Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 23,434
- 28,779
Jeshi la Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) limekabiliwa na ukosoaji mkali baada ya kufyatua mabomu ya machozi dhidi ya maaskofu, mapadri na waseminari wa Kanisa Katoliki waliokuwa katika maandamano ya amani kudai ardhi ya kanisa mjini Lubumbashi . Maafisa wa polisi waliuzuia msafara huo karibu na seminari kuu ya Saint-Paul katika eneo la Pengapenga wakati viongozi hao wa dini wakiandamana kudai utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuhusu ardhi ya eneo la Tshamalale katika tarafa ya Annexe, huku video zikisambaa mitandaoni zikionyesha maaskofu na mapadri wakiwa wameshikilia misalaba na kuendelea kusali katikati ya moshi mzito wa mabomu ya machozi. Akilaani vikali hatua hiyo, Askofu Désiré Lenge wa Kilwa-Kasenga alisema: "Tunajiuliza tumefanya dhambi gani. Yalikuwa maandamano ya amani, na hiyo ni haki katika demokrasia. Hatujui tuko katika nchi ya aina gani,"
#KIMBELE_MBELE.
#KIMBELE_MBELE.