QM,
Pamoja na maneno mazuri uliyosema hapo juu, bado hujahitismisha vizuri.Unadhani ipi ni ideal situation?
Hii mada inafurahisha sana maana ukianza kuijadili, mawazo na mitizamo ya kila aina inajitokeza:
1.Ni mzazi gani asiyetaka mwanae awe na maisha mazuri? Mara nyingi sana wazazi wa binti husumbuka na kufadhaika sana pale wanapoona au kuhisi kuwa binti anataka kuolewa na bwana asiye na mwelekeo kimaisha.Kuna baadhi inasemekana hata huwapiga interview hao wanaotaka kuposa na maswali na majibu ni kama hivi-
Q. una nyumba?
A.HAPANA
Q.UNA GARI
A.HAPANA
Q.UNA kazi , biashara (PESA)
A.HAPANA
Q.UNA DEGREE
A.HAPANA
Q.UNA DIPLOMA
A.HAPANA
Q. SASA HAPA UMEFUATA NINI?
Kwa maana nyingine mzazi anapima ni kwa vipi muoaji atamudu kuendesha familia kama hana kitu chochote hata angalu cheti ( elimu ni ufunguo wa maisha!)
Huu ni ukweli jamani hata tukikataa....
Negative.
Kama ni kweli wazazi wanauliza haya maswali kwa prospect in-laws wao, basi wanafanya kosa kubwa sana. Japokuwa ni kweli kwamba hakuna mzazi anayetaka mtoto wake apate shida ya uchumi kwenye maisha ya ndoa, lakini kumuhoji mkwe mtarajiwa ni dalili tosha ya udhaifu katika familia hiyo. Kwanza, kama ni mimi ndio nawekwa kitimoto na wazazi wa mke mtarajiwa na kuulizwa maswali ya aina hiyo, wazo la haraka haraka litakalonijia ni kuwa hii familia iko 'closed-minded' and 'dismantled'. To me, that's a straight up red-flag.
Kwa maana nyingine mzazi anapima ni kwa vipi muoaji atamudu kuendesha familia kama hana kitu chochote hata angalu cheti ( elimu ni ufunguo wa maisha!)
Kwa nini mzazi ndio apime? Kwa nini mapimo hayo yasifanywe kati ya wapendanao hao?
Mzazi wa binti kujadili jinsi gani mkwe mtarajiwa ataweza kumudu uendeshaji wa familia, ni dalili tosha ya "mzazi-ng'ang'anizi"...i.e. wale wazazi kutwa kucha wananusanusa ndani ya ndoa za watoto wao kutaka kujua kila kitu kinachoendelea humo. In my opinion, familia yenye wazazi wa aina hii ni familia ya kuiogopa kama 'ukoma.'
Unadhani ipi ni ideal situation?
Hili ndilo swali la msingi. Labda nili-rephrase kidogo hili lilete maana zaidi:-
Unadhani ni mbinu zipi zinafaa kutumika katika kutaka kujua financial situation za mwezi (both female and male) kabla ya kuji-commit fully?
For God's sake, wazazi hawapaswi kujihusisha kabisa (directly) kwenye majadiliano ya finances za watoto wao wanaotaka kuungana kindoa. The most they can do ni kujadiliana na mtoto wao kuhusu masuala haya. Lakini ku-cross over na kumchachafya kwa maswali mkwe mtarajiwa ni No No. Period. Of course, if it's really really necessary, mzazi atapaswa kum-feed mtoto wake mbinu/umuhimu wa kujua financial situation ya mwenzi wake kabla ya kuji-commit.
Tukirudi kwenye swali muhimu - kwa Tanzania sidhani kama ni kazi ngumu (kwa yeyote anayejali) kujua mwenzako ana uchumi wa aina gani. I mean, kuna ugumu gani kujua kama bwana wako ana nyumba au hana, ana kazi au hana? Labda pengine unaweza usijue kirahisi kama ana kisomo na/au akaunti yake benki ina hela, lakini as time turns the pages utajua tu sooner.
Ninaamini wale wadada wanaodanganywa (na wanaume kuwa wana nyumba na kazi mzuri, wakati hawana) ni upumbavu wao tu na/au tamaa zao ndizo zinazowafanya wawekwa sawa kirahisi. Mwanaume hawezi kukudanganya kuwa anaishi kwenye nyumba yake Sinza, halafu kila siku mnakutana baa na kuishia gesti huko Temeke AU hawezi kukudanganya anafanya kazi hazina, halafu kila siku mnakutana mida ya kazi Tabata relini. I mean, where is the conciusness?