainika anatangaza kufanya miujiza, ikiwemo kuponya ukimwi.
Video hapa pia, ni mwanadada alietoa ushuhuda wake, jinsi alivyoamini na kuomba akaweza kuandika meseji kutumia simu, huku hajawahi kukanyaga darasani hata siku moja.

Ni baada pia ya yeye kujipost na kudai ni mama wa mataifa.
 

Attachments

  • Aombewa na kuweza kuandika.mp4
    4.2 MB
Back
Top Bottom